Huu ndio wakati rasmi wa kuongea ukweli kuhusu Fiesal

Huu ndio wakati rasmi wa kuongea ukweli kuhusu Fiesal

Feisal ana Bahati ya kufunga magori kwenye mechi mhimu , Ila sio mchezaji hatari wa kutegemewa
 
Screenshot_20221226-081601.jpg
 
Nianze kwa kutoa lawama zangu KWA uongozi wa Yanga kwa sababu nimesikia eti Feisal amejiunga na kambi ya Yanga.

Ni kwamba mashabiki wa Yanga hatumtaki Feisal.

Tumeshakubali kwamba ameondoka.

Hatumuhitaji please. Msije kushangaa akizomewa..

Na kwa wewe unaesema msimponde Fei kutaka kuondoka kwa sababu mpira ni kazi yake na kule kafuata maslahi blah blah blah jua wewe sio shabiki halisi wa mpira.

Wewe ni mchambuzi wa masuala.ya uchumi na sio shabiki wa mpira.

Shabiki wa mpira huwa haangalii hizo.

Shabiki wa mpira anataka kuona mchezaji alie lelewa na timu yake akiwa loyal kwa timu kama ambavyo yeye shabiki alivyo loyal KWA timu.

Huo ndio ushabiki wa mpira wa miguu na ndio ulio FANYA mpira kuwa mchezo unao pendwa na watu wengi Duniani.

Katika mpira wa miguu hakuna watu muhimu kama mashabiki wenye tabia na mentality za ushabiki.. HAWA ndio roho ya mpira wa miguu.

Shabiki wa mpira wa miguu ni yule anaesema Yanga mlibebwa ndio maana mliweza kutufunga Simba na sio anaesema Yanga mlituzidi mbinu uwanjani ndio maana mkashinda.

Huyu anaesema Yanga mlituzidi mbinu uwanjani ni mchambuzi wa mpira na sio shabiki.

Kama mashabiki wangekuaga wanatoa maoni yao kuhusu mechi kama wachambuzi leo hii nisingekuwa shabiki wa mpira ningetemana nao tangu nikiwa darasa la kwanza. Maana mpira ungekuwa mchezo unao boa sana na ungekosa mantiki ya ushabiki.

So waacheni mashabiki watumie haki yao ya ushabiki.

Waacheni mashabiki waseme Fei Toto ni mchezaji wa kawaida na kwamba kuondoka kwake hakuta Punguza chochote ndani ya Yanga.

Waacheni mashabiki waseme Fei Toto anaenda kuua kiwango chake. Hiyo ndio ladha ya ushabiki.

BACK TO MY POINT: HUU NDIO WAKATI WA KUMWAMBIA FEISAL UKWELI KUHUSU YEYE.

Naanza mimi kusema kama ifuatavyo:

1. Feisal is overrated. Hana kiwango hicho ambacho mashabiki wa Yanga walikuwa wanasema anacho. Fei Toto ana nyota tu ya kupendwa na mashabiki wa Yanga lakini ni mchezaji wa kawaida sana.

Mnakumbuka alivyo kuwaga anacheza namba sita? He was just a surplus. Ameanza walau kuonekana baada ya kuanza kuchezeshwa namba kumi lakini kiukweli ni mchezaji wa kawaida sana.

Fei mdogo wangu. Maneno ya Haji Manara kwamba eti wewe sio mchezaji wa ligi ya Tz ni kile ambacho wakongo wanaita " Tapash" . Ni kukupa tu sifa ambazo huna KWA ajili ya kuku encourage na kuwa kejeli watani. Ila kiukweli wewe huna kiwango hicho.

Narudia tena Feisal wewe sio mchezaji wa kutisha isipokuwa tu umekuwa na nyota ya kupendwa na mashabiki wa Yanga.

Wewe ni mchezaji mzuri KWA sababu mashabiki wa Yanga walikuwa wanasema wewe ni mchezaji mzuri lakini tofauti na hapo believe me, wewe ni mchezaji wa kawaida sana.

2. Mashabiki wa Yanga walioumizwa na kuondoka kwako ni kwa sababu ya mazoea tu na sio KWA sababu eti wewe ni mchezaji wa kutisha.

Ni mazoea KWA maana wamezoea kulisikia jina lako likitajwa sambamba na majina ya wachezaji wengine wa Yanga. Anachukua mpira Kibwana Shomari anampa Aucho, Aucho kwake Fistoo Mayele, Mayele anamuachia Feisal Salum Abdallah..Ni hivyo tu wala si kingine.

