matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Dunia inamengi.
Kuna mshkaji wangu amefungua biashara mahala hapa jijini. Mambo yanaenda kasi na anafanikiwa kiasi kwamba aliowakuta wengine wanafikiria kufunga wengine wamepata presha kwa kuhofia hatma yao.
Ghafla vita vikali vikaanza. Kama kawaida sisi watu wa dua huwa hatushindwi na ushirikina. Kila shambulio tulihakikisha linapanguliwa na dua. Mwenyewe nimeshiriki kutia dua kwenye hiyo bizness.
Juzi kaja dada mmoja katumwa kaanza kutukana matusi na kulazimisha ugomvi (huku waliompanga wamekaa kwa mbali wanafuatila mchakato waliouset ), dua zikatuelekeza kunyamaza kimya. Kataka kurusha hadi mawe, sisi kimya. Alipoona lengo halitimii akaamua kuondoka.
Mfanya biashara pembeni akatutonya kuwa mmeepusha jambo kubwa. Huo uchawi upo, mtu anatumwa kuja kukuchokoza ili upaniki na kujibishana. Ukifanya hivyo tu unakuwa umefungua njia ya ule uchawi kufanya kazi. Yule jamaa akadai kwao watu wanapigwa sana kwa njia hiyo. Basi tukamwambia haina shida huku tukijua dua hupangua hila zote za kishirikina.
Note: Mimi ni mshauri wa kiroho kwenye biashara ya mdau wangu na nimekuwa nikifika hapo mara kwa mara kumuongezea nguvu ili apige pesa zaidi.
Ni hayo tu.