Huu Mkataba siyo Intergovernmental, Dubai siyo Nchi

Hujui makubaliano yao yakoje, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar huwa inasaini mikataba ya kimataifa kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kukubaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Wakishakubaliwa hawahitaji kuonesha kwenye mkataba kwamba wamekubaliwa, kwa sababu hilo ni suala kati ya SMZ na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.Sasa hivi wamesaini mkataba na Wafaransa kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wafaransa kuendeleza Bandari.

Hiyo point yako si material, ndiyo maana hata TLS hawajaitaja.
 
Umeleza mkuu vizuri, lakini Dubai siyo kama Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi ikaungana na nchi nyingine kama ilivyokuwa Czech na Slovakia. Dubai ni mkoa toka awali ndani ya UAE, ninamashaka sana kama kweli walisaini mkataba wa IGA na Dubai.
 
Whether Dubai ilikuwa nchi ikaungana na Emirates nyingine na kuwa jimbo la UAE, au ni jimbo la UAE tangu awali is immaterial.Si muhimu.

Kitu muhimu ni kwamba, Je, Dubai ina idhini kutoka kwa UAE kusaini mkataba huu?

Ikiwa Dubai ina idhini ya UAE kusaini mkataba huu, hoja ya kwamba Dubai haina nguvu za kusaini mkataba huu inavunjika, kwa sababu idhini ya UAE inaifanya Dubai iweze kusaini mkataba huu.

Na mpaka sasa hatujui kama Dubai ina au haina idhini ya UAE kusaini mkataba huu, na Dubai watakuwa wajinga sana kufanya biashara kubwa hivi bila hiyo idhini.

TLS wenyewe wamesema hili suala linahitaji mtu anayejua mambo ya UAE, kwa sababu si kila kitu kinawekwa wazi, kuna mambo mengine yanawekwa siri strategically.

Tujadili mapungufu ya mkataba, hoja ya kwamba Dubai haina nguvu ya kusaini mkataba ni hoja tata, TLS wenyewe wamesema hilo katika uchambuzi wao, tuna gap of information ambayo inatufanya tusiweze kujadili hili na kufikia conclusion either way, lakini all logic seems to indicate Dubai wamepata idhini ya UAE, hawawezi kufanya biashara kubwa hivi bila idhini hiyo.
 
Mh! Kwani mkataba ni baina ya Tanzania na Dubai au Tanzania na DPW?
 
Mh! Kwani mkataba ni baina ya Tanzania na Dubai au Tanzania na DPW?
Intergovernmental Agreement ni kati ya Dubai na Tanzania, DPW ni kampuni ya serikali ya Dubai.

DPW haiwezi kufanya intergovernmental agreement, kwa sababu DPW si government, ni kampuni.
 
Intergovernmental Agreement ni kati ya Dubai na Tanzania, DPW ni kampuni ya serikali ya Dubai.

DPW haiwezi kufanya intergovernmental agreement, kwa sababu DPW si government, ni kampuni.
Mtia saini kwa upande wa Dubai (KAMA NCHI) ni nani? Maana kwa Tanzania ni waziri wa JMT!
 
Mtia saini kwa upande wa Dubai (KAMA NCHI) ni nani? Maana kwa Tanzania ni waziri wa JMT!
Mtia saini si muhimu, kwa sababu anaweza kuwa deputized. Kitu muhimu ni mkataba unasemasemaje, ni mkataba wa nini? Aanatia saini kwa niaba ya nani?

IGA ipo hapa

Upande wa Dubai ametia saini CEO wa Ports Customs and Free Zone Corporation, for the Emirate of Dubai.
 
Oukey. Kwa hiyo huyo CEO ameiwakilisha nchi gani?
 
Hakuna nchi Dunia ijulikanayo kama Emirate of Dubai.
Intergovernment agreement si lazima iwe ya nchi na nchi, usichanganye international agreement na intergovernment agreement.

Hata serikali ya kijiji inaweza kusaini intergovernment agreement na serikali nyingine ya kijiji.

Na kama serikali hiyo ya kijiji ikipata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi, serikali hiyo ya kijiji inaweza kusaini intergovernment agreement na nchi ya kigeni.

Usichanganye intergovernment agreement na international agreement, you don't need to be a nation to have a government.

Kuna serikali za majimbo, mikoa, semi-autonomous parts of nations kama Zanzibar.

Zanzibar nayo si nchi, lakini inaweza ku sign intergovernment agreement na nchi za nje ikipata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikli ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Usichanganye government na nation, unaweza kuwa na government bila ya kuwa na nation.
 
