Wewe ni kilaza kama walivyo vilaza wengine na ndio mmejaza Africa, Unategemea nini hapo ? Unajisifia umasikini kwenye nchi ya Ardhi tajiri , nyie wajinga ndio mnaturudisha Nyuma sana .
Alichokisema muanzisha uzi ni rahisi kueleweka. Sijui kwa nini hujaelewa.
Umesema ni kilaza na a ajisifia umaskini.
Kiufupi, ni kama vile ulitaka aseme kama Magufuli alivyokuwa akiwaambia Watanzania watembee vifua mbele kwa vile wao siyo maskini,na nchi yao ni tajiri....,siyo?
Ukitaka mtu awe na fikra za kujitoa katika hali aliyomo,unatakiwa kumuambia ukweli wake. Waambie watanzania ukweli mchungu kwamba wao ni maskini na nchi yao ni maskini sana ili wajiulize ni kwa nini wako katika hali hiyo ,na wafanye nini ili kujitoa katika dimbwi la umaskini.
Katika nyanja ya diplomasia,mwenye nguvu ya kiuchumi ndiye mwenye ushawishi(influence)...hakuna two way traffic hapo.
Tanzania ni nchi maskini ambayo bajeti yake hadi sasa inachangiwa na wahisani,..sasa inapataje ujeuri wa kuwapiga mkwara na kutukana wahisani wake...tena kwa kuzungumzia jambo jema la kufanyika kwa uchunguzi ambalo hata rais mwenyewe alilisemea?
Ni kweli tunatakiwa kuwa na jeuri hiyo ya kupiga mkwara nchi nyingine kwa sababu zenye mashiko na hadi pale tutakapojitoa katika umaskini tulionao.
Kwa taarifa yako tu,kitendo cha rais kusema kwamba atawachongea mabalozi wa nchi za magharibi kwa marais wao kwa vile uamuzi wao ni wa binafsi, kimetuaibisha kama taifa...maana ,kidiplomasia inaeleweka sauti ya balozi ni sauti ya nchi anayowakilisha. Sasa kama rais wetu hajui hata jambo dogo kama hilo,sasa hayo masuala mazito ya kuitoa nchi katika umasikini ataelewaje?
Rais alitakiwa kujua endapo balozi ataongea maneno yake binafsi kinyume na takwa la nchi anayoiwakilisha,nchi husika inamrudisha nyumbani(recalled).
Kuza uchumi wako kwanza ndipo uwe na jeuri ya kupiga mkwara wengine....,vinginevyo kaa kimya.