Mazoea yana tabu ila wanayanga ambao bado hamjamuondoa Feisal kwenye mioyo yenu msijali muda si mrefu mtamsahau..

Kundi jingine ni la wanayanga ambao Wana amini timu yao inaenda kupata mafanikio makubwa kitaifa na kimataifa na wewe Feisal umekua na kulelewa hapo Yanga so walitaka wewe uwe sehemu ya hayo mafanikio ya Yanga. Wamekuwa dis appointed baada ya wewe kuondoka ghafla bila jambo hilo kutimia.

Kundi jingine ni la mashabiki wanao ona aibu kuonekana Yanga haina hela za kukulipa. Wana ogopa kutaniwa na mashabiki wa Simba kwamba Yanga mmeshindwa kumzuia Feisal aondoke KWA sababu hamna hela. Hawahuzuniki KWA sababu eti wewe umeondoka la hasha wanahuzunika KWA sababu wanaona aibu ya kutaniwa na mashabiki wa Simba ila kiukweli wewe ni mchezaji wa kawaida sana na hilo litaenda kujidhihirisha utakapo anza kucheza Azam.

Blv me huzuni ya wanayanga kuhusu sakata la Feisal ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko uwezo ama kiwango cha Feisal.

NB: Kwenu mashabiki na wasemaji wa Yanga. Acheni utani wa kuwapa wachezaji wenu sifa ambazo hawana.

Mwisho wa siku hao wachezaji wanaamini kweli huo utani. Unawapanda kichwani halafu wanaanza kusumbua sumbua kama Feisal.

Eti sio mchezaji wa kucheza ligi ya Tanzania.

Eti thamani yake ni sh bilioni mbili. KWA mpira GANI alio nao?
Mkataba wa Feitoto ni wa kihuni sana Yanga hawana hoja yoyote ya maana shimo walichimba wenyewe acha wakae humo ndani
 
Umeongea point sana Feisal n mchezaji wa kawaida sana tena sana.. hana skills kabisa yeye kupiga mishuti isiyo na macho na kujiangusha ovyo ovyo... ball controll yake iko chini hawezi mfikia hata Ambundo.
kilichompa umaarufu ni ushabiki hasa pale alipolinganishwa na mwamba wa Lusaka. LAKINI kule azam hakuna tena wa kumuimba ndani ya msimu atakua kasauhulika kama babu wa loliondo.
young killer katika ubora wake aliwahi kuimba kua wasanii hawajui kuchana na wanataka wapewe sifa ambazo hawana... nazani kama alimuimba Fei
 
LIKUD ni kama umeeleweka vile??
Ila alikua ana shaiiiini hapo Yanga....Toto alikua ni Yanga na Yanga ilikua ni Toto...leo mtoto kakua achaa akaanze maisha yake mapya
 
Alichokosea Feisal ni kwamba

1. Kuvunja mkataba kienyeji

2. Feisal kasubiri siku zote hizo, akaamua kuvunja mkataba siku 2 before derby

3. Kuna njia ya kutafuta Haki yako Ila sio kihuni kama anavyofanya
 
Alichokosea Feisal ni kwamba

1. Kuvunja mkataba kienyeji

2. Feisal kasubiri siku zote hizo, akaamua kuvunja mkataba siku 2 before derby

3. Kuna njia ya kutafuta Haki yako Ila sio kihuni kama anavyofanya
Halafu at least angesubiri kwenye dirisha kubwa
 
Tunaona wenzetu uingireza wachezaji wa nchi yao wana wathamini na kuwapa promo za hali ya juu na miishahara yao inapandishwa ,rahim steling katoka city kuja chelsea mkataba wake ulibaki mwaka mmoja lakin chelsea walitoa hela nyingi kumnasa

Kuna hawa vijana jude beligham na rice wa westham hawa watoto wapuuzi mpira wao wa kawaida sana ila media zao zinawapa promo ya kutosha ili thamani yao ipande

Hivi kwa akili ya kawaida jude anafika 100 mil us katika transfer market???? Diclane rice anafika hiyo hela ??? Ni kwakuwa ni vijana wa kwao hapo mjini

Ila bongo sasa ukishakuwa mzawa ndio wanakulalia hatar ,usishangae ukapewa mkataba wa milion 10 kwa mwaka na mshahara wa milion wakati wageni wanapewa milion 200 na mshahara wa milion 15

