Huu ndio Mtihani kwa ACT-Wazalendo: Kukubali maridhiano na kuunda Serikali

Huu ndio Mtihani kwa ACT-Wazalendo: Kukubali maridhiano na kuunda Serikali

Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Kwa akili yako wananchi ndio wamemuadhibu Seif au vyombo batili vya ulinzi na usalama?
Mayalla sio jambo lenye afya kwa mtu mzima, msomi, unayefahamika na huna njaa kujivua utu wako kwa ushabiki wa kijinga kwa vile tu umeingia chama cha wajinga.
 
Kwani katiba ya Zanziba inataja makubaliano ya SUK ktk upinzani ni Maalim Seif tu? Mfano kwa sasa CUF pia imepata viti Pemba, hakuna uwezekano kwa mgombea wa CUF au Chama kingine kuingia ktk SUK?
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P
 
Wananchi ndio wamefanya maamuzi ya kuwafanya mkia..unamlaumu Nani hapo..na mkizidi hata huo mkia watawaondolea..subiri

Jeshi la wavamizi ndio wananchi pamoja na jeshi la kukodiwa la Burundi ??
 
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P

Kwa uchaguzi upi huu wa jeshi la wavamizi na majeshi ya kukodi ya Burundi ??
 
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P
nani aliyekwambia watu wanafata katiba
 
nani aliyekwambia watu wanafata katiba
Kila kitu katika uendeshaji wa serikali kinaongozwa na katiba, sheria, taratibu na kanuni, sasa kama zinafuatwa au la, hilo sio letu ni la watendaji na watekelezaji.
P
 
Wananchi ndio wamefanya maamuzi ya kuwafanya mkia..unamlaumu Nani hapo..na mkizidi hata huo mkia watawaondolea..subiri
Hahaha wauondoe tu, mbona tunaishi poa tu?!

Ujinga wao sio wetu, mabavu kama yatawasaidia na waendelee who cares!.

Wafanye wenyewe hakuna kulazimishana hapa

Wameshinda sawa na waunde serikali waendelee na maisha nasi tunaendelea na maisha yetu.
 
Mi nazungumzia wananchi sio serikali..wananchi ndio wanaiweka serikali madarakanii.
 
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P

Waambie hao waliokutuma waendelee kuadhibu wazanzibari na hali hii kwani ndio maridhiano yanakuwa matamu zaidi upande wake mwana wa Mkuranga

Waambie hao waliokutuma waendelee kuadhibu wazanzibari na hali hii kwani ndio maridhiano yanakuwa matamu zaidi upande wake mwana wa Mkuranga

Mkuu Gavana , mimi ni an independent freelance journalist, situmwi na mtu wala sipangiwi na yeyote.
p
 
Atasubiri tena kuapishwa na UN
Kauli ileile itakuja ya 2015 subirni miezi 3
Kama Maalim Seif atakubali kuunda serikal ya Umoja wa kitaifa kwa matukio hovyo yaliyojitokeza basi Atakuwa nae ni Mchumia tumbo tu na kwa upande wang hakuna Mwanasiasa wa upinzani nitakayemuamin tena katika nchi ya TANZANIA kwan watakuwa wanatuyumbisha sisi wafuasi wao!.
 
Atasubiri tena kuapishwa na UN
Kauli ileile itakuja ya 2015 subirni miezi 3
Mbona alishasema zamani mar hii kila mtu aitafute haki yake kwa njia aijuayo mwenyewe na tumo wengine tunatafakari namna ya kurudisha haki zetu zilizoporwa
 
Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Hawakufanya kosa ila walifuata katiba ya nchi. CCM wakivunja katiba au kudharau sheria haimaanishi kila mtu afuate mwendo wao. Sisi tunaheshimu katiba na haki za wananchi.
 
Tafsiri kupitia tamko la Rais mteule wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, baada ya kutangazwa mshindi, inaweza kujenga taswira kuwa kiongozi huyo anaweza kuwa na dhamira ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo, mtihani upo kwa mpinzani wake, Maalim Seif Sharif Hamad na chama chake cha ACT-Wazalendo kutoa uamuzi ndani ya siku saba baada ya Rais kuapishwa.

