Huu ugonjwa bado unaogopeka na wagonjwa bado wananyanyapaliwa

Huu ugonjwa bado unaogopeka na wagonjwa bado wananyanyapaliwa

Kuna wengine si wastaarabu wa kutunza siri zao za ugonjwa. Ile mikebe ya dawa na karatasi zake za maelezo ya dawa hutupwa hovyo mitaani huku baadhi ya mikebe ikiwa na dawa mbili tatu zilizobaki baada ya mgonjwa kwenda kuchukua dawa zingine. Karatasi zinapepea unashindwa kujua imetokea kwenye nyumba ipi ili ujue kuna mgonjwa pale
 
Jana katika tembea tembea zangu nikakutana na mmama anatembea kwa miguu, tukiwa umbali wa meter kama 100 hivi yule mmama alidondosha kitu akaacha kukiokota akawa anaendelea kutembea, kwa mbali naona ishara za watu wakistua nimstue yule mama arudie kitu alichodondosha nami sikuelewa tukapishana kila mtu na zake

Kusogea mbele nakuta kumbe alidondosha dawa ni nyingi sana yaani zimetapakaa njia nzima na nikubwa kiasi, zimekaa kama AZUMA lakini ni kubwa kuliko azuma, binafsi sikujua ni dawa gani ila niliowakuta pale wanasema ni dawa za kufubaza virus vya VVU, na kuna mmoja anasema ndio maana yule mama na kustuliwa kote kule hakugeuka akaendelea kuondoka

Pale ndio nilopojisemea wagonjwa wa ukimwi kwenye jamii yetu bado wananyanyapaliwa ni vile tu hawaugui kama mwanzo kutokana na kuwepo kwa ARVs lakini pia wanaogopeka balaa.
Hisia tu za mwenye vidonge, siku hizi unyanyapaa kwa kiwango kikubwa umepungua sana watu wana elimu ya huo ugonjwaz kunyaanyapaliwa kwao kunakuja kwenye kujamiiana watu wanakuwa wanaogopa
 
Sasa hivi kuna magonjwa yanawapata watu ni ya kuhofia kuliko HIV.

Mwenye cancer/figo na mwenye HIV yupi mwenye hafadhari?
 
Ila wagonjwa wamenona aisee, wengine wanatongoza wakapigwe shoo/wapeleke moto. Kama hujui mwenye moto utaunguzwa kizembe bila kinga
 
Sasa hivi kuna magonjwa yanawapata watu ni ya kuhofia kuliko HIV.

Mwenye cancer/figo na mwenye HIV yupi mwenye hafadhari?
Kinachowafanya watu kuhofia HIV ni ugonjwa ambao una ambukiza,tofauti na Figo au Cancer,
Cancer/Kidney are not transmitted disease.
 
Back
Top Bottom