goodhearted
JF-Expert Member
- Feb 15, 2015
- 1,079
- 1,406
Ni mtoto wa jamaa yangu. Huyu kijana ana miaka 12 tu ila amemtoa jasho jembamba jamaa yangu . Mtoto alianza kwa kukataa shule akienda shuleni anaishia kujificha anakuwa hafiki. Alipogundulika kuwa hafiki shule akatoroka nyumbani. Ameishi kwa kujificha ficha huko mitaani huku akitafutwa takribani wiki alipopatikana akatorokea kwa bibi yake.
Ikabidi ahamishiwe huko kimasomo lakini mwendo umekuwa ule ule tu. Mtoto akifanya makosa huondoka nyumbani na kwenda kuishi mitaani huku akiomba omba chakula kama asiye na wazazi
Aliwahi kupelekwa polisi kama kumtisha ili atulie ni kweli alitulia lakini baada ya kama wiki moja mwendo ukawa ni ule ule.
Ndugu wengine wame connect na imani za kishirikina kwamba mtoto amechezewa. Anaweza aondoke nyumbani kwa kufanya makosa au kwa hiari na kurudi ni mpaka atafutwe. Na akirudi atajituliza siku 2 au 3 na ataanza tena