Asanteni WanaJF kwa utayari. Pia maoni na mapendekezo kuwa tuweke packages tulizonazo msimu huu, japo lengo letu lilikuwa kuambizana tu na haikuwa na ulazima msafiri kupitia huduma zetu. Ni heshima kubwa mmetupatia.
Kwa bahati nzuri, tuliandaa posters za package ambazo zina taarifa za kutosha. Tutaweka moja baada ya nyingine na kuzifafanua kwa uchache ili mtu awe na chaguo lake.
1. ISTANBUL - VALENTINE's PACKAGE
View attachment 2089317
Package hii gharama yake inaanzia Dola 230 sawa na takribani laki 5 na elfu 30 za Kitanzania.
Yaliyomo:
1. Siku nzima kutembelea majengo ya kihistoria ya utawala wa Ottoman. Utapatiwa na chakula cha mchana.
2. Siku nzima Kubarizi katika njia asili ya maji inayotenganisha bahari mbili. Njia hii ni maarufu kwa jina la Bosphorus. Utapatiwa chakula cha mchana.
3. Utalala siku 4 kwenye hoteli ya nyota 3 na kushinda siku moja. Kifungua kinywa ni bure kuanzia siku ya 2 hadi 5.
4. Ziara zote zilizotajwa hapo juu HUTOLIPIA ikiwemo viingilio katika maeneo ya utalii na mizunguko yote.
Na mengine mengi.
NB: Ofa hii imeanza Januari 15 hadi Machi 31, 2022.