POTOSHI Huu ni mkutano wa kwanza baada ya Lissu kuachiwa huru

POTOSHI Huu ni mkutano wa kwanza baada ya Lissu kuachiwa huru

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha


1759131835697.png

​
 
Tunachokijua
Tundu Lissu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo anayekabiliwa na kesi ya uhaini, Septemba 22, 2025 Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ilitupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Tundu Lissu kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka pamoja na maelezo ya mashahidi ambayo yanadaiwa kuandikwa kinyume cha sheria.

Lissu alidai hati hiyo pamoja na viambatanisho vyake, ikiwemo maelezo ya mashahidi, vimeandikwa kinyume cha sheria na havikidhi matakwa ya kisheria. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 06, 2025

Madai

Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Tundu Lissu akihutubia wananchi na kuelezwa kuwani mkutano wa kwanza baada ya Lissu kuachiwa huru.

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umejiridhisha kuwa video hiyo si ya mwaka 2025 bali ni ya Oktoba 2020 Tundu Lissu alipokuwa akifanya kampeni za urais mkoani Tanga.

Video hiyo ilichapishwa Oktoba 21, 2020 hapa, hapa na hapa.

Aidha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X Lissu aliichapisha video hiyo ikiambatana na maelezo yanayosema "#Tanga pia wapo tayari kuondoa serikali hii ya kidhalimu. Asanteni sana Tanga. Twende tukapige kura ya Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu!"​
Back
Top Bottom