Mtindo wa kuficha ni ule ule kwa serikali yetu, ni kama walivyoficha kwenye Marburg Virus (Ebola fulani hivi) kule Kagera mpaka tukasikia kichini chini kuwa mkurugenzi mkuu wa WHO akaamua kutua mwenyewe hapa nchini ili kumwambia Rais hicho kinachofichwa ni hatari kwa dunia, sasa ili kuzuga na kufunika kombe ikabidi Rais ajifanye hana taarifa rasmi na hapo hapo akamfukuza Mganga mkuu wa serikali na kuteua katibu mkuu mpya wa wizara ya Afya na akatoa hotuba rasmi ya kutangaza uwepo wa Marburg hapa.
Serikali iseme tu sasa kuwa kuna Monkeypox yakutosha ili hatua madhubuti zichukulie.