Huu mtindo wa Rais kujifichia kwenye kamati/ kikosi kazi unaitwaje kitaalamu?

Huu mtindo wa Rais kujifichia kwenye kamati/ kikosi kazi unaitwaje kitaalamu?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Tumeona maamuzi kadhaa ya kitaifa hivi karibuni yamekuwa yakitolewa kupitia uundwaji wa tume, kamati na vikosi kazi.

Tunaona imeundwa timu ya kuangalia kanuni za kuendesha mikutano ya siasa

Baadae kidogo tunaona kuna kikosi kazi cha kuangalia tume huru na kushauri kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.

Mbali na vikosi kutokuwepo kisheria, bado baadhi ya vitu ni ukiukwaji wa sheria.

Kwa jicho la 3 naona huu uundaji wa vikosi kazi ni kutafuta endorsement tu.

Rais anajifichia kwenye vikosi kazi ili ikitokea shida mbeleni ionekane ni vikosi kazi ndio vimeshauri vibaya.

Hii mbinu hutumiwa sana na mawaziri na viongozi ngazi za mikoa.

Wakiwa na mambo yao wanayapitisha kwa menejimenti yapewe baraka ili ikibumbuluka inaonekana ni menejimenti ilimshauri vibaya kwa hivyo yeye anakuwa hawajibiki.

My Take

Tumshauri Rais asimame yeye kama yeye kama mkuu wa nchi badala ya kujifichia kwenye vikosi kazi
 
Hivi Kwanini anaogopa Katiba?
Nitaamini km weak mara tu baada ya wewe kwenda kumtoa! Lkn km unapiga kelele hz kwa ujanja wa kuiga huku ukiwa zako hukoo nanjilinji, basi wewe ni the most miserable!
 
Tumeona maamuzi kadhaa ya kitaifa hivi karibuni yamekuwa yakitolewa kupitia uundwaji wa tume,kamati na vikosi kazi.

Tunaona imeundwa timu ya kuangalia kanuni za kuendesha mikutano ya siasa

Baadae kidogo tunaona kuna kikosi kazi cha kuangalia tume huru na kushauri kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.

Mbali na vikosi kutokuwepo kisheria,bado baadhi ya vitu ni ukiukwaji wa sheria.

Kwa jicho la 3 naona huu uundaji wa vikosi kazi ni kutafuta endorsement tu.

Rais anajifichia kwenye vikosi kazi ili ikitokea shida mbeleni ionekane ni vikosi kazi ndio vimeshauri vibaya.

Hii mbinu hutumiwa sana na mawaziri na viongozi ngazi za mikoa.

Wakiwa na mambo yao wanayapitisha kwa menejimenti yapewe baraka ili ikibumbuluka inaonekana ni menejimenti ilimshauri vibaya kwa hivyo yeye anakuwa hawajibiki.

My Take

Tumshauri Rais asimame yeye kama yeye kama mkuu wa nchi badala ya kujifichia kwenye vikosi kazi
She is trying to run but she cant hide.

The rocks are boiling.

Katiba Mpya ni sasa.
 
Na wameambiwa wasifanye lolote bila kumjulisha mwenye shamba
🤣🤣🤣🤣Baada ya kusikia Viongozi wa Chadema wamekubali Tume huru viende pamoja na Katiba Mpya na Zitto akakubali.

Kasema jana nimesikia wanataka kuja ila msiwaruhusu mpaka mwenye shamba mnijulishe.

Hofu ya nini Mama?
 
Yanabana lakini yataachia.Katiba mpya ni lazima,huwezi kuzuia hitaji la wenye nchi yao🐒🐒🐒
 
Na wameambiwa wasifanye lolote bila kumjulisha mwenye shamba
Wana ccm wana tatizo kubwa sana nalo ni woga wa kuongozwa na chama tofauti na CCM.
Wanaamini kuwa endapo chama kingine kitashinda basi hilo ni zari la raisi aliye madarakani.
Kila rais wa ccm anatawaliwa na hili zimwi uchwara. Kitendo hicho husemwa kama ccm imefia viganjani mwake. Kwa hiyo kila mmoja atapambana by any means hata wakifa watu si neno ili mradi ccm isife mikononi mwake huku ni amirijeshi mkuu.
Katika hili hakua rais shujaha tangu kuanzia Kikwete.
Basi huu woga ndio dhambi kuu itakayopeleka ccm motoni.
Lazima aje rais shujaa atayeamini upatanisho na kujenga kuaminiana.
Lazima watanzania tuaminiane katika kujenga nchi. Hatuaminiani kabisa yaani wapinzani ccm wanawaona kama Mungiki au Intarahamwe na zaidi Alshabab aka magaidi. THIS IS WRONG .
Kwa kuanza kujenga kuaminiana tuanze na hili la katiba, utararatibu wa haki na mzuri wa kujitawala, tunaogopa nini maana tutaifuata wote.
Hili taifa halitakomboka KAMWE kama hatataminiana na kujua kuwa wote ni Watanzania. Ccm mna wajibu mkubwa na wa kwanza katika hili kama kweli mnaipenda nchi hii nzuri tuliyozawadiwa na Mungu.
 
Anajificha kwenye kikosi kazi ili majibu yakiwa ya hovyo kama yale ya jana ya kina Mukandara aseme yeye hausiki, amepokea tu mapendekezo toka kwa wajumbe wa tume, kumbe yeye ndie aliyewanyooshea njia tume waje na majibu gani.
 
Nitaamini km weak mara tu baada ya wewe kwenda kumtoa! Lkn km unapiga kelele hz kwa ujanja wa kuiga huku ukiwa zako hukoo nanjilinji, basi wewe ni the most miserable!
Nonsensical!
 
Back
Top Bottom