The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Hii ndiyo elimu ya kukaririshwa shuleni ktk shule zetu...Mkuu mtu akija kwako anachuma mchicha wa 500 anauza halafu baadae anakuletea 200 jioni hakusaidii, hao wanahitaji Africa zaidi kuliko Africa inavyowahitaji wao. Mentality zenu hizo ndio za Kutojitegemea ndio zinafanya kila siku bara lipo gizani.
Kama ndiyo hivyo, si kauchume mwenyewe huo mchicha ili ukauze 500 na ubaki nazo zote...???
Na kama huwezi kuuchuma mwenyewe, unategemea uchumiwe na mtu mwingine kwanini unamdharau huyo mtu anayekusaidia kwa wakati huo...?
Kama ndiyo tabia yako ya kutukana na kudharau waliokusaidia ulipokuwa hujiwezi, basi subiri mpaka akili yako itakapokuwezesha kujiweza kujichumia huo mchicha mwenyewe kisha warudie na watukane....
Otherwise unapotukana wakunga huku uzazi ungalipo, wewe huna akili na huna maarifa wala ufahamu. Na huyu ndiye Rais wenu Samia Suluhu Hassan....!!
Msaidieni kumwambia ukweli. Acheni ujinga wa kujidanganya hivi....!!
