Huu ni mwaka wa kusafiri sana kuifaidi dunia

Bonheur Travels Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
252
Reaction score
499
Mwaka 2022 unagawanyika kwa mbili. Ni mwaka mzuri. Usikubali ukaishi maisha ya dhiki na kutofurahia maisha. Unafanya kazi ili iweje kama huwezi kutenga siku kadhaa za kufurahia maisha?

Dhamiria kuufanya mwaka huu kuwa mwaka wa kujipa nafasi binafsi. Au kama uwezo unaruhusu, basi jipe nafasi na wale uwapendao muizunguke dunia japo kwa nchi chache.

Kwa mfano, kama upo Tanzania. Unashindwaje kwenda Misri hapo kushangaa shangaa uzuri wa Cairo? Dubai kuona kufuru za Waarabu? Kusini mwa Afrika kuwehuka na maporomoko ya Viktoria? Au hata kule Instabul-Uturuki kwa 'akina Sultana kufurahia miji ya kihistoria? Basi hata Kenya tu hapo ukazunguke Masai Mara kubadilisha mazingira?

Januari achana nayo, unaweza kuanza kuweka mipango ya kuanza kuzunguka Februari sababu ni msimu wa sikukuu hivyo bei ziko chini sana kuanzia tiketi za ndege hadi maeneo ya kula maisha.

Uhai ni zawadi. Ufurahie!

-----

Asanteni WanaJF kwa utayari. Pia maoni na mapendekezo kuwa tuweke packages tulizonazo msimu huu, japo lengo letu lilikuwa kuambizana tu na haikuwa na ulazima msafiri kupitia huduma zetu. Ni heshima kubwa mmetupatia.

Kwa bahati nzuri, tuliandaa posters za package ambazo zina taarifa za kutosha. Tutaweka moja baada ya nyingine na kuzifafanua kwa uchache ili mtu awe na chaguo lake.

1. ISTANBUL - VALENTINE's PACKAGE

View attachment 2089317

Package hii gharama yake inaanzia Dola 230 sawa na takribani laki 5 na elfu 30 za Kitanzania.

Yaliyomo:

1. Siku nzima kutembelea majengo ya kihistoria ya utawala wa Ottoman. Utapatiwa na chakula cha mchana.
2. Siku nzima Kubarizi katika njia asili ya maji inayotenganisha bahari mbili. Njia hii ni maarufu kwa jina la Bosphorus. Utapatiwa chakula cha mchana.
3. Utalala siku 4 kwenye hoteli ya nyota 3 na kushinda siku moja. Kifungua kinywa ni bure kuanzia siku ya 2 hadi 5.
4. Ziara zote zilizotajwa hapo juu HUTOLIPIA ikiwemo viingilio katika maeneo ya utalii na mizunguko yote.

Na mengine mengi.

Kwa maswali zaidi na mawasiliano: 0757 212 122 / 0737 555 522
NB: Ofa hii imeanza Januari 15 hadi Machi 31, 2022.

Yes, ukiweka kiasi tajwa unapokelewa Airport (bure), unapelekwa hoteli ya nyota 3 (bure), unaanza tours zote kesho yake na siku zinazofuata (bure), viingilio na watakaokuzungusha (bure), chakula cha mchana huko kwenye tours (bure).

Kwa ufupi gharama za Hoteli, Usafiri kutoka Airport na Tours zote ni BURE baada ya kulipia hicho kiasi cha package.

Gharama PEKEE zitakazokuhusu ni Tiketi ya Ndege, Vipimo vya Uviko na Visa tu!
 
vyote hivi hapa ulivyosema havitakamilika bila KIBUNDA mzee baba

Kiukweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
 
Kiujweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
Hapo kwenye kujua taarifa sahihi ndio tatizo, mfano kwangu sijui
 
Kiukweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
Msaada wa link ninakoweza kupata hizo taarifa
 
Kiukweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
Ndio unataka uanze kutupiga fix. Kwa hiyo hela wangeenda wengi sana nikiwamo mimi.

Anyway tunaomba package zenu kwa destination tofauti tofauti
 
Hebu tangaza biashara vizuri.

Weka packages zenu na huduma mnazotoa pamoja na gharama zake kwa ukamilifu na uwazi kabisa.

Weka Jina la kampuni na physical location pia anonymity ya JF usiilete kwenye biashara.

Relief Mirzska muda wa kuzurura unakaribia.

Hatutangazi biashara mdau wetu Karucee, tunapeana elimu pia manake wengi hawajui hivi vitu.

1. Packages zipo. Tunazo siku zote. Tuitaziambatanisha hapa za msimu huu uangalie unayohitaji.

2. Jina la Kampuni ndio hili hili na akaunti yetu iko verified hapa JF. Hivyo tunatambulika na wala sio anonymous.

3. Physical Location ni Dar es Salaam. Mawasiliano zaidi sheria za JF zikiruhusu tutachapisha pamoja na namba zetu. Vinginevyo tucheki PM.

NB: Tunakubaliana nawe. Mwaka wa kuzurura umewadia!
 
Hebu tangaza biashara vizuri.

Weka packages zenu na huduma mnazotoa pamoja na gharama zake kwa ukamilifu na uwazi kabisa.

Weka Jina la kampuni na physical location pia anonymity ya JF usiilete kwenye biashara.

Relief Mirzska muda wa kuzurura unakaribia.

