Huu ugonjwa bado unaogopeka na wagonjwa bado wananyanyapaliwa

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Jana katika tembea tembea zangu nikakutana na mmama anatembea kwa miguu, tukiwa umbali wa meter kama 100 hivi yule mmama alidondosha kitu akaacha kukiokota akawa anaendelea kutembea, kwa mbali naona ishara za watu wakistua nimstue yule mama arudie kitu alichodondosha nami sikuelewa tukapishana kila mtu na zake

Kusogea mbele nakuta kumbe alidondosha dawa ni nyingi sana yaani zimetapakaa njia nzima na nikubwa kiasi, zimekaa kama AZUMA lakini ni kubwa kuliko azuma, binafsi sikujua ni dawa gani ila niliowakuta pale wanasema ni dawa za kufubaza virus vya VVU, na kuna mmoja anasema ndio maana yule mama na kustuliwa kote kule hakugeuka akaendelea kuondoka

Pale ndio nilopojisemea wagonjwa wa ukimwi kwenye jamii yetu bado wananyanyapaliwa ni vile tu hawaugui kama mwanzo kutokana na kuwepo kwa ARVs lakini pia wanaogopeka balaa.
 
.
 
Attachments

  • downloadfile-20.jpg
    downloadfile-20.jpg
    70.4 KB · Views: 22
Pale ndio nilopojisemea wagonjwa wa ukimwi kwenye jamii yetu bado wananyanyapaliwa ni vile tu hawaugui kama mwanzo kutokana na kuwepo kwa ARVs lakini pia wanaogopeka balaa.
Sasa hapo mkuu huyo mgonjwa amenyanyapaliwa kivipi? watu wamemshtua kua ameangusha dawa zake ila yeye mwenyewe akakausha,

Je na wewe unahusika na wale wote waliomyanyapaa? kama hauhusiki,ulichukua hatua gani ili na wewe usionekane kua umemyanyapaa?
 
Nimetafuta sehemu huyo mwanamama aliponyanyapaliwa kwenye maelezo ya uzi nimeikosa wallah!
 
Jana katika tembea tembea zangu nikakutana na mmama anatembea kwa miguu, tukiwa umbali wa kilometer kama 100 hivi yule mmama alidondosha kitu akaacha kukiokota akawa anaendelea kutembea, kwa mbali naona ishara za watu wakistua nimstue yule mama arudie kitu alichodondosha nami sikuelewa tukapishana kila mtu na zake

Kusogea mbele nakuta kumbe alidondosha dawa ni nyingi sana yaani zimetapakaa njia nzima na nikubwa kiasi, zimekaa kama AZUMA lakini ni kubwa kuliko azuma, binafsi sikujua ni dawa gani ila niliowakuta pale wanasema ni dawa za kufubaza virus vya VVU, na kuna mmoja anasema ndio maana yule mama na kustuliwa kote kule hakugeuka akaendelea kuondoka

Pale ndio nilopojisemea wagonjwa wa ukimwi kwenye jamii yetu bado wananyanyapaliwa ni vile tu hawaugui kama mwanzo kutokana na kuwepo kwa ARVs lakini pia wanaogopeka balaa.
tukiwa umbali wa kilometer kama 100 hivi 🥺🥺🥺 Far Chalinze hiyo ujue
 
Wanafiki tu hao watembea kwa miguu wenzako.Ikiingia giza tu wanagegedana kuliko simbilisi tena bila tahadhari muhimu.
NB:Ulieleza mlitembea kama kilometa 100? Okay! Nadhani itakuwa ni moja kati ya mistake au error.
 
Sorry nime edit ni just meter sio km makosa ya keyboad
 
Sasa hapo mkuu huyo mgonjwa amenyanyapaliwa kivipi? watu wamemshtua kua ameangusha dawa zake ila yeye mwenyewe akakausha,

Je na wewe unahusika na wale wote waliomyanyapaa? kama hauhusiki,ulichukua hatua gani ili na wewe usionekane kua umemyanyapaa?
Watu waliokuwa wanajua zile dawa ni za nini wengi wao walikuwa wanacheka kwa kebehi na walikusanyika wengi sana kiasi kwamba yule mtu angerudi kuzichukua angejihisi vibaya sana ni bora alivyoondoka

Lakini pia kutokana na mshangao ule na vicheko ulisababisha yule mama hajarudia dawa zake na kama ndio anatoka kuchukua dozi na yeye ndio mhusika huko aendako ataenda meza nini na dawa kadondosha just think of it
 
Back
Top Bottom