Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Mkuu Bandari kuna uozo sana unless huna habari watu wanavyojizolea mahela na kujenga nyumba na kuishi maisha ya kifahari. Bandari kuna uzembe ambao unakimbiza meli zinaacha kuja kwetu