Upo Tanzania?
Unataka kusema Rais Samia alidanganya kwa kutangaza rasmi akiwa Ikulu kuhusu kupatikana kwa wagonjwa wa Marburg hapa Tanzania?
Upo Kagera?
Njoo Kagera tukuonyeshe makaburi ya watu waliokufa kwa Marburg na kuzikwa kistyle zile za kiserikali-afya.
Upande wa pili, inakuwaje kusiwe na Marburg kule Kagera halafu zaidi ya wataalamu 100 wa magonjwa ya mlipuko kutoka wizara ya afya watie kambi kule Kagera zaidi ya mwezi mzima sasa, wakifanya kazi za afya huku wakiwa na vifaa vyote kinga dhidi ya Marburg, kutoa elimu ya kujikinga na kuweka matangazo ya kupambana na Marburg mkoa mzima.
Yote kwa yote hao kwenye video ni wagonjwa Mpox hapo Dar, watu wengi wanajua hilo na hata ndugu zao wameshaelezwa kimya kimya, ni video imetrend mitandaoni mapema sana, na wala hakuna ubishi kila kitu kinafanana na video zingine za wagonjwa wa Mpox hapa Afrika. Hakuna cha ajabu wala kuficha, iko wazi mnoo.