Huu ndiyo wakati wa majibu uliyokuwa unajiuliza ukiwa mtoto

Umenifikirisha sana, enzi hizo Nyerere bado Rais mshuwa alitoka ughaibuni na gari yake Datsun na Radio player.

Ile gari baadaye tuliambiwa iko gereji mpaka Sasa hivi na Mimi nimeuza gari yangu ili kuclear bill za shule za Watoto wangu ndio naelewa The Great Man alipitia magumu gani.

Nina ugomvi mkubwa sana wa matumizi ya hovyo ya umeme na maji, na hasa umeme.

Kwenye kuwasha taa Giza likiingia ni mahodari ila asubuhi taa za nje nisipozima Mimi zitashinda hivyohivyo, ni vigumu Kwa hawa kunielewa Kwa Sasa ni Kwa nini nakuwa mkali kwenye matumizi ya hovyo ya nishati, mfano wote mpo sebuleni usiku halafu taa za vyumbani ziko on unamulika nini?
 


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Watoto hawajui ni wachache Sana wenye akili ya kuelewa mapema Baba unazungumzia Jambo gani.

Wengi watasema Baba mKoloni, au mnokoπŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Watoto hawajui ni wachache Sana wenye akili ya kuelewa mapema Baba unazungumzia Jambo gani.

Wengi watasema Baba mKoloni, au mnokoπŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna katoto ka dada yangu kapo chuo ila akil zake ni 2. Akiwasha taa ile usiku usipozima asubuhi ndio bas, chakula mfano mpo wawil atapika cha watu 6 na hajali wala nini. Akienda kufua hayo maji anavyomwaga nikamuambia uzur sio muda utaingia kitaani na wewe utaelewa vizuri shoo inakwendaje.
 
Nilipokuwa mdogo wajomba zangu walikuwa hawanisaidii kwa lolote.basi nikawa na hizo chuki rohoni .ila sasa na mm nishakuwa kuna vitoto vya wajomba na binadamu vikataka hata msaada wakati mwingine nataka kuwasaidia ila sina chakuwapa dah.nikajisehemea kumbe nilikuwa na chuki za bure huenda na wale pia hawakuwa na chochote cha kunipa.
 
Mimi nyumbani Sasa hivi naonekana kama mwehu Fulani hivi ila nitawafunza Kwa njia ambayo watajifunza Kwa vitendo.

Huwezi kuamini thermos ya chai IPO lakini inachemshwa chai inaachwa kwenye sufulia bila kuweka kwenye chupa, kila anayetaka kunywa atapasha moto kwakuwa gesi IPO na asubuhi maji ya kuoga jiko la gesi.

Sasa hili somo lieleweke vyema hii gesi ikikata wapambane na mkaa, je chai ikichemshwa haitowekwa kwenye chupa?
 

Wale ndugu uliosema hawakusaidii umegeuka kuwa wao Kwa watoto wa Dada zakoπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…