Huu ni ushahidi kuwa lugha ya kiswahili hakijitoshelezi (ina uhaba mkubwa wa misamiati)

Unatakiwa kufahamu haya mambo;
1.Hakuna lugha inayojitosheleza
2.Hakuna lugha bora kuliko nyingine.
3.Lugha zinatabia ya kukopeshana misamiati kutokana na point namba 1.(mfano ukifungua oxford dictionary utakutana na neno UGALI kama lilivyo halina kiingereza chake.
4.Ni ukweli usiopingika lugha ya kiingereza ina utajiri mkubwa wa misamiati kutokana na sababu nyingi tu (za kihistoria na za maendeleo ya sayansi na technolojia)lakini point namba moja itasimama kama ilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila lugha ni hivyo hivyo. Angalia:

Mama mdogo - aunt
Shangazi - aunt

Baba mdogo - uncle
Mjomba - uncle

Wifi - sister in law
Shemeji - brother in law/sister in law.
 
Sio kwamba 60%ya maneno ya kifaransa ni ya kingereza?


Hapana ni kinyume chake, Kiingereza imechukuwa maneno karibia yote kutoka kwenye Kifaransa. Kifaransa ni Lugha ya jamii ya Kilatini, na bila ya Kilatini Kiingereza ni lugha masikini sana kuliko labda hata Kiswahili, maneno asilia ya Kiingereza ni machache sana!
 
Kiingereza chenyewe kina maneno mengi tu kutoka kifaransa na Lugha nyinginen ila haibadili haja ya kukiita Kiingereza. Kwa nini Kiswahili kisiitwe hivyo. Hao wasomi kabla ya usomi wao walikuwa wakiongea lugha gani, baada ya kujua Kiingereza ndio Kiswahili wanakisahau?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapo ni Kiswahili au Kiingereza kisichojitosheleza? Kama tabasamu inaeleweka ni nini, kuwa na maneno sita kuelezea hali moja ndio kutokujitosheleza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kiswahili kipana sana japo hakuna lugha inayojitosheleza duniani na kinaweza kufafanua maana 1 ktk maneno zaidi ya 7-8 tofauti tofauti.

Mfano:

Kuongea = Kueleza
= kuambia
= kunena
= kusema
= kutamka
= kubonga
= kulonga.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa maana hata mie huwa nakishangaa kiingereza kilivyoishiwa misamiati pia.

Mfano neno right.

1. Right now = sasa hivi
2. Right hand = mkono wa kulia
3. Right man = mtu sahihi
4. Rights = Haki

[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
Hoja ya mtoa mada ni dhaifu kuwa Duniani kote, hakuna lugha inayoweza kuelezea maarifa yote. Kwa mantiki hiyo Kiswahili, kama zilivyo lugha nyingine kinaweza azima msamiati kutoka lugha yoyote ili kujenga dhana na maarifa kiyatakayo.
 


Neno lipi la kisayansi ni la kingereza Mkuu??
 
Hivi unajua lugha zenye chembe za ukamilifu duniani ni kiarabu na kilatini tu... Hata hiyo unayoiona imekamilika kama kisingekuwepo kilatini kisingefika kokote
 
Lithium

The origin of the name comes from the Greek word lithos meaning stone , apparently because it was ...
 
Mama mdogo...aunt
Mama mkubwa...aunt
Shangazi....aunt
Je kingereza hakijitoshelezi? Utoshelevu wa lugha tunaipima kwa watumiaji wake kuweza kueleza vitu mbalimbali kwa kutumia lugha hiyo hicho kigezo hata wenye kingereza wanaipinga na kusema kila lugha hijitosheleza kulingana na mahitaji...pitia upya maarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kingereza kimeathiriwa sana kifaransa pamoja na lugha za mashariki ya kati.... Ni tabia ya lugha kuathiri na kuathiriana ...rudi kupitia mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivyo tujaribu Kijapan (hata Kiingereza hakifai). Linganisha Kiingereza na Kijapan hapa chini:

Your WIFE - Okusan

My WIFE - Tsuma

Your HUSBAND - goshujin

My HUSBAND - Oto

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…