ruralofficer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2014
- 2,494
- 3,630
Unatakiwa kufahamu haya mambo;Mfano matumizi ya neno la kiswahili BARAZA kufasiri maneno yafuatayo.
Veranda-BARAZA
Cabinet-BARAZA La Mawaziri
House of Representative-BARAZA La Wawakilishi
Ward Tribunal-BARAZA La Kata
Court Assessors-Wazee wa BARAZA
Rejea pia BARAZA la madiwani.
Huu ni ushahidi wa uhaba mkubwa wa misamiati unaokikumba kiswahili.
Sent using Jamii Forums mobile app
1.Hakuna lugha inayojitosheleza
2.Hakuna lugha bora kuliko nyingine.
3.Lugha zinatabia ya kukopeshana misamiati kutokana na point namba 1.(mfano ukifungua oxford dictionary utakutana na neno UGALI kama lilivyo halina kiingereza chake.
4.Ni ukweli usiopingika lugha ya kiingereza ina utajiri mkubwa wa misamiati kutokana na sababu nyingi tu (za kihistoria na za maendeleo ya sayansi na technolojia)lakini point namba moja itasimama kama ilivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app