Huu Mwenge usiwe unakimbizwa Dar es Salaam, unatuchosha na kutupotezea muda

Hili jina la uhuru litolewe uitwe mwenge wa kero na siyo mwenge wa uhuru.Maana unawafanya watu wasiwe huru barabarani na ni matumizi mabaya ya pesa za umma.Siku sisi chauma mkituchagua kuongoza Nchi,Cha kwanza kabisa huu mwenge tutaupeleka pale uwanja wa uhuru kuuchoma moto mbele ya umma.
 
Sisi tumeuwasha mwenge, na kuuweka juu mlima, mlima Kilimanjaro.
Umulike ndani hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini.
Penye chuki ulete tumaini
penye dharau ulete tumaini
heshima palipojaa dharau.

Hivi kweli CCM haioni AIBU kwa wimbo huo hapo juu bado kuendelea na Mwenge wakati yote hayo wao ndio wanaongoza kuyatenda?
 
Na kweli huo mwenge ndio umekufanya hue na mawazo hayo
Sasa kama mwenge ndio umeleta uhuru kwanini mnamuita nyerere mpigania uhuru

Na kama mwenge unalinda nchi yetu
Majeshi yana kazi gani

Hila sishangai yyte anayeshiriki
Mbio za mwenge lazima awe na mawazo kama yako
 
Sijasema Mwenge umepigania uhuru. Nimesema ni kielelezo cha uhuru.

Uwe unasoma na kuelewa!
 
Demu (not a girlfriend) wangu kakesha kuupokea kwenye mwenge uko halmashauri katoka usiku sana, kesho yake jana kaenda Kigamboni eti "mama anazindua kiwanda". Alafu alinipiga kizinga kumbe ni hela ya kushona sare ya mwenge.
 
Duniani sasa watu wanatengeneza mashine zenye akili kuliko binadamu AI, sisi tunakimbizana na mwenge wa kishirikina. Aibu!
 
Mkuu unataka kuharibu tambiko!!!
 
Mwenge ndio zindiko la kufanya ccm iendelee kukaa madarakani. Hakuna namna wataacha huo ushirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…