Miezi michache iliyopita kumekuwa na mikwaju mizito ikielekezwa kwa uislam. Hasa suala lankutumia lugha katika ibada. Mpaka ikaonekana kwamba uislam siyo dini, bali ni chombo au mpango wa waarabu kueneza tamaduni, mila na desturi zao. Hivyo siyo dini bali ni utaratibu jumla wa maisha wa tamaduni za wengine.
Pia lingine ambalo watu wengi wameanza kulimulika ni ile hali ya chombo hiki kuwa sura ya uana harakati au upigania uhuru. Uislam ulivyo unajitanabaisha na harakati za kudai uhuru/haki maeneo mbali mbali duniani. Tofauti na tulivyokuwa tukitarajia uislam uwe kwa kuwaelekeza waumini wake kwenye maisha ya peponi baada ya haya. Wenyewe sasa wanawaendeleza maandamano na migogoro na mamlaka. Wakitaka haki na uhuru wao. Wakilazimisha sheria za nchi ambako wanaishi ziibadili sheria na kuongoza nchi hizo kwa sharia law. Kitu ambacho dini zingine hazijawahi kufanya.
Baada ya kuyaona hayo, nchi nyingi sasa hazichukulii uislam kama dini (kama waumini wake wanavyodai), bali ni mpango au chombo cha (wanaharakati cha) kupigania uhuru na haki ya waislam/waarabu kwa njia ya kipekee (exclusive right). Wanataka mahali popote wanapoishi wapewe uhuru/haki zao katika njia ambayo wengine hawawezi kupata. Wanataka wapewe special attention na mamlaka ya nchi husika. Hata kama kufanya hivyo kunaweza kwa hali au namna fulani kuathiri haki, uhuru, mamlaka na ustawi wa wengine.
Ndiyo maana mara zote nimekuwa nikiwa dhidi ya wazo la kwamba uislam ni dini. Kwa sababu nilizozitaja. Hiyo ni desturi yaani zaidi ya dini. Binafsi nawafananisha na wamasai. Wamasai licha ya kuwa wana ishi katika nchi zenye serikali yaani Jamhuri. Lakini bado wana utaratibu au namna yao ya utawala, siasa, imani (beliefs), lugha, sheria, mavazi nk. Pia jamii hii popote ikienda, lazima kuwe na msuguano na jamii walioikuta kwa kuwa siku zote wanaamini utamaduni wao ni bora kuliko wa wengine. Hili nilo mfanano dhahili wa uislam (yaani desturi za waarabu) na wamasai.
Naomba niishie hapa.
Alamsiki