Na kama serikali hiyo ya kijiji ikipata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi, serikali hiyo ya kijiji inaweza kusaini intergovernment agreement na nchi ya kigeni.
Hapa sasa, nionyeshe idhini ya kinchi inayompa mamlaka hiyo huyo CEO
 
Nimekwenda Leo bandarini hapa DSM hawa DPWORLD hawana mitambo ila wananunua mitambo ya TICS iliwaweze kufanya kazi,Mimi nawauliza hawa wanaosema wanakuja kurahisisha kazi mbona mitambo yenyewe ni chakavu?Lakini pia Kwa nini waanze kazi wakati Mikataba midogomidogo haijasainiwa?
 
Umeleza mkuu vizuri, lakini Dubai siyo kama Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi ikaungana na nchi nyingine kama ilivyokuwa Czech na Slovakia. Dubai ni mkoa toka awali ndani ya UAE, ninamashaka sana kama kweli walisaini mkataba wa IGA na Dubai.
Dubai ilikuwa nchi inayojitegemea kabla ya kuungana na nchi nadhani saba kuunda United Arab Emirates.
 
Na kama serikali hiyo ya kijiji ikipata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi, serikali hiyo ya kijiji inaweza kusaini intergovernment agreement na nchi ya kigeni.
Hapa sasa, nionyeshe idhini ya kinchi inayompa mamlaka hiyo huyo CEO
Soma uchambuzi wa Tanganyika Law Society, hayo ni mambo ya ndani ya nchi na wanayajua wao wenyewe, na pengine hawataki kuweka wazi kwa sababu zao.

Ukibisha na kusema Dubai hawajapata idhini, wewe ndiye utatakiwa kuonesha hawana hiyo idhini, na wao si wajinga kusaini mkataba huu.

Hoja yenu imejengwa kwa msingi unaoweza kukanushwa na barua moja tu ya kutoka serikali ya UAE kusema kwamba imeidhinisha Serikali ya Dubai na DPW kuingia intergovernment agreement.

TLS wamesema hili ni suala tata na linahitaji mtu aliye insider Dubai/UAE ku verify.

You are building an argument on flimsy information.
 
Good. So, we need verification. What if no?
 
Good. So, we need verification. What if no?
If no, hakutakuwa na tatizo mpaka serikali ya UAE ilete matatizo.

Zanzibar ilijiunga na OIC, hakukuwa na tatizo mpaka serikali ya Muungano ilipoingilia kati na kusema kwamba Zanzibar haikutakiwa kuingia katika OIC.

Bila ya serikali ya Muungano ku raise objectiin, Zanzibar ilikuwa ishajiunga.

So, first of all, Dubai watakuwa wajinga sana kuingia makubaliano bila idhini ya UAE.

Hapa kuna research inayoonesha jinsi UAE inavyotumia DPW strategically.

There is no way Dubai na DPW hawajapata idhini ya UAE kufanya hiki deal, hawa wanafanya kazi pamoja.

You can make an academic argument kwamba inawezekana Dubai hawana idhininya UAE, but the practical reality points otherwise.

UAE imepitisha sheria kabisa ku boost biashara ya bandari through DPW, haiyumkiniki wasiiruhusu Dubai kufanya hili deal.

Soma hapa.

Ndugu mimi ni muumuni wa uchumi huru, serikali za kiafrika zimefeli kuendesha hata mashirika muhimu kwa usalama (mfano nishati). Africa ya kusini wanahangaika na shirika lao (kwangu mimi ni uafrika ndio tatizo). Kuleta muwekezaji bandari ili kuongeza tija kwa nchi hapo hakuna tatizo. Tatizo ni lilelile la muda wote kuwa wawekezaji wa nje ndio jibu letu ( kwa mfano umeona mwenyewe UAE wanatumia kimkakati DPW!) Hiyo mikakati kwa kawaida ni kwa usalama na faida yao kwanza!.
Kama DPW inatumiwa kimkakati, kwanini sasa tuseme wamekuja tu kuongeza tija kwetu? Vipi mikakati hiyo ya UAE ikiwa ni hatari kwetu ( kupoka uhuru wetu?) Kwanini utata huu (ambao hata wewe umewanukuu TLS) usitatuliwe kwanza na mengine mengi yanayopigiwa kelele na wenye nchi (kama KWELI ni wenye NCHI) yasitatuliwe?
Nchi imegawanyika katika hili (na historia ya nyuma ni mwalimu mzuri), kwanini tuende tu na migawanyiko hii? Kumbe Zanzibar ilikosea ila kosa hilo lilikuwa linawapa faida Zanzibar ila hatari kwa muungano! Vipi ikiwa DPW wamekosea ila kosa hilo linawapa faida wao wenyewe na UAE na hatari kwetu, unadhani UAE watakuja ku- claim? (Kumbe ndo ile maana ya hata uhusiano wa kidiplomasia ukiharibika baina ya nchi huu MKATABA hauvunjiki!)..maana siku tukijajua tuliingizwa chaka kuwa Dubai ni nchi na tukaanza kupishana na UAE, mkataba utaendelea kutudunda tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…