Huu ndo Ushahidi wa Nchi za Magharibi zinavyotusaidia. Anayewatukana na kuwasimanga muonee huruma sana!

Huu ndo Ushahidi wa Nchi za Magharibi zinavyotusaidia. Anayewatukana na kuwasimanga muonee huruma sana!

Mbona mambo kibao yanaenda kwa ushirikiano wa China na mambo yanasonga??
Kwanini wamagharibi wasifanye kama China we do business with mutual benefit??
Shida yako akili kisoda.
Una akili mgando.
China anawasaidia nini kwenye maisha yenu ya kila siku hapa?

Kuwaletea bidhaa feki na kukisupport chama cha Mapinduzi?
 
Kwa kifupi Nchi za Magharibi zinatusaidia kuanzia miradi ya Afya ikiwemo kupambana na magonjwa kama Ukimwi, Kifua kikuu, utapia mlo na mingine mingi. Zinatusaidia Kuokoa uhai wa Mama wajawazito na watoto kwa kutoa fedha nyingi sana tunazotumia kuboresha hospitali zetu!

Nchi hizi zinatusaidia hadi kutujengea vituo vya kupokea kupoza na kusambaza umeme. Miradi mingi inayoendelea ni fedha wanazotoa wao kama misaada!

Zinatusaidia hadi kwenye miradi ya uzalishaji chakula ili tuwe na chakula cha kutosha.

Zinatusaidia kwenye masuala ya ya nishati mbadala bila kusahau miradi ya ujenzi wa shule, hospitali na maeneo mengi.

Sijawahi ona mchina akitusaidia miradi ya afya zetu na uhai wetu.

Sijawahi ona Urusi akitusaidia miradi ya afya zetu na uhai wetu.

Kusema ukweli namuonea sana huruma aliyewapiga biti hawa watu. Wakati ndo wanawasaidia wajisifu kwa wananchi kuwa wanatoa huduma bora.

Tuwaombe tu hawa wakubwa wamuonee huruma wasimchukulie hatua kali huyu aliyewatishia. Maana wakimchukulia hatua tu twafaaaaa🙌View attachment 3100424View attachment 3100425View attachment 3100426View attachment 3100427View attachment 3100434View attachment 3100434View attachment 3100428View attachment 3100435
Swali fikirishi je tukijiwekea malengo na kuacha kulea ufisadi hatuwezi kuzipata hizo pesa?
 
kama MUNGU akiamua, huenda nikawa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT)2045.nawaomba kabisa wana_JF kwa upendo kabisa kama mtakua HAI basi mnichague.mko tayari?na hii ni 21st century, na imebaki 21 year$?
 
kama MUNGU akiamua, huenda nikawa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT)2045.nawaomba kabisa wana_JF kwa upendo kabisa kama mtakua HAI basi mnichague.
Kwa tume ipi, inayo teuliwa na Rais, sina kumbukumbu za kutosha kuhusu fungu la uwendeshaji wake kama wako huru nalo
 
Serikali ya Canada ina haki ya kusitisha misaada yake kwa yeyote, kwa sababu yoyote, au hata bila sababu.

Kwa sababu yenyewe ndiyo inatoa misaada hiyo.

Unataka kuilazimisha jinsi ya kutoa misaada yake?

Tengeneza uchumi wako usihitaji msaada. Laumu viongozi wako kwa kufanya nchi yako yenye utajiri mwingi kutegemea misaada.

Kwa nini unailaumu serikali ya Canada kwa kujipangia yenyewe itoe misaada kwa nani na kwa sababu gani? Hiyo ni haki ya serikali ya Canada.
Ndio inaweza ila kuna sheria yoyote Canada ama Nchi yoyote ya Kidemokrasia kuitisha nchi ama mtu yoyote adrop kesi sababu ya Misaada?
 
Kwa hio suluhisho ni kuwafurumusha wote na tufunge balozi zote kisa tu wamesema ule uuaji na utekaji ufanyiwe uchunguzi wenye majibu yanayoeleweka kisha somebody nanii anawaambia wasimwambie wala wasimuelekeze cha kufanya yeye mboni kwao kukiungua huko hata rais wao akiapishwa huko hasogezi pua yake na hajawahi kukanyaga kwao hata wanaowawakilisha wasimzingue wao wanapokua na mambo yao huko yanaendelea hawaingilii anawaacha wafanye wanavyoona wao kwanini yeye wanamuingilia yaan wasimuingilie muingilie nyumbani kwake wamuache na nyumba yake
Nani ameongelea nini kuhusu kumfukuza mtu?
 
China anawasaidia nini kwenye maisha yenu ya kila siku hapa?

Kuwaletea bidhaa feki na kukisupport chama cha Mapinduzi?
Reli ya Tazara amekujengea China.
Smart fone amekuletea China.
Madaraja amekujengea China.
Miundombinu barabara amekujengea China.
Soko lako la parachichi kubwa moja wapo ni China.

Wakati huo USA hakukufanyia lolote wewe.
Anakutega kwa misaada ya vyandarua.
Hata huijui dunia ikoje China ndio amekuletea globalisation.

China ni business man masuala ya wewe na chama chako shughulika nacho mwenyewe.
 
Ndio inaweza ila kuna sheria yoyote Canada ama Nchi yoyote ya Kidemokrasia kuitisha nchi ama mtu yoyote adrop kesi sababu ya Misaada?
Hiyo haihitaji kuwa sheria, na wala si kitisho.

Kwa sababu Tanzania haina haki ya kupewa msaada na Canada.

Canada inaweza kuamua kuacha kuisaidia Tanzania kwa sababu yoyote, au bila sababu.

