Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Hivi kweli wahariri zaidi ya 50 mliohudhuria mkutano wa Rais Samia suluhu Hassan mmeshindwa kuuliza maswali mazito yanayotesa taifa kwa miaka mitano mizima ambayo mwenye majibu ni Rais wa Nchi ya Tanzania? Mfano hata hili la kikatiba juu ya Wabunge waliopo bungeni bila kuwa na chama cha siasa mmeshindwa kuuliza?
Enyi Wahariri ni kweli hamjui ama kulikuwa na maelekezo ya kuzuia baadhi ya maswali? Hamjui kuwa Kwamjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, "Msimamizi Mkuu wa Katiba na Sheria za nchi, ni Serikali. Mamlaka yote ya Serikali yapo mikononi mwa Rais. Hivyo, Msimamizi mkuu wa Utii wa Katiba na sheria ni Rais. ibara za 33 na 34 zipo wazi. Rais anawajibu kulinda sheria na katiba zisivunjwe na mhimili wa Bunge"
Je kuwepo na Wabunge wasio na vyama vya siasa Bungeni wahariri hili hamkulioni ama hamkukumbuka?
Wahariri wa Tanzania mkashindwa kuuliza Watu wasuojulikana wameshughulikiwaje? Mkashindwa kuuliza aliko Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengine? Mkashindwa kuuliza nani alimpiga risasi Tundu Lussu?
Wahariri wa Tanzania Mkashindwa kuuliza kauli na msimamo wa Rais kuhusu Watanzania walioikimbia nchi kunusuru maisha yao katika utawala wa Magufuli mfano Lissu, Ngurumo, Lema nk?
Nafasi mliyoipata jana ilikuwa ni ya dhahabu na umma uliwategemea kuondoa mtanziko wa miaka 5 iliyopita, Mmeipoteza na mmesaliti umma. Umma hautapata tena nafasi ya aina hii. Umma ulitegemea uondoe zile dhana tata juu ya wasiojulikana, juu ya wabunge tata, juu ya mambo mengi yasiyo na majibu. Lakini mategemeo yametegea.
Wasaliti wakubwa nyie! Hamfai Msikitini, Hamfai Kanisani.... Wala kwenye dini yangu ya Mizimu hamfai.
Au juice za Ikulu ziliwasahaulisha? Ok kivuli cha Dikteta Magufuli bado kimetanda baadhi ya maeneo.