Ndugu Bonheur Travels Tanzania kwa kuwa umesema kazi yenu ni kuzitoa hizi taarifa sahihi kwa watu wajue kila mtu aweze kumudu, basi kama hutojali tunaomba hizo taarifa za vifurushi/package and gharama zake na taarifa zote sahihi zinazohusu kwenda na kurudi katika nchi husika mtu apendayo
Siyo kwako peke yako. Tumegundua ni tatizo la mindset za Watanzania wengi. Kazi yetu ni kuzitoa hizi taarifa watu wajue kila mtu anaweza kumudu.
 
Ndio unataka uanze kutupiga fix. Kwa hiyo hela wandeenda wengi sana nikiwamo mimi.
Anyway tunaomba package zenu kwa destination tofauti tofauti

Tunaelewa huu mtazamo, wengi wako nao lakini kiuhalisia gharama za kusafiri kwa baadhi ya nchi ni nafuu sana. Ushajiuliza kwanini siku hizi warembo wengi waTanzania wanaruka sana kwenda Uturuki kwa masuala yao ya urembo? Ni nafuu.

Packages zetu tunazipandisha muda wowote kutoka sasa. Baki nasi.
 
Hatutangazi biashara mdau wetu Karucee, tunapeana elimu pia manake wengi hawajui hivi vitu.

1. Packages zipo. Tunazo siku zote. Tuitaziambatanisha hapa za msimu huu uangalie unayohitaji...
hiyo elimu ningependekeza uiweke wazi wadau wote tuone, haya mambo ya ''tucheki DM/PM/INBOX'' yanatia mashaka

Kama ni kampuni halali na iliyosajiliwa na mko verified hapa JF sioni sababu ya kuwa na maneno meeengi bali tunataka tuone hizo habari nzuri.. It is like mnabishana na mteja kwa kitu ambacho ni cha kwenda straight to the point, Mawasiliano yakiwa wazi mtu ndio anakuwa wazi kuja inbox, ofisini au asije. Wengine tuna hisia mbaya tunavyoambiwa njoo inbox kwa ajili ya kuogopa ''upigwaji''
 
Tunaelewa huu mtazamo, wengi wako nao lakini kiuhalisia gharama za kusafiri kwa baadhi ya nchi ni nafuu sana. Ushajiuliza kwanini siku hizi warembo wengi waTanzania wanaruka sana kwenda Uturuki kwa masuala yao ya urembo? Ni nafuu.

Packages zetu tunazipandisha muda wowote kutoka sasa. Baki nasi.
Kuruka kwao hakuwi justified na gharama bali wanachokiendea. Hawa warembo wana mambo mengi ya kiurembo hatuwezi kimbizana nao.
Ili kutujengea mindset unayomaanisha tuwekee detailed package.
 
ndugu Bonheur Travels Tanzania kwa kuwa umesema kazi yenu ni kuzitoa hizi taarifa sahihi kwa watu wajue kila mtu aweze kumudu, basi kama hutojali tunaomba hizo taarifa za vifurushi/package and gharama zake na taarifa zote sahihi zinazohusu kwenda na kurudi katika nchi husika mtu apendayo

Bila shaka. Baki nasi hapa. Tutazichapisha hivi punde kwa ukamilifu wake. Huu mwaka tunataka angalau watu kadhaa kutoka JF wakatalii walete mrejesho hapa.
 
hiyo elimu ningependekeza uiweke wazi wadau wote tuone, haya mambo ya ''tucheki DM/PM/INBOX'' yanatia mashaka

Kama ni kampuni halali na iliyosajiliwa na mko verified hapa JF sioni sababu ya kuwa na maneno meeengi bali tunataka tuone hizo habari nzuri.. It is like mnabishana na mteja kwa kitu ambacho ni cha kwenda straight to the point, Mawasiliano yakiwa wazi mtu ndio anakuwa wazi kuja inbox, ofisini au asije. Wengine tuna hisia mbaya tunavyoambiwa njoo inbox kwa ajili ya kuogopa ''upigwaji''

Umeeleza vizuri sana mkuu. Ni hofu tu ya sheria za JF isije kuonekana tunafanya matangazo lakini hatuna tatizo kuchapisha na kutoa taarifa zote. Tutafanya hivyo punde na watu wachague wenyewe. Baki nasi.
 
Basi sawa na sidhani kama sheria za JF zinakataza kwa sababu kuna jukwaa la matangazo, na kama ni realistic basi tuone uhalisia na mirejesho

Isije ikawa unapigia promo kampuni za michongo halafu raia wakaishia kupigwa (mkaonekana matapeli, aisee kula hela ya mtu kirahisi tu itakutafuna)
 
Kiukweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
Asante, hebu tuletee chap hizo packages tuzione katika uwazi, naweka kambia hapa
 
Asanteni WanaJF kwa utayari. Pia maoni na mapendekezo kuwa tuweke packages tulizonazo msimu huu, japo lengo letu lilikuwa kuambizana tu na haikuwa na ulazima msafiri kupitia huduma zetu. Ni heshima kubwa mmetupatia.

Kwa bahati nzuri, tuliandaa posters za package ambazo zina taarifa za kutosha. Tutaweka moja baada ya nyingine na kuzifafanua kwa uchache ili mtu awe na chaguo lake.

1. ISTANBUL - VALENTINE's PACKAGE

Istanbul Turkey.jpg

Back
Top Bottom