Akizungumza baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Rais mteule wa Zanzibar, Dk Mwinyi alisema ataendeleza maridhiano yaliyopo kikatiba

Alisema atadumisha amani iliyopo kwa kushirikiana na wapinzani kwa sababu wao ni nyenzo muhimu katika kukuza demokrasia nchini.

“Nipo tayari kuyaendeleza maridhiano yaliyopo katika katiba yetu, kwani Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zetu, nitashirikiana nanyi kujenga Zanzibar mpya,” alisema Dkt. Mwinyi

Akiwa ameshinda kwa zaidi ya asilimia 76.2 alisema kuwa amepokea ushindi kwa mikono miwili na akaahidi kuijenga Zanzibar kwa ushirikiano na Wazanzibari wote bila kujali itikadi

Hata hivyo, kwa mwongozo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ACT-Wazalendo wanapaswa kuketi na Dk Mwinyi ndani ya siku saba kisha kumpa jina la mtu wanayempendekeza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, vilevile kufanya mashauriano kuhusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Kauli hiyo ya Dk Mwinyi, pamoja na ile nyingine kwamba “Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti za kisiasa”, inaweza kujenga picha ya utayari wake wa kushirikiana na wapinzani wake kuunda Serikali

Mtihani ni Seif ambaye awali alitangaza hatamtambua aliyetangazwa kama Rais wa Zanzibar, vilevile uchaguzi uliompa ushindi

Seif alisema uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 27 na 28, haukuwa uchaguzi, bali zoezi la kijeshi. “Uchaguzi ulitekwa na vyombo vya dola. Ikiwa kulikuwa hakuna uchaguzi vipi nitamkubali aliyetangazwa?, hakuwekwa madarakani na wananchi kama Katiba inavyotaka. Amewekwa madarakani isivyo halali,”alisema

Pamoja na msimamo wake huo, bado Seif jana alipozungumza na Mwananchi kwa simu kuhusiana na msimamo wake juu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alirejesha mpira kwa chama chake kwamba ndicho kitakachokuwa na uamuzi wa mwisho

“Kwanza itategemea huyo aliyetangazwa! Akiamua kuunda GNU na kutaka kutushirikisha sisi itategemea maamuzi ya Chama. Si maamuzi yangu,” alisema

Kauli hiyo ya Seif, imeshabihiana na ile ya Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Salim Bimani aliyesema: “Chama kitakaa na kutoa tamko la pamoja kuhusu vurugu zote hizi za uchaguzi. Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia ushiriki wetu kwenye hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa”

Kwa mujibu wa Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Rais, si hiari kwa Rais aliyeshinda, bali ni lazima pale mshindi wa pili anapopata kura za urais asilimia 10 au zaidi

Katika matokeo ya urais Zanzibar yaliyotangazwa Oktoba 29, mwaka huu na Jaji Hamid, Seif aliyegombea urais kupitia ACT-Wazalendo, amepata asilimia 19.87, ambayo ni karibu mara mbili ya asilimia zinazohitajika ili chama kilichoshika nafasi ya pili kitoe Makamu wa Kwanza wa Rais na kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Ibara hiyo inaeleza bila kutaja idadi, kuwa endapo mshindi wa kiti cha urais hakuwa na mpinzani, basi Makamu wa Kwanza wa Rais atapatikana kupitia chama kitakachoshika nafasi ya pili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Hadi sasa, kabla ya kupitisha majina ya viti maalumu, CCM ina viti 49 na ACT-Wazalendo kimoja
Kwa ufafanuzi huo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, mantiki yake ni kuwa ACT-Wazalendo ndiyo wenye kutakiwa kutoa majibu ya mtihani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ama wakubali au wakatae

Na kwa mujibu wa Katibu, wanapaswa kuwa na majibu ndani ya siku saba kutoka siku ambayo Dk Mwinyi ataapishwa.
Kingine kinachoweza kuwapa mtihani ACT-Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Mpaka sasa wana mjumbe mmoja ambaye ndiye pekee ana sifa ya kuteuliwa kabla ya kungoja viti maalum au hisani ya uteuzi katika viti 10 vya Rais wa Zanzibar.

