Huu ni mwaka wa kusafiri sana kuifaidi dunia

Huu ni mwaka wa kusafiri sana kuifaidi dunia

Yes, ukiweka kiasi tajwa unapokelewa Airport (bure), unapelekwa hoteli ya nyota 3 (bure), unaanza tours zote kesho yake na siku zinazofuata (bure), viingilio na watakaokuzungusha (bure), chakula cha mchana huko kwenye tours (bure....
Hapa ndiyo umeeleweka, tofauti na Blablaa ulizokuwa unatupigia!!
 
Duh changamoto ni gharama ya tiketi ya ndege, nimecheki Qatar airways mpaka Istanbul ni dola 1500 hivi, jumla na return ticket ni kama dola 3000 hivi, hivyo sio poa cha msingi tutafute nauli tu wakuu, ila kuzurura huko ulaya sio ghali
yaani nilipie milioni 6+ kwaajili ya nauli halafu nishindwe kulipia laki 5 ya kuzurura nianze kuwatafuta hawa jamaa hiyo itakuwa akili au kaili..
 
Duh changamoto ni gharama ya tiketi ya ndege, nimecheki Qatar airways mpaka Istanbul ni dola 1500 hivi, jumla na return ticket ni kama dola 3000 hivi, hivyo sio poa cha msingi tutafute nauli tu wakuu, ila kuzurura huko ulaya sio ghali

Umechagua shirika la ndege ghali duniani. Hata hivyo ukikata tiketi mapema (go & return) gharama inapungua sana.

Kwa bahati nzuri, moja ya huduma zetu ni ukatishaji tiketi, hivyo tunaweza kukuangalizia ndege zinazoenda Uturuki kwa gharama nafuu na tukakusimamia hadi siku utakayosafiri usipate usumbufu wowote. Faida nyingine utakayopata ni kupunguziwa bei kwa sababu tayari tuna mkono mrefu kwenye baadhi ya mashirika ya ndege.

Mawasiliano: 0757 212 122 / 0737 555 522

Karibu.
 
Asanteni WanaJF kwa utayari. Pia maoni na mapendekezo kuwa tuweke packages tulizonazo msimu huu, japo lengo letu lilikuwa kuambizana tu na haikuwa na ulazima msafiri kupitia huduma zetu. Ni heshima kubwa mmetupatia...
Gharama za usafiri kutoka Tanzania hadi Uturuki kwenda na kurudi ni kwa dola hizo 230 jumulisha malazi na sehemu za utalii ama inakuwaje?

Mbona napata wasiwasi?
 
Kiukweli tatizo sio kibunda bali ni taarifa mkuu Joseverest. Watanzania wengi hawajui kuwa baadhi ya safari za kutalii nje ya nchi ni cheap zaidi kuliko hata za hapa ndani.

Mfano katika Msimu huu zipo packages za kwenda Uturuki na gharama inaanzia laki 5 tu ($230) kwa siku 4 hadi 5. Utashindwaje hapo?
Mkuu hebu tusaidie mchanganuo $230 nauli kwenda na kurudi bei gani? Siku 4/5 kwa siku bei gani?
 
Asanteni WanaJF kwa utayari. Pia maoni na mapendekezo kuwa tuweke packages tulizonazo msimu huu, japo lengo letu lilikuwa kuambizana tu na haikuwa na ulazima msafiri kupitia huduma zetu. Ni heshima kubwa mmetupatia....
Nina maswali kadhaa;
1.Je hii ni tour ya siku 5?na katika hizo siku tano kuna siku 1 ya safari ya kwenda(kama ni safari ya siku 1) na moja ya kurudi?maana yake kuna siku mbili zimetoka zinabaki 3 za kutalii Instanbul?naomba ufafanue.

2.Umesema mtu atalala siku 4 kwenye hoteli ya nyota tatu na kushinda siku moja hotelini ,fafanua unamaanisha nini?

3.Hiyo siku moja ya kushinda hotelini chakula cha mchana na jioni nani analipia(maana umesema kifungua kinywa ni bure siku ya( 2-5)?

4.Siku ya kwanza na ya pili kutalii umesema chakula cha mchana tutapatiwa,Je chakula cha jioni nani analipia?

