Uzembe, wizi, ufisadi, huko bandarini, kama ilivyo kwenye Serikali nzima na taasisi zake, hakuna anayepinga wala kukataa. Lakini tusitafute suluhisho linalotupeleka kwenye matatizo makubwa zaidi kupitia ufisadi mkubwa unaofanywa na watawala wetu kupitia mikataba.
Kama dhamira ni njema, kwa nini tusiingie kwenye JV kwa kupitia mkataba mzuri bila ya kupoteza sovereignity yetu? Kama hatuna watu wenye akili na uwezo huko Serikalini kwenye masuala ya mikataba kwa nini hata tusi-copy na ku-paste e.g.mkataba wa Uingereza na DPW? Kwa nini tunaruka majivu na kukanyaga moto?
Uchafu uliopo bandarini na taasisi nyingine za Serikali ni picha halisi ya Serikali nzima ilivyo. Je, tuwape DPW waendeshe na serikali yetu kwa sababu imejaa mafisadi, majizi, wala rushwa, wazembe na walaghai? Polisi na mahakama, kupitia reports za kila mwaka, ni taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Je tuwape DPW wasimamie polisi na mahakama zetu?
Kushamiri kwa rushwa, wizi, uzembe na ufisadi ndani ya Serikali na taasisi zake, kama bandari, ndiyo ushahidi halisia kuwa Serikali imefeli kabisa, kwa sababu hizo taasisi zote, msimamizi mkuu ni Serikali. Na inafeli kwa sababu na yenyewe ni sehemu ya huo uchafu.