Huu umati anao ukusanya mwamposa ata wakiungana wasanii wa TZ nzima hawawezi, Unabii unalipa !!

Huu umati anao ukusanya mwamposa ata wakiungana wasanii wa TZ nzima hawawezi, Unabii unalipa !!

Serikali ya CCM wanapoona haya wanatakiwa kuina aibu maana wingi wa watu eneo hilo inaonyesha ni kiasi Gani Maisha yamekuwa magumu kwao watu wanategemea miujiza kutatua shida zao kuliko uhalisia.
Mkuu serikali ione aibu tena wakati wao ndio wanafurahia wakiona hivyo, unadhani serikali haijui kama hawa manabii ni wa uongo, inajua sana lakini kamwe haiwezi kuwapiga marufuku

Sababu kwanza wanakula nao, halafu pili hao manabii wanasaidia kuyafunika madhaifu ya serikali kwenye uchumi na huduma mbovu za kijamii, hao manabii wakipigwa marufuku maana yake watu wote wataigeukia serikali na kuipa pressure

Watataka iboreshe uchumi hasa ajira na biashara na huduma za kijamii, ambavyo wengi walitegemea kuvipata kupitia miujiza huko kwa manabii kwahiyo serikali haiko tayari kwa hilo, we jiulize kwanini nchi zilizoendelea watu wengi hawadanganyiki na haya mambo ya miujiza ya manabii sijui nini
 
Inaonyesha ni jinsi gani maisha ya watu yana changamoto hence kutafuta their Opium....

"Religion is the sigh of the oppressed creature, the heart of a heartless world, and the soul of soulless conditions. It is the opium of the people."
 
Unataka kusema ule umati wa kusoma quran pale uwanja wa mpira ni mdogo kwa huu wa kawe kwa mwamposa?
 
Umelinganisha vibaya, hilo ni kusanyiko la wenye shida, wasanii ni kusanyiko la wenye raha
 
Tofauti kati ya Shetani na Mungu ni ndogo sana mkuu!
Yawezekana mkuu na ndo maana wasanii wakubwa (Mtoe MJ)wanaweza kuwa hata kumi kwenye show moja na wasiwe na watu wengi lakini huyu anayeaminika kuwa ni mtumishi wa Mungu mmoja pekeyake kwenye show yake moja akajaza watu namna hii
 
Back
Top Bottom