5.Kama jibu la namba 3 anayelipia chakula ni mtalii mwenyewe,tupe bei ya chakula kwenye hio hoteli ya Nyota 3.(Jibu hili pia linahusiana na swali la 4)

5.Vipi akitokea mtu akapata dharura kama ya kuugua akiwa ugenini mnamsaidije au kuna utaratibu gani?

Naomba ujibu kwa namba.

Ahsante.
 
Gharama za usafiri kutoka Tanzania hadi Uturuki kwenda na kurudi ni kwa dola hizo 230 jumulisha malazi na sehemu za utalii ama inakuwaje?

Mbona napata wasiwasi?

Labda kwa train ya mwendo kasi haha huyu anautani kutoka bongo had Kenya tu kwa Ndege haitoshi hiyo ndio itakua uturuk hahaha
 
Tunaelewa huu mtazamo, wengi wako nao lakini kiuhalisia gharama za kusafiri kwa baadhi ya nchi ni nafuu sana. Ushajiuliza kwanini siku hizi warembo wengi waTanzania wanaruka sana kwenda Uturuki kwa masuala yao ya urembo? Ni nafuu.

Packages zetu tunazipandisha muda wowote kutoka sasa. Baki nasi.

Hii true Nchi kama Bulgaria vitu cheaper sana tena inaeza kuwa zaidi ya Bongo gharama kwenye usafiri tu
 
Nina maswali kadhaa;
1.Je hii ni tour ya siku 5?na katika hizo siku tano kuna siku 1 ya safari ya kwenda(kama ni safari ya siku 1) na moja ya kurudi?maana yake kuna siku mbili zimetoka zinabaki 3 za kutalii Instanbul?naomba ufafanue.

2.Umesema mtu atalala siku 4 kwenye hoteli ya nyota tatu na kushinda siku moja hotelini ,fafanua unamaanisha nini?

3.Hiyo siku moja ya kushinda hotelini chakula cha mchana na jioni nani analipia(maana umesema kifungua kinywa ni bure siku ya( 2-5)?

4.Siku ya kwanza na ya pili kutalii umesema chakula cha mchana tutapatiwa,Je chakula cha jioni nani analipia?

5.Kama jibu la namba 3 anayelipia chakula ni mtalii mwenyewe,tupe bei ya chakula kwenye hio hoteli ya Nyota 3.(Jibu hili pia linahusiana na swali la 4)

5.Vipi akitokea mtu akapata dharura kama ya kuugua akiwa ugenini mnamsaidije au kuna utaratibu gani?

Naomba ujibu kwa namba.

Ahsante.

Maswali mazuri, tutajitahidi kuyafafanua kama ifuatavyo:

1. Ukisoma maelezo ya package utaona kuna siku 4 hadi 5 za kuwepo huko. Siku zinaanza kuhesabika pale utakapopokelewa kwenda hotelini.

2. 4 nights / 1 day maana yake hiyo siku ya 5 ndiyo siku ya ku-checkout hotelini. Hutaweza kulala ila utaruhusiwa kucheck out muda wowote ndani ya siku hiyo.

3. Package imeainisha kuwa hotelini utapatiwa breakfast tu na kwenye tours lunch tu. Hiyo ndiyo ofa ya package. Huduma nyingine zozote nje ya hapo ni mapendeleo yako.

4. Kama jibu la swali namba 3.

5. Gharama za vyakula inategemea na chaguo la chakula unachohitaji. Ni ngumu kutaja bei moja.

6. Masuala ya dharura yapo kwenye sera za hoteli na camps utakazofikia.

Ni matumaini yetu tumejibu maswali yako mkuu Farolito.
 
Mambo yawe wazi isijekuwa kama ya yule mdau aliyelipia kwenda kutalii kalipia kila kitu mwisho wa siku simu hazipatikani,uaminifu umekua mdogo Kweli Kwenye haya mambo ya online

Sahihi kabisa. Ndiyo maana tunajibu kila kitu kwa uwazi na kufafanua ili kuondoa mashaka na wasiwasi. Kwa bahati nzuri hatutapokea pesa ya mteja mpaka atakapojiridhisha na huduma. Tunaaminika ndiyo sababu JF ikatupa verification badge baada ya kuwatumia documents zote halali.
 
Back
Top Bottom