Tubadilike wabongo

Tunanyonyana kama tupo enzi za utumwa kumbe tayar tushapata uhuru tangia 1961
 
Tunaona wenzetu uingireza wachezaji wa nchi yao wana wathamini na kuwapa promo za hali ya juu na miishahara yao inapandishwa ,rahim steling katoka city kuja chelsea mkataba wake ulibaki mwaka mmoja lakin chelsea walitoa hela nyingi kumnasa

Kuna hawa vijana jude beligham na rice wa westham hawa watoto wapuuzi mpira wao wa kawaida sana ila media zao zinawapa promo ya kutosha ili thamani yao ipande

Hivi kwa akili ya kawaida jude anafika 100 mil us katika transfer market???? Diclane rice anafika hiyo hela ??? Ni kwakuwa ni vijana wa kwao hapo mjini

Ila bongo sasa ukishakuwa mzawa ndio wanakulalia hatar ,usishangae ukapewa mkataba wa milion 10 kwa mwaka na mshahara wa milion wakati wageni wanapewa milion 200 na mshahara wa milion 15

Tubadilike wabongo

Tunanyonyana kama tupo enzi za utumwa kumbe tayar tushapata uhuru tangia 1961
Kipindi unalinganisha na uingereza angalia pia na uchumi wa vilabu vya bongo.

Bado uwekezaji kwenye vilabu vyetu ni mdogo na pia tunategemea zaidi watu binafsi Leo GSM akikaa pembeni hiyo mil 4 mnayoisema mdogo itatafutwa kwa tochi.

Wachezaji wetu hawanyonywi bali hawajui kwamba mpira ni biashara, hawajui kujiuza, hawajui ku bargain wanapewa mikataba wanasaini tu kiholela.

Kingine wachezaji wa kibongo waongeze viwango hakuna mtu atakulipa mil 10 alafu kiwango hakieleweki.
 
acha aende zake Domayo Frank na Bahanuzi hata Ngasa pia walienda huko huko kilichowakuta wao ndo wanajua bora Ngasa , Domayo sijui alipoteleaga wapi kijana wa watu
 
Kuhama kwa mchezaji haimaanishi ndio iwe sababu ya kumuona et ni wakawaida....!!! Upo serious na mpira?. Wachezaji wangapi wapo yanga na tumashangilia mbona hawafanyi Kama anayofanya Fei??, Tuache chuki na roho mbaya kwa wachezaji wetu.
Fei sio mchezaji wa kawaida hata kidogo ni panic na hasira zako juu ya fei tu kwa alichokifanya, fei ana haki zake Kama mchezaji ni wakati wake kupata pesa kupitia kipaji chake.... Kama timu yetu imeshindwa kutimiza anachokitaka tumuache aende basi....!!!.
Kumchukia mtu kisa anadai haki ya anachokifanya nao ni ulevi wakijinga sana......!!, Ninachoshukuru na kuona ni mhimu kwa yanga yetu ni Nabii kutengeneza timu isiyotegemea sana mchezaji mmoja mmoja ili kupata MATOKEO..... Fei ni mchezaji wa daraja zuri Sana tuache chuki za uyanga hapa Kama hatutaki kumpa anachokitaka tumuache... Mambo ya eti kumuencourage mbona ambundo au makamba hawafanyi akiyoyafanya fei...!!
Yan nakazia kabisa hapa
 
Wewe uko loyal kwa timu yako? Mashabiki wa bongo ni malaya wa soka ndio maana T. P. MAZEMBE au timu yote ya ugenini ikija kucheza na Simba, Yanga mnaenda kuipokea, na kesho yake mnanunua jezi zao mnavaa uwanjani, na mnaishabikia. Mnaishabikia hiyo ni timu yenu?

Hapo mnakuwaje loyal? Hapo ni sawa na kuzini nje ya ndoa.

Huu upumbavu hauko kwa Yanga tu, na Simba mnao sana tu.

Mwacheni Faisal akale maisha, nyie mlimuona ni wa 4ml, wenzenu wamemuona ni wa 10ml. Au mkataba wake unasema atakaa Yanga hadi KIFO KIWATENGANISHE?
Shabiki wa mpira anataka kuona mchezaji alie lelewa na timu yake akiwa loyal kwa timu kama ambavyo yeye shabiki alivyo loyal KWA timu.
 
Back
Top Bottom