Huu ni muda mzuri usiku huu kufanya maombi

Huu ni muda mzuri usiku huu kufanya maombi

Wakuu mnaopitia humu usiku huu ni muda mzuri sana kufanya maombi.

Maombi unaweza ukayafanya kwa kufukiria bila kutamka. Mungu anasikiq tunavyofikiria
ni usiku mnene tulivu, nimezima tv na kufungulia redio kwa sauti ndogo. Nasikiliza nyimbo za taratibu za vitabuni kutoka kwenye redio moja ya kikristo. Muongoza maombi bado hajaanza kuomba. Kwa kweli ni muda mzuri usiku huu kumetulia kiasi cha kuoweza kuomba Mungu, hakuna bughudha
 
Eeh, Mwenyezi Mungu. Nakushukuru kwa kunilinda mchana kutwa, umenikinga dhidi ya majanga mbalimbali ambayo yalikuwa yakinikabili, eidha mengine kwa kuyaona au pasipo kuyaona na kutambua.
Nakuomba unisamehe pale nilipo kukosea, eidha katika kunena, kutenda nahata kuwaza. Nisamehe Mungu wangu na unioshe kwa damu ya mwanao Yesu Kriso aliyo imwaga pale msalabani ili nipate kukombolewa. Nakuomba ee Mungu wangu unilinde dhidi ya hila zote za mwovu. Malaika wako walinde nyumba yangu kwa moto ulao, funika nyumba yangu dhidi ya uovu waaina yoyote ile. Pia Mungu wangu nakuomba kesho niamke nikiwa salama mimi pamoja na wote walio katika nyumba hii, tuwe na ari ya kukupenda, kukutukuza na kulihimidi na kulitangaza jina lako ili watu wengine waokolewe. Tujalie afya njema, wape nguvu wagonjwa pia bariki wanao wauguza ili wawauguze kwa upole na kwa unyenyekevu, wakumbuke wafungwa, wajane, wasafiri na wenye mahitaji mbalimbali. Navunja na kuharibu nguvu za giza, nikatika JINA LA YESU zikashindwe na kuharibika. Pia watumishi wako nawaweka mikononi mwako ili wakatumiwe na wewe kama chombo chakufikisha neno lako ili mavuno yatakayo patikana yakawe kwaajili ya sifa na utukufu wako.
Naomba nakuamini ni katika Jina lipitalo majina yote la Yesu Kristo. Amin.
 
Moyo akili nafsi naikabidhi kwako Yesu nashindwa kutamka maneno yanayofaa
 
Swali la msingi hapa ni kwamba inakuwaje saa tisa usiku huu Mama Edina hujalala?
kuna wakati usiku usingizi hukata na huna kazi ya kufanya muda huo. Wengine huwa tuna tv, redio, simu, magazeti na vitabu tunasoma huku tumejilaza vitandani kusubiri usingizi wa alfajiri kabla ya kwenda kazini asubuhi
 
Back
Top Bottom