Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Sijui hata inaandikwaje.
Ni Sukuma Gang, Sukuma gang, au Sukumagang?
Mtajaza wenyewe.
Wangapi wengine mmegundua kama mimi kuwa huo msamiati sasa hautumiki tena?
Kuna kipindi humu baadhi ya watu tuliandamwa sana.
Ilikuwa popote pale tukitia neno, hujibiwi kwa hoja.
Ilikuwa unakuwa dismissed tu kuwa wewe ni Sukuma Gang, hata kama hoja uliyonayo ina mashiko.
Marekani tokea 2016 kuna TDS [Trump derangement syndrome]. Nasi hapa kwetu tokea 2015 mpaka 2022 hivi, kulikuwepo na Magufuli derangement syndrome [MDS].
Kwa ufupi ni kwamba, hao watu wenye MDS tuliwaonya, tuliwafahamisha, na tukawatahadharisha kuwa tatizo la msingi wala halikuwa ni mtu [Rais Magufuli] bali lilikuwa ni CCM.
Tulifanya hivyo kwa kuangalia tulikotoka kabla ya ujio wa Magufuli na kuona kuwa kuna mambo ambayo yalikuwepo kabla yake na yakaendelea kuwepo wakati wake na sasa bado yapo na yanaendelea baada ya uwepo wake.
Ilikuwa ukiwaambia hao wagonjwa wa MDS kuwa mbona hayo mambo mnayomlaumu Magufuli yamekuwepo tokea siku nyingi, ilikuwa ni sawa na kuchokoza nyuki.
Ilikuwa unashukiwa na ghadhabu za raia utadhani umetenda dhambi isiyosameheka.
Sasa ni kipi kilichobadilika? Jibu ni muda!
Muda haujawahi kushindwa hata kidogo. Haujawahi kushindwa katika kuelezea au kuonyesha kitu au jambo.
Mwanzoni mwa utawala wake alisifiwa sana.
Sifa kem kem toka kila pande 🤣.
Tuliambiwa hafoki, hatumbui, hateki watu, hana kauli mbaya, na kadhalika.
Tukaonyeshwa na ushahidi wa matokeo ya hizo sifa: halindwi na maaskari wenye bunduki za kivita kama yule dikteta Msukuma.
Tulio na busara na hekima tukawaonya kuwa ni mapema mno kuanza kutoa mahitimisho ya namna hiyo.
Tukaishia kupuuzwa, kuchekwa, na kuitwa ma-Sukuma gang tulio na machungu ya kufiwa.
Haya, peleka muda mbele mpaka leo hii, zaidi ya miaka minne tokea Msukuma arudishe namba…..
Akina nani ndo wamekuwa wa mwisho kucheka na akina nani ndo wanaolia na kusaga meno leo?
Schadenfreude, for now, is my new favorite word…….that is if you’re picking up what I’m putting down 😉.
Happy Sunday and happy Memorial Day weekend for those in the US 🇺🇸.