Huu ni zaidi ya wizi mashabiki wa simba na Yanga Amkeni kwenye huo usingizi mzito.

Huu ni zaidi ya wizi mashabiki wa simba na Yanga Amkeni kwenye huo usingizi mzito.

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili saini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao uligharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 na ulipaswa kukamilika Julai 2024.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja.

Maeneo yaliyopangwa yakarabatiwe ni pamoja na.
1. vyumba vya wachezaji,
2. chumba cha waandishi wa
Habari,
3.Eneo la watu mashuhuri (VVIP), 4. kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo,
5. ubao wa kuonesha matokeo,
kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba,
7. mfumo wa umeme,
8. mfumo wa sauti,
9. Eneo la kukimbilia wanariadha, 10. chumba cha VAR,
11. lifti mbili mpya,
12. mfumo wa taa,
13. mfumo wa maji taka,
14. mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.

INASIKITISHA SANA.
 
Back
Top Bottom