Uchaguzi 2020 Huu u-chifu Zanzibar unakubalika?

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Naona huko Zanzibar mnaleta mambo ya ki-chifu.
  • Abeid Amani Karume-Rais wa Kwanza Zanzibar
  • Aman Abeid Karume- Rais Mstaafu Zanzibar
  • Ali Hassan Mwinyi -Rais Mstaafu Zanzibar na Tanzania
  • Hussein Mwinyi -Mgombea urais 2020
  • Ali Karume -Mgombea urais 2020
Hii yote ni himaya ya CCM, ndugu Watanzania tuwe macho na machifu hawa tuwakatae.
 
Kama wanna Sifa sioni shida na hussen Katia Nia na sio kawa rais. Mbarawa kuchukua au kakatwa kuchukua fomu?
 
ukoo wa ubwenyenye tupu hapo watoto wa walalahoi hawatii mguu,dah ccm bhana
 
Alivyowafanyia watumishi hakika Mungu yupo.Miaka yote 5 ni kapa huku wakidhalilika kwa hali ngumu ya maisha huko mtaani.Poleni walimu,madaktari,wauguzi etc
 
Mwongeze na wakili Machachari na Rais msataafu Fatma Karume.
 
Nimemsikia Dr. Hussein Alli Mwinyi kuchukua fomu za kugombea Urais wa Tanzania Visiwani(Zanzibar). Dr. Hussein ni mtoto wa Rais mstaafu wa JMT, Mzee Alli Hassan Mwinyi(1985-1995).

Lakini pia nimemsikia Balozi Ali Amani Karume kuwa naye kachukua fomu. Balozi Ali ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar(1964~1972)Marehemu Abedi Amani Karume.

Balozi Ali pia ni mdogo wake Abedi Karume Rais mstaafu wa awamu ya 6(2000~2010)aliyekabidhi kijiti kwa Dr. Shein.

Iwapo CCM watampitisha mmoja wa 2 Hawa yaani Dr. Hussein Mwinyi au Balozi Ali Karume basi itakuwa ni kuendeleza USULTANI ambao wanamapinduzi wa Zanzibar chini ya ASP walimtimua Mwarabu kupinga USULTANI!

Hatutaki kusikia Habari ya Hussein Mwinyi wala Balozi Karume! Zanzibar au Bara tuna Watz wengi tu wenye Uwezo wake kuongoza hivo hakuna haja ya Familia moja kuwa inarithishana Utawala....huo Ni USULTANI na UFALME usio na tija kwa wote Bara na Visiwani.
 
Kwamba mnafaa hilo halina upinzani, mmefanya mengi ya kutukuka Nchi inajua Mbali na hayo wazazi wenu wamekuwa maRais wa Nchi na Karume ni zaidi mpaka Kaka kawa Rais, Maono ya Wazazi wenu ndiyo mnayotembea nayo na kusema kweli ni maono ya kutukuka.

Lakini wapo wazanzibari wengi wenye maono mbadala pengine zaidi ya mliyonayo ktk kulinda Muungano na kudumisha mapinduzi matukufu na kwa bahati mbaya hawajapata nafasi.

Jifunzeni kwa Nyerere lakini ukichukua Bara watu 40 waliokuwa wamejipanga kwa Urais 2015 isingetumika hekima ya kiMungu JPM asingepata nafasi. Leo hii tunamwita shujaa wa Afrika kwa Kazi mliyofanya ni kubwa msiitie doa ridhikeni waachie wengine.
 
Hayo mambo yote wanayoyapanga ni ccm, sisi wananchi tuko undercontrol ya ccm, wanachoamua wao ndio hichohicho amna kubadilisha, kama upinzani Zanzibar walishinda thn eti matokeo yakaghairishwa na alaf ukafamyika uchaguzi mpya.

Basi tambueni kuwa ccm itatawala daima na daima mpka pale wananchi watakapoamua wenyewe, chochote kinachofanyika usilalamike, ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
 
Wacha tuu znz itawaliwe KIFALME Kama uarabuni. HAKUNA namna nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…