Huu ni wakati wa kusimamia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Huu ni wakati wa kusimamia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge lipi ilo mkuu? Au unasema like lililo chini yake.
Kuingiria haki ya vyama vya Siasa sini kinyume cha Katiba mkuu...
Jikite kwenye mada, usilete hoja kwa hisia. Siku akiharibu ndio utajua bunge linaweza kumg'oa.
 
Kijana naomba tuheshimiane, lini Ccm walichukua ubongo wangu? Lini nimeongea pumba? Mimi ni mtu ninaejitambua.
Hata hii ya leo ni pumba tu, katiba iheshimiwe leo?! Kwani kuiba kura, kumrudisha Mwambe bungeni, kuwakingia kifua Lijuhakali na Silinde, ni kulinda katiba?! Pumba tu, kama kawaida yako!
 
Hata hii ya leo ni pumba tu, katiba iheshimiwe leo?! Kwani kuiba kura, kumrudisha Mwambe bungeni, kuwakingia kifua Lijuhakali na Silinde, ni kulinda katiba?! Pumba tu, kama kawaida yako!
Dogo huwezi kufanya uchaguzi miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu. Kwa ishu ya Mwambe na akina Silinde Ayubu alikuwa sawa kisheria. Sio hii bado miaka minne na miezi kadhaa. Hapa hamna pumba tumia akili kabla ya kupanic!
 
Dogo huwezi kufanya uchaguzi miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu. Kwa ishu ya Mwambe na akina Silinde Ayubu alikuwa sawa kisheria. Sio hii bado miaka minne na miezi kadhaa. Hapa hamna pumba tumia akili kabla ya kupanic!
U-dogo unaishia umri gani huko kwenu?
 
Hata kuua
Mawazo yako ndio hali inavyotakiwa kuwa, lakini nani anafuata Katiba kwa sasa. Uliyemtag ameshasema atawalinda kina HALIMA kwa gharama yoyote. GHARAMA YOYOTE ni pamoja na kuvunja katiba.
 
Taifa letu tangu limepata uhuru limekuwa likitawaliwa kwa misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi yetu

Ndio maana hatuoni nchi hii ikiendeshwa kwa presidential decrees au ubabe na udikteta.

Tulishuhudia bunge la kumi jinsi lilivyoweza kuiadhibu serikali kwa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wakati huo. Na kila mtu alishangaa kwa namna serikali ilivyowajibika kama ibara ya 53A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inavyosema.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mbunge akifukuzwa uanachama, Mbunge huyo hupoteza uanachama wake. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 67(1)(b). Kwa hiyo Mbunge akifukuzwa uanachama wa chama chake basi hana shavu tena.

Kwa hiyo ili amani kwenye Taifa lolote ili amani itamalaki lazima Katiba ya Taifa hilo iheshimiwe na kusimamiwa.

Hivyo basi Spika wa Bunge letu aheshimu na kusimamia misingi ya katiba yetu. Kama kweli Halima Mdee na wenzake 18 wamefukuzwa uanachama CHADEMA basi sio wabunge halali tena. Watanzania tunaopenda utawala wa sheria tutashangaa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwakingia kifua watu kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hizi Id zako mbili leo unajifanya akili zimekurudia. Mbona Cecil Mwambe alirudi bungeni kwa kuitwa na spika na wala hukuhoji ule uhuni? Tatizo la sheria za nchi yetu kutokuheshimiwa ni kwa maagizo ya jiwe. Hata uchaguzi huu yeye ndio aliagiza unajisiwe na kila mtu hilo analijua.
 
Nani yupo juu ya sheria hapa Tanzania? Hujui kuwa bunge linamlaka ya kumvua urais kama atatumia madaraka yake vibaya?

Sio hili bunge kibogoyo. Hilo bunge la watoa rushwa na wezi wa kura. Nusu ya wabunge wa ccm wako bungeni kwa kura za tiss na tume ya uchaguzi, wabunge wa aina hiyo wanaweza kufanya nini la maana?
 
Back
Top Bottom