JINSI MAJINI WA UGANGA/UCHAWI WANAVYO SHIRIKIANA NA BINADAMU.
Nimesha sema hapo juu kwamba sio kila jini anajua KILA kitu.
Sio kila jini anaweza kufanya KILA kitu.
Sio kila jini ana maarifa makubwa kuliko KILA.mtu.
Sio kila jini anaweza kufanya KILA kitu KWA KILA mtu.
Sio KILA jini anajua yatakayo tokea siku za usoni. Mfano Mfalme Suleiman alifanya kazi zake KWA kishirikina na majini.
Miongoni mwa walinzi wake walikuwa ni majini.
Mfalme Suleiman alipo fariki, HADI inafika siku ya tatu tangu Mfalme Suleiman afariki bado jini anae mlinda alikuwa hajui kama bwana wake amesha fariki toka enzi za Pontyo wa Pilato.
So inakuwaje kwenye uganga.
Bwana
Kiranga Wewe ndo huyo umeenda KWA mganga
Mshana Jr unataka kumuua kichawi ndugu
DeepPond kea sababu amekuchukulia nyumba ndogo YAKO.
Bwana Mganga atawapa majini wake wa uganga kazi ya kumuua deep pond.
Tatizo ni kwamba majini wa Mshana hawana maarifa ya kuua mtu.
Lakini wanajuana na majini ambao Wana maarifa ya kuua mtu na wapo tayari kuua mtu.
Jini wa uganga wa Mshana, atamwambia Mshana nitakuletea taarifa ya kitu gani cha kufanya ifikapo saa saba usiku.
Jini wa uganga wa Mshana ataenda KWA majini wenzake ambao Wana maarifa ya kuua atawaambia ndugu zangu eeh nisaidieni kufanya kazi ya kumuua mwanadamu.
Hao majini wauaji wataomba majina ya huyo mtu anae takiwa kuuwawa.
Tatizo kwao nao ni moja hawana maarifa ya kupiga ramli na hawazijui details zote kuhusu binadamu wao wanacho jua ni kuua.
Ila na wao anajuana na jini mwenye maarifa ya falakh.
Wata enda KWA jini mwenye maarifa ya falakh.
Kazi ya huyu jini mwenye maarifa ya falakh ni kusoma nyota ya huyo mtu anae takiwa kuuwawa ILI kuangalia ILI operation ya kumuua mtu huyo ifanikiwe inatakiwa ifanyike siku GANI saa ngapi na eneo gani ( ardhini, angani, au kwenye maji)
Pia atatazama kama mtu huyo ana kinga na je kinga hiyo ni ya kijini au ya Mungu. Na kama.ni ya kijini wanatakiwa wafanye kitu GANI ILI kuidhoofisha hiyo kinga au kuua hiyo kinga kabla ya kupeleka shambulizi.
Huyu jini wa ramli huheshimiwa sana na hawa majini wauaji kama anavyo heshima gun supplier na ma armed robbers.
Huyu jini wa falaq akisha fanya intelligence analysis kuhusu mtu husika anatoa intelligence report ambayo itatumiwa na hao majini wauaji kama road map ya kwenda kumuua huyo binadamu husika
( Mara nyingi majini wanapo enda kumshambulia mtu bila kumconsult jini wa falaq huwa wanakuwa defeated na wanapokuwa defeated hurudisha taarifa KWA aliye watuma kwamba wamemshindwa mhusika.. hii HUTOKEA mara nyingi KWA WATU ambao kinga zao hazionekani na macho ya kichawi au macho ya kijini.. hapa hawa majini wataenda kichwa kichwa na mwisho wa siku wanakuwa defeated. The defeat is always not a good one for the djinn most of the time huwa ni kifo..ndio maana majini wakitumwa kumshambulia mtu wakakuta kinga yake ni kali BASI humrudia alie watuma na kumuua/ kufa nae)
SASA BASI huyu jini wa falaq anaweza kutoa report kwamba ili huyu deep pond auwawe lazima shambulizi dhidi yake KIFANYIKE akiwa ndani ya maji.
Na hawa majini walio pewa kazi ya kumuua deep pond wao territory yao ipo nchi kavu. Hawawezi kufanya chochote ndani ya maji
Watarudisha taarifa KWA jini wa uganga wa Mshana kwamba hiyo kazi hawawezi kuifanya wao KWA sababu mhusika anatakiwa auwawe akiwa ndani ya maji na wao hawana nguvu ya kufanya chochote ndani ya maji so wata mtefer jini wa uganga wa Mshana kwa jini muuaji ambae anaishi ndani ya maji.
Jini muuaji wa majini atachukua hiyo kazi lakini tatizo yeye hana uwezo wa kumvuta Deep Pond HADI pwani au majini.
Atatafutwa jini mwingine mwenye uwezo wa kumvuta Deep pond HADI ndani ya maji.
Jini wa falaq KWA sababu anakuwa tayari amemsoma Deep Pond anapenda vitu gani, atatoa ushauri kwamba jini pekee anaeweza kumvuta Deep pond HADI BAHARINI ni jini ashkhi majununi/ jini wa askhi na mapenzi.
Kumbuka hapo jini wa falaq alisha soma nafsi ya deep pond na kubaini kwamba Deep pond anatamani sana penzi la
Nifah . Amesha omba mara kibao kutoka na Nifah lakini Nifah anamzingua.
KWA hiyo Jini wa Falaq atashauri kwamba huyu jini wa Mahaba aombe kuingia ndani ya moyo wa Hanifa amuwekee wazo la kutaka kukutana na Deep Pond lakini lazima wakutane Coco Beach.
Jini askhi akiingia ndani ya moyo wa Nifah, Nifah atapata ghafla wazo la Mahaba kwa Deep Pond.
Kwa kuwa nature ya mwanamke sio kutongoza mwanaume na majini hawana uwezo wa kufanya kazi kinyume na nature, Nifah atamtext Deep Pond kwamba ana hamu ya
Kula mihogo ya Coco Beach.
Deep pond hatoamini anacho kiona, KWANZA atanitumia Nifah hela ya nauli na ya kutolea halafu atawasha gari fasta kwenda coco Beach.
Wakifika coco Beach kea furaha ya kukutana na.Nifah, Deep Pond atalewa sana halafu baadae ataomuomba Nifah waende kuogelea.
Kumbuka kule ndani ya bahari kuna jini muuaji ametegwa anamsubiri Deep pond aingie BAHARINi.
Deep pond akiingia BAHARINi huyo jini muuaji wa BAHARINi ata mzamisha deep pond ndani ya bahari na habari utaishia hapo.
KWA hiyo umeona hapo kwenye task moja wamehusika zaidi ya majini watano.
Uliza chochote unacho taka kukijua kuhusu majini.