Source: citizen
Kila mmoja wetu anajuwa lililotokea zanzibar ni UCHAFUZI. Hawa makada waliopo hapa ukumbini natumai ni watu weledi sana na wanafahamu uzuri na ubaya wa binadamu. Kweli kabisa mara hii CCM wamepigwa bao na wameingia kizunguzungu maana hakupata hata majimbo kumi katika hamsini. Maamuzi yote haya ya kuuwa na kuiba watajibu siku moja. Sisi tuliopoteza watu wetu kwa mututu wa bunduki hatuwezi kuisahau serikali ya CCM na munazidi kutuskuma pembeni. Iko haja ya kufanya maamuzi magumu kama waliodhulumiwa.
 
Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Hii adhabu ya Maalimu ilitolewa na vyombo vya dola? Maana wananchi walikua tayari hata kulinda kura zake na wengi wamepoteza maisha.
 
Mimi ni muumini wa kufuta katiba na sheria za nchi. 2015, walicho kifanya CCM Zanzibar kurudia kura ilikuwa ni kinyume cha katiba na sheria. Pia serikali iliofuata ilikuwa ni kinyume cha katiba. Kwa kuwa wengi hamusomi katiba ya nchi yenu ndio munaona kila kitu wakisema wakubwa ni kweli. Laiti kama viongozi wa taifa hili wana heshimu katiba basi ilikuwa haina haja kupeleka majeshi na kuuwa watu bure. Siku kumi baada ya kura bado wazanzibari tunaingiliwa usiku na vikosi kwanini?. Kweli nchi hii kuna usalama. Nyinyi makada munafurahia mambo haya?. Jamani tuweni wakweli na nafsi zetu. CCM ni majambazi maana kama ilikuwa ni viongozi bora wangeliheshimu katiba na sheria za nchi. Hapa zanzibar ukiwa sio mwanachama wa CCM huwezi kupata ajira au kufanikiwa na chochote katika ofisi za serikali.
 
Hasira Hasara!!! Kususa ni hasara kubwa mno. Ubinafsi (egoism) ni mbaya. Learn from a very simple issue within the ruling party, kama Rais Magufuli angazira kutumikia wa Tanzania kama Mbunge, Waziri Mdogo, Waziri ndani ya serikali wakati viongozi wengine ndani ya seeikali walikuwa mafisadi, waliuza mashirika ya umma kama Reli Simu, Bandari, madini, Gesi, ndege zote walizigida, Je angalipa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania na kwa muda mfupi kuweza kurudisha mikononi mwa serikali mashirika yote hayo pamoja na miradi yote inayoendelea nchini? Kama angatoka CCM asingelifika hapo alipo. Kwa hiyo Maalim Seif aingie kazini mara moja bila kusita.
umesahau aliyeuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa
 
Kweli mtu akikwambia huna akili, inapaswa ukitafakari.

Sasa dogo hii comment yako unamwambia babako au unamkusufia nani?
👉Utakuwa hujasoma mpaka mwisho andiko hili 😬!

Hizi pumba za wavamizi peleka Lumumba , ZANZIBAR inapigania uhuru wake tumechoka kuuliwa

ZANZIBAR freedom first.
 
Kweli mtu akikwambia huna akili, inapaswa ukitafakari.

Sasa dogo hii comment yako unamwambia babako au unamkusufia nani?
👉Utakuwa hujasoma mpaka mwisho andiko hili 😬!
Vyovyote unavyofikiri nindio uhuru tunaonyimwa na hawa majambazi yanayoifanya nchi ni mali yao.
Zanzibar haihitaji maridhiano inahitaji uhuru wake ilioupata dec. 1963 ukaporwa na Nyerere na genge lake kwa kutuvamia hapo Jan 1964.
 
Back
Top Bottom