Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,221
- 2,359
Kudai CCM hawataki uwepo Katiba bora ni upotoshaji vinginevyo 1914 wasingekubali kuanza kwa mchakato. Na tutambue mchakato ulianza kukiwa na wabunge wengi wa upinzani wakiongozwa na Chadema, kwa kuunda sheria ya kuongoza mchakato wenyewe iliyoridhiwa na wabunge wote.Ccm wanadumu kwa kutumia huu ujinga na kwa kupitia dola wameendelea kutisha watu kuwa upinzani si kitu.
Wanakataa vitu vya msingi kama katiba bora na tume huru ya uchaguzi bila kujua kwamba hivyo vitawafanya waendelee kuwepo.
Hatari iliyopo ni kuwa ikiwa itatokea chama kingine kikashinda kwa katiba hii na tume hii na kikatawala kwa mfumo huo ccm itafutika kama KANU na UNIP vilivyofutika huko Kenya na Zambia.
Sheria pamoja na mambo mengine ilielekeza lini/kipi kianze na lini/kipi kitaishia na lini ianze kitumika. Tunajua ninì kilitokea kwa sababu ya wanasiasa kujali masilahi yao badala ya katiba bora.
Na hata sasa CCM Wanapotoa fulsa ya wa majadiliano kuangaĺia namna ya kukwamua mkwamo wa 2014, wanasiasa maslahi wanashinikiza yao ya kisiasa na hawataki mijadala.
Katiba ni ya wananchi lazima kuwe na uongozi wa kutoa dira ya LINI kwa MAMNA GANI kulingana na mazingira ya sasa na Uwekezaji, unaweza kutupatia Katiba bora.
Katiba sio dodo unaloweza okota kwa kudondoka toka mtini. Ni mchakato wa zaidi ya miaka minne hadi itumike.