DOKEZO Huu ni ugonjwa gani? Wizara ya Afya semeni kitu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kuna hii video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, huyo jamaa anasema wako katika hospitali maeneo ya kipawa majani ya chai.

Ambako yeye na wengine wanaumwa ugonjwa kama huo wametengwa, hawaruhusiwi kuonana na watu.

Kuna ka ujumbe kanapita kanasema tuache kupeana mikono hovyo, maana hujui nani ako nao.

Wizara ya Afya Tanzania huu ni ugonjwa gani?

Majibu ya Wizara ya Afya: News Alert: - Wizara ya Afya yathibitisha uwepo wa wagonjwa wawili wa Mpox nchini
 
Monkeypox 😬😔
Labda wanajaribu kuicontain isisambae.

chicken-pox-vs-monkey-pox-1.jpg
 
Wakuu,

Kuna hii video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, huyo jamaa anasema wako katika hospitali maeneo ya kipawa majani ya chai.

Ambako yeye na wengine wanaumwa ugonjwa kama huo wametengwa, hawaruhusiwi kuonana na watu.

Kuna ka ujumbe kanapita kanasema tuache kupeana mikono hovyo, maana hujui nani ako nao.

Wizara ya Afya Tanzania huu ni ugonjwa gani?

View attachment 3264801
Nadhani hiyo ni wazi ni Monkey Pox. Ndio video za watu wenye huo ugonjwa sehemu mbali mbali huku afrika wanakuwa hivyo.

Ni serikali yetu tu inaficha ficha lakini hao wagonjwa wa dizaini hiyo wametapakaa karibu nchi nzima. Mtu akigundulika anapelekwa na mamlaka za serikali kwenye vituo vya afya mafichoni na hautasikia wakisema au wakipewa majibu.
 
Mtindo wa kuficha ni ule ule kwa serikali yetu, ni kama walivyoficha kwenye Marburg Virus (Ebola fulani hivi) kule Kagera mpaka tukasikia kichini chini kuwa mkurugenzi mkuu wa WHO akaamua kutua mwenyewe hapa nchini ili kumwambia Rais hicho kinachofichwa ni hatari kwa dunia, sasa ili kuzuga na kufunika kombe ikabidi Rais ajifanye hana taarifa rasmi na hapo hapo akamfukuza Mganga mkuu wa serikali na kuteua katibu mkuu mpya wa wizara ya Afya na akatoa hotuba rasmi ya kutangaza uwepo wa Marburg hapa.

Serikali iseme tu sasa kuwa kuna Monkeypox yakutosha ili hatua madhubuti zichukulie.
 
Walifanya research na kugundua hamna ugonjwa huo, walirudi ikulu na vyombo vya habari vilirusha, jamaa alisema hamna ugonjwa husika.

Second. Nyie mnaosema huu ugo hwa unafichwa upo, ni wangapi, mmeshuhudia marburg maeneo yenu au watu kuchukuliwa.

Hata huyu story yake ni kwamba alifika hospitali akapewa kitanda sehemu ya kivyake na wagonjwa wengine na tunawaona hapo, na pia wagonjwa hao unaweza kuwaona ila kupitia dirishani, my people mbona mnapenda sana story muonekane mnajua.
 
Huku mtaani kwetu kuna shoga aliumwa huu ugonjwa, madaktari walikuja kumchukua wamejifunika mwili mzima na walipulizia nyumba yake dawa.
Na kwa jinsi kina dada mnakuaga na urafiki na hao watu, na wewe ukapime mkuu
 
Wakuu,

Kuna hii video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, huyo jamaa anasema wako katika hospitali maeneo ya kipawa majani ya chai.

Ambako yeye na wengine wanaumwa ugonjwa kama huo wametengwa, hawaruhusiwi kuonana na watu.

Kuna ka ujumbe kanapita kanasema tuache kupeana mikono hovyo, maana hujui nani ako nao.

Wizara ya Afya Tanzania huu ni ugonjwa gani?

View attachment 3264801
Anatia huruma kweli jamani 😔
 
Mtindo wa kuficha ni ule ule kwa serikali yetu, ni kama walivyoficha kwenye Marburg Virus (Ebola fulani hivi) kule Kagera mpaka tukasikia kichini chini kuwa mkurugenzi mkuu wa WHO akaamua kutua mwenyewe hapa nchini ili kumwambia Rais hicho kinachofichwa ni hatari kwa dunia, sasa ili kuzuga na kufunika kombe ikabidi Rais ajifanye hana taarifa rasmi na hapo hapo akamfukuza Mganga mkuu wa serikali na kuteua katibu mkuu mpya wa wizara ya Afya na akatoa hotuba rasmi ya kutangaza uwepo wa Marburg hapa.

Serikali iseme tu sasa kuwa kuna Monkeypox yakutosha ili hatua madhubuti zichukulie.

Tatizo la ulimwengu wa tatu ni ulimbukeni wa technologia;
Taarifa ya Case moja au mbili ya kitu chochote inaweza kusambaa Nchi nzima kwa muda mfupi sana.
Sasa kwa sababu akili zetu hazina uwezo wa kufilter kuwa ni case hiyo hiyo au ni picha hiyo hiyo inasambaa Nchi nzima; Huweza kuleta hofu na taaruiki hata pale ambapo hapakuwa na sababu ya kupanic...
Technologia imesambaa ulimwengu wa tatu kwa kasi wakati watu hawajaelimika vya kutosha kuipokea!
KIMSINGI TAARIFA HAZIFICHWI ILA WANANCHI WALIO WENGI HAWAJUI KUCHAKATA TAARIFA!
 
Back
Top Bottom