Kwa akili yako wananchi ndio wamemuadhibu Seif au vyombo batili vya ulinzi na usalama?Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.Kwani katiba ya Zanziba inataja makubaliano ya SUK ktk upinzani ni Maalim Seif tu? Mfano kwa sasa CUF pia imepata viti Pemba, hakuna uwezekano kwa mgombea wa CUF au Chama kingine kuingia ktk SUK?
Wananchi ndio wamefanya maamuzi ya kuwafanya mkia..unamlaumu Nani hapo..na mkizidi hata huo mkia watawaondolea..subiri
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P
nani aliyekwambia watu wanafata katibaKatiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P
Kila kitu katika uendeshaji wa serikali kinaongozwa na katiba, sheria, taratibu na kanuni, sasa kama zinafuatwa au la, hilo sio letu ni la watendaji na watekelezaji.nani aliyekwambia watu wanafata katiba
Hahaha wauondoe tu, mbona tunaishi poa tu?!Wananchi ndio wamefanya maamuzi ya kuwafanya mkia..unamlaumu Nani hapo..na mkizidi hata huo mkia watawaondolea..subiri
Mi nazungumzia wananchi sio serikali..wananchi ndio wanaiweka serikali madarakanii.Hahaha wauondoe tu, mbona tunaishi poa tu?!
Ujinga wao sio wetu, mabavu kama yatawasaidia na waendelee who cares!.
Wafanye wenyewe hakuna kulazimishana hapa
Wameshinda sawa na waunde serikali waendelee na maisha nasi tunaendelea na maisha yetu.
Katiba ya Zanzibar haijaji mtu, inataja chama cha pili chenye more than 10% ya votes. Ni chama ndio kinapewa fursa ya kupendekeza jina, by now barua ya ombi la jina imeisha pelekwa ACT.
Katika mawaziri, wanaweza kuteua mawaziri toka vyama vyote.
P
Mkuu Gavana , mimi ni an independent freelance journalist, situmwi na mtu wala sipangiwi na yeyote.Waambie hao waliokutuma waendelee kuadhibu wazanzibari na hali hii kwani ndio maridhiano yanakuwa matamu zaidi upande wake mwana wa Mkuranga
Kama Maalim Seif atakubali kuunda serikal ya Umoja wa kitaifa kwa matukio hovyo yaliyojitokeza basi Atakuwa nae ni Mchumia tumbo tu na kwa upande wang hakuna Mwanasiasa wa upinzani nitakayemuamin tena katika nchi ya TANZANIA kwan watakuwa wanatuyumbisha sisi wafuasi wao!.
Mbona alishasema zamani mar hii kila mtu aitafute haki yake kwa njia aijuayo mwenyewe na tumo wengine tunatafakari namna ya kurudisha haki zetu zilizoporwaAtasubiri tena kuapishwa na UN
Kauli ileile itakuja ya 2015 subirni miezi 3
Hawakufanya kosa ila walifuata katiba ya nchi. CCM wakivunja katiba au kudharau sheria haimaanishi kila mtu afuate mwendo wao. Sisi tunaheshimu katiba na haki za wananchi.Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
Kila mmoja wetu anajuwa lililotokea zanzibar ni UCHAFUZI. Hawa makada waliopo hapa ukumbini natumai ni watu weledi sana na wanafahamu uzuri na ubaya wa binadamu. Kweli kabisa mara hii CCM wamepigwa bao na wameingia kizunguzungu maana hakupata hata majimbo kumi katika hamsini. Maamuzi yote haya ya kuuwa na kuiba watajibu siku moja. Sisi tuliopoteza watu wetu kwa mututu wa bunduki hatuwezi kuisahau serikali ya CCM na munazidi kutuskuma pembeni. Iko haja ya kufanya maamuzi magumu kama waliodhulumiwa.Tafsiri kupitia tamko la Rais mteule wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, baada ya kutangazwa mshindi, inaweza kujenga taswira kuwa kiongozi huyo anaweza kuwa na dhamira ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Hata hivyo, mtihani upo kwa mpinzani wake, Maalim Seif Sharif Hamad na chama chake cha ACT-Wazalendo kutoa uamuzi ndani ya siku saba baada ya Rais kuapishwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Rais mteule wa Zanzibar, Dk Mwinyi alisema ataendeleza maridhiano yaliyopo kikatiba
Alisema atadumisha amani iliyopo kwa kushirikiana na wapinzani kwa sababu wao ni nyenzo muhimu katika kukuza demokrasia nchini.