Laumu viongozi wako kwa kufanya Tanzania itegemee misaada ya Canada.

Usiilaumu Canada kwa kupanga inatoa vipi misaada yake.
 
Reli ya Tazara amekujengea China.
Smart fone amekuletea China.
Madaraja amekujengea China.
Miundombinu barabara amekujengea China.
Soko lako la parachichi kubwa moja wapo ni China.

Wakati huo USA hakukufanyia lolote wewe.
Anakutega kwa misaada ya vyandarua.
Hata huijui dunia ikoje China ndio amekuletea globalisation.

China ni business man masuala ya wewe na chama chako shughulika nacho mwenyewe.
Reli ya TAZARA alijenga ndiyo kama mkopo!

Hiyo mihndombinu hatujengea bure tena anatukopesha. Tena mbaya zaidi anatupiga maana anatujengea miondominu yenye viwango duni vya ubora tena kwa mikopo umiza yenye interest mbaya sana!

Hakuna msaada wa ujenzi anaoufanya mchina. Mchina yupo kibiashara tena kaa ajili ya kutuibia
 
Hiyo haihitaji kuwa sheria, na wala si kitisho.

Kwa sababu Tanzania haina haki ya kupewa msaada na Canada.

Canada inaweza kuamua kuacha kuisaidia Tanzania kwa sababu yoyote, au bila sababu.

Laumu viongozi wako kwa kufanya Tanzania itegemee misaada ya Canada.

Usiilaumu Canada kwa kupanga inatoa vipi misaada yake.
Kukwepa kodi ni kosa la jinai, kuzuia mtu asipelekwe Mahakamani pia ni jinai ama hili ni jinai akifanya tu China na tutamwita Dikteta ila wakifanya mabwana zetu tunajitoa ufahamu na kukata mauno?

Reverse hii situation Mtanzania yupo Canada kakwepa kodi, then China Aingilie kati kama Canada wanamfunga huyo Mtanzania basi China ana stop viwanda vya Canada China, Dunia nzima ingeimba.
 
Ila huyu Mama kidiplomasia anaturudisha kwa jiwe.Alafu naona kakwepa mkutano wa UNGA kamtuma Majaliwa!🤣🤣🤣
 
Kukwepa kodi ni kosa la jinai, kuzuia mtu asipelekwe Mahakamani pia ni jinai ama hili ni jinai akifanya tu China na tutamwita Dikteta ila wakifanya mabwana zetu tunajitoa ufahamu na kukata mauno?

Reverse hii situation Mtanzania yupo Canada kakwepa kodi, then China Aingilie kati kama Canada wanamfunga huyo Mtanzania basi China ana stop viwanda vya Canada China, Dunia nzima ingeimba.
Hiyo kodi yenyewe unayoisema ilikiwa ni kichekesho cha dunia nzima.

Ilikuwa sawa na habari ya "Amini Usiamini" katika gazeti la Mfanyakazi la miaka ya 1980.

Zaidi, narudia, serikali ya Canada ina haki ya kutoa na kusitisha misaada inavyotaka.

Laumu viongozi wako kwa kufanya taifa lako litegemee misaada ya Canda.

Usiilaumu serikali ya Canda kwa kuamua isaidie wapi na wapi isitishe misaada.
 
Mzungu hakusaidii chochote mzee.
Tena huyu mzungu ndio kakuzuia wewe kuendelea.
Wewe bora umshukuru Mchina ambaye kakubali kufanya biashara na wewe ndio maana una miundombinu na maendeleo mengine.
Nenda kafuatilie sakata la SAP-Structured adjustment Program.
Nchi nyingi Afrika hususan sub Saharan Afrika ndio zilimalizwa kwa mtego huu wa SAP.
Halafu walivyo washenzi wakawa wanawaletea msaada wa vyandarua na madawa mkiwa hafifu kwa miundombinu na kila kitu.
Aliyewasaidia angalau Mchina kwa kukubali kuwafungulia hata hivyo viwanda vya kushona Chandarua.

Mzungu huwa anataka sisi tuonekane tegemezi kwake siku zote.
Mtu kama huyo hakusaidii bali anakutawala kikoloni mambo leo.
Sawa mkuu, tuna mitizamo tofauti kuhusu hili, labda sijui maana sahihi ya kusaidiwa. Mbona tunawasumbua na kuwapigia magoti kila kukicha hata kwa mambo ambayo kama tungekuwa serious tungayafanya wenyewe?. Kwa nini wanapata ujasiri wa kutukemea kwa mambo yetu ya ndani ya nchi na hawawezi kuthubutu kufanya hivyo kwa nchi zinazojitegemea.
Tatizo ni sisi au ni wao? kwamba bado tunahitaji kusaidiwa hata ujenzi wa vyoo mashuleni? bado tunahitaji kusaidiwa hata kupambana na Malaria na magonjwa mengine ya umaskini? Kwa nini hata huyo mchina aje tena kutusaidia reli ta TAZARA miaka takribani 50 baada ya kusaidia ujenzi wake. Kiongozi akisimama na kuwapiga mkwara hao watu anakuwa anaongea kwa dhati toka moyoni au anajifaragua tu. Ni lini wamewahi kuja kutuomba watusaidie hayo wanayotusaidia?
 
Alifanya kipi cha maana? Yote uliyoandika/ kuuliza ni mashudu tu
Wewe sema hujui sio kwamba ni mashudu.
Uliuliza kuna ushahidi gani kama wanaotuletea misaada wananufaika zaidi.Nikakuuliza hayo maswali kukupa jibu.
Mwishowe unakana tena!??

Hizi hatua za muda mfupi ndani ya miaka mitano nani alizifanya tukazipiga??
 
Back
Top Bottom