Huu umaskini ni wa kutisha

Huu umaskini ni wa kutisha

Ujio wa Magufuli kwenye uongozi wa Tanzania umeleta umasikini wa kutisha halafu Watu wanaoneshwa Madaraja.

N.a. ndio haohao juzi na jana walikuwa wanalia ilhali wananjaa.
Lisu si anakuwekea pesa mfukoni bana
 
Na bado wanaendelea kufyatua
Watu wanaoishi hivyo nchi hii ni wengiii mnooo. Kumbe hujaona mengi, siku moja pita hata Kariakoo saa 8 usiku ujionee, watu wanalala kwenye mabox ya kukodi pembeni kwenye maduka ya watu kwa gharama ya Tsh 400.

Pita pita Dar usiku ujionee watu wanaolala barabarani.

Nchi hii ni ina hohe hahe wa kiwango cha kutishaaaa.
 
Kuna watu wana dharau utadhani wao wana maisha mazuri sana, aliyempa yeye ni Mungu na aliemnyima mwingine ni Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes. Tunajisahau sana. Life is a Mystery. Kama umewahi kupitia shida na Mambo yakawa mazuri baadae .... Huwezi kuja kuandika huu Utumbo alioandika huyu mwanzisha Uzi.
 
Habari za mchana ndugu zangu,

Kuna dada mmoja alikuja home kutafuta chumba cha kupanga tukamuonesha chumba kimoja akakisafisha kesho yake akaja na mumewe kumuonesha.

Mume akadai chumba hajakipenda wakaondoka baada ya week akarudi tena, kile chumba kikawa kimepata mteja tukamuonesha chumba kingine.

Akasafisha akahamia jioni, jambo lililonifikirisha ni umaskini alionao huyu mama. Imagine ana watoto wanne hana kitanda wala gogoro yani yeye pamoja na mumewe na watoto wanalalia mkeka hata stuli moja tu hamna, ni nguo na vyombo vya ndani tu.

Najiuliza mumewe alikua na jeuri gani ya kukataa chumba kile wakati yeye hana kitu ndani.

Dunia ina maajabu hii, mume mlevi wa kutupwa dah poleni kina mama.
Huenda walikotoka wanadaiwa kodi wameacha vyombo
 
Inasikitisha sana
maisha ukipata kidogo usikufuru Kuna wasionacho kabisa
 
Kwa nini watu wanazaa watoto wengi hivyo wakati wanajua hawawezi kuwatunza??
Hiyo familia imepitia mikononi mwako ili uweze kuwasaidia kwa kadiri ya uwezo wako na sio kuja huku mitandaoni na kuwakashifu na kuwakejeli.
 
Sasa wengine ndio Kama hao... Wanakuja kutujazia nyuzi humu za kejeli. Badala ya kutoa msaada hata kidogo kwa kadiri ya alivyojaliwa. Watu tunajisahau Sana. Tunafikiri hivi tulivyonavyo Ni kwa ujanja na akili zetu .... Ni Kudra za Mwenyezi Mungu. Maisha huwa yanageuka wakati mwingine huwezi kuamuni.

Tenda Wema ... Malipo Ni Hapa Hapa Duniani.
Utajiri ni mtego!
Ukiona umepewa uwezo wa kifedha ujue hizo sio zako bali za wakosaji. Ila wengi hupuuzia hili makusudi tu. Imagine mtu una miaka 80 unafisadi pesa ambazo zingesaidia watoto wasioijiweza.

Sometimes I think we don't deserve this world kwakweli...Tumeumbwa tusaidiane na kula kwa kugawana kidogo tupatacho ila sasa tunavyoishi heri wanyama.

".........Tunatoka wapi tunakwenda wapi, Ona tulivyomgeuka muumba wetu! hatukumbuki Mungu ametuumba kwa makusidi gani"😢
 
Kwa nini uzae watoto ambao huwezi kuwahudumia??
Kuna eneo nilikua naangalia wanafunzi wa shule ndio nikaona dhiki kuu inayotukabili watanzania. Mtu hata sabubni ya 100/= hawezi mudu.

Afu kuna mtu anajaza mabilioni benki sijui hua wanamuwekea nani.
The worst part ni kua wenye kujali maimivu ya wenzao hawana uwezo...Wenye uwezo hawajali kabisa[emoji22]
 
Yes. Tunajisahau sana. Life is a Mystery. Kama unewahi kupitia shida na Mambo yakawa mazuri baadae .... Huwezi kuja kuandika huu Utumbo alioandika huyu mwanzisha Uzi.
Umri pia unaweza kuta alioleta huu uzi ni kachalii tu, mtu mwenye akili zake timamu na utu uzima asingeweza kufanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama umesema uyo mme wake nimlevi utajuaje pangine alivyo kuja mara ya kwanza alikua amelewa[emoji848]..?
 
Kwa nini watu wanazaa watoto wengi hivyo wakati wanajua hawawezi kuwatunza??
Umejuaje kama hali imembadilikia tayari alikua na watoto na mke ? ukishakua mwanaume unaweza ukaparangana tu,, hata huyo mwanamke mnaomsema anamvumili huyo baba huenda wakati mzee yupo vizuri aliwahudumia vizuri sana, msijaji vitu msivyovijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za mchana ndugu zangu,

Kuna dada mmoja alikuja home kutafuta chumba cha kupanga tukamuonesha chumba kimoja akakisafisha kesho yake akaja na mumewe kumuonesha.

Mume akadai chumba hajakipenda wakaondoka baada ya week akarudi tena, kile chumba kikawa kimepata mteja tukamuonesha chumba kingine.

Akasafisha akahamia jioni, jambo lililonifikirisha ni umaskini alionao huyu mama. Imagine ana watoto wanne hana kitanda wala gogoro yani yeye pamoja na mumewe na watoto wanalalia mkeka hata stuli moja tu hamna, ni nguo na vyombo vya ndani tu.

Najiuliza mumewe alikua na jeuri gani ya kukataa chumba kile wakati yeye hana kitu ndani.

Dunia ina maajabu hii, mume mlevi wa kutupwa dah poleni kina mama.
Unatakiwa kumpa pole mwanaume mwenzako. Huyo mama ndo anaiendesha familia...wanawake oyee

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Tajiri na mali zake masikini na watoto wake.
 
Back
Top Bottom