“Nipo tayari kuyaendeleza maridhiano yaliyopo katika katiba yetu, kwani Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zetu, nitashirikiana nanyi kujenga Zanzibar mpya,” alisema Dkt. Mwinyi
Akiwa ameshinda kwa zaidi ya asilimia 76.2 alisema kuwa amepokea ushindi kwa mikono miwili na akaahidi kuijenga Zanzibar kwa ushirikiano na Wazanzibari wote bila kujali itikadi
Hata hivyo, kwa mwongozo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ACT-Wazalendo wanapaswa kuketi na Dk Mwinyi ndani ya siku saba kisha kumpa jina la mtu wanayempendekeza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, vilevile kufanya mashauriano kuhusu muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Kauli hiyo ya Dk Mwinyi, pamoja na ile nyingine kwamba “Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti za kisiasa”, inaweza kujenga picha ya utayari wake wa kushirikiana na wapinzani wake kuunda Serikali
Mtihani ni Seif ambaye awali alitangaza hatamtambua aliyetangazwa kama Rais wa Zanzibar, vilevile uchaguzi uliompa ushindi
Seif alisema uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 27 na 28, haukuwa uchaguzi, bali zoezi la kijeshi. “Uchaguzi ulitekwa na vyombo vya dola. Ikiwa kulikuwa hakuna uchaguzi vipi nitamkubali aliyetangazwa?, hakuwekwa madarakani na wananchi kama Katiba inavyotaka. Amewekwa madarakani isivyo halali,”alisema
Pamoja na msimamo wake huo, bado Seif jana alipozungumza na Mwananchi kwa simu kuhusiana na msimamo wake juu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alirejesha mpira kwa chama chake kwamba ndicho kitakachokuwa na uamuzi wa mwisho
“Kwanza itategemea huyo aliyetangazwa! Akiamua kuunda GNU na kutaka kutushirikisha sisi itategemea maamuzi ya Chama. Si maamuzi yangu,” alisema
Kauli hiyo ya Seif, imeshabihiana na ile ya Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Salim Bimani aliyesema: “Chama kitakaa na kutoa tamko la pamoja kuhusu vurugu zote hizi za uchaguzi. Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia ushiriki wetu kwenye hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa”
Kwa mujibu wa Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Rais, si hiari kwa Rais aliyeshinda, bali ni lazima pale mshindi wa pili anapopata kura za urais asilimia 10 au zaidi
Katika matokeo ya urais Zanzibar yaliyotangazwa Oktoba 29, mwaka huu na Jaji Hamid, Seif aliyegombea urais kupitia ACT-Wazalendo, amepata asilimia 19.87, ambayo ni karibu mara mbili ya asilimia zinazohitajika ili chama kilichoshika nafasi ya pili kitoe Makamu wa Kwanza wa Rais na kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Ibara hiyo inaeleza bila kutaja idadi, kuwa endapo mshindi wa kiti cha urais hakuwa na mpinzani, basi Makamu wa Kwanza wa Rais atapatikana kupitia chama kitakachoshika nafasi ya pili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
Hadi sasa, kabla ya kupitisha majina ya viti maalumu, CCM ina viti 49 na ACT-Wazalendo kimoja
Kwa ufafanuzi huo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, mantiki yake ni kuwa ACT-Wazalendo ndiyo wenye kutakiwa kutoa majibu ya mtihani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ama wakubali au wakatae
Na kwa mujibu wa Katibu, wanapaswa kuwa na majibu ndani ya siku saba kutoka siku ambayo Dk Mwinyi ataapishwa.
Kingine kinachoweza kuwapa mtihani ACT-Wazalendo kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni idadi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
Mpaka sasa wana mjumbe mmoja ambaye ndiye pekee ana sifa ya kuteuliwa kabla ya kungoja viti maalum au hisani ya uteuzi katika viti 10 vya Rais wa Zanzibar.
Source: citizen
Hii adhabu ya Maalimu ilitolewa na vyombo vya dola? Maana wananchi walikua tayari hata kulinda kura zake na wengi wamepoteza maisha.Hoja nzuri sana hii.
Uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa CUF, walifanya ujinga kususia uchaguzi ule wa marudio, na matokeo ya uchaguzi huu ni kufidia makosa, sasa Maalim kupitia ACT, ameadhibiwa. Hata hivyo, kufanya kosa, si kosa, kosa ni kurudia kosa, Maalim Seif alifanya Kosa ile 2015, sasa 2020, asilirudie kosa!.
P
umesahau aliyeuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupaHasira Hasara!!! Kususa ni hasara kubwa mno. Ubinafsi (egoism) ni mbaya. Learn from a very simple issue within the ruling party, kama Rais Magufuli angazira kutumikia wa Tanzania kama Mbunge, Waziri Mdogo, Waziri ndani ya serikali wakati viongozi wengine ndani ya seeikali walikuwa mafisadi, waliuza mashirika ya umma kama Reli Simu, Bandari, madini, Gesi, ndege zote walizigida, Je angalipa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania na kwa muda mfupi kuweza kurudisha mikononi mwa serikali mashirika yote hayo pamoja na miradi yote inayoendelea nchini? Kama angatoka CCM asingelifika hapo alipo. Kwa hiyo Maalim Seif aingie kazini mara moja bila kusita.
Hizi pumba za wavamizi peleka Lumumba , ZANZIBAR inapigania uhuru wake tumechoka kuuliwa
ZANZIBAR freedom first.
Vyovyote unavyofikiri nindio uhuru tunaonyimwa na hawa majambazi yanayoifanya nchi ni mali yao.Kweli mtu akikwambia huna akili, inapaswa ukitafakari.
Sasa dogo hii comment yako unamwambia babako au unamkusufia nani?
👉Utakuwa hujasoma mpaka mwisho andiko hili 😬!