Huu ndo Ushahidi wa Nchi za Magharibi zinavyotusaidia. Anayewatukana na kuwasimanga muonee huruma sana!

Wewe jamaa si ulikua unamuunga mkono chura kiziwi kuuza bandari. Basi endelea kumuunga mkono msimamo wa kuwavimbia hao wazungu. Ukipenda Boga ndo hiyo sasa. Sio unabadilisha gia angani kisa umeguswa tako kwa huo msimamo
Hadi leo nasimama nae kwenye suala la Bandari
 
Uelewa wako ni mdogo sana na ishu ya kuongea Rais mnaikuza , mbona Mgufuli alikuwa anaongea kila siku ?


Kabla ya kuja hao hapakuwa na magonjwa ya hovyo ...Hamna msaada wa bure kama wewe ni mzungu ni bora kuomba uraia huko kabisa hapa utateseka sana kwa vile hatuwezi kuwa wazungu .
 
Ukipitisha mkataba mbovu halafu utake kuuvunja kiholela, kwa dunia ya leo, utapigwa tu.
 
Hadi leo nasimama nae kwenye suala la Bandari
Mfuatilie Traore ndio utajua...Waafrika wanaweza kufunga mipaka yao wakaishi ndani wasitegemee kitu chochote hata media za nje tusiangalie na wakaishi ...Ni kwa vile nchi haijapata dikteta unaweza kuhama .

Magufuli kipind safari za nje zilianza kukoma mpaka mkaanza kusema wawekezaji ....nachoongea kinamlinda kutokana na Tanzania foreign affairs policy ;hakuna kibaya ila kakumbusho moja ya sheria yake hakuna kuingilia mambo ya ndani ya Tz , kama unatoa msaada toa then jikatae huwezi kuingilia mambo ya ndani .

Kama ukiingilia mambo ya ndani, ishu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni dk sifuri .

Nchi zao kutwa watu wanapigana bastola umesikia ubalozi wa Tz ukipiga kelele , unajua kazi za ubalozi ? kwani katekwa mzungu ?
 
Mungu Wabariki Wazungu
 
Hadi leo nasimama nae kwenye suala la Bandari
Hapa kwa bandari natofautiana na wewe......ila twende mbele na hao wanaowasema vibaya nchi za magharibi. Hakika hawajitambui......na kwa hili bandiko umewaacha midomo wazi 😀
 
North Korea waliwekewa vikwazo na kunyimwa misaada, bado wametengeneza mpaka nuclear. Wanamtisha mpaka Mmarekani. Sisi tunalilia kusaidiwa. Labda ubongo wa mtu mweusi uliumbwa kwa mabaki ya material.
 
Kama Kuna mtu kawatunaka wazungu itakuwa ni kichaa.
 
Hela za kupambana na ukimwi tu huna alafu unajifanya kiburi. Mwehu wewe!
Ukitukana ndo unakuwa mwanademokrasia mzuri? na siku ukipewa utawale Nchi hali itakuwaje? Si maiti zitaokotwa majalalani kama chupa za maji. Pole sana hujui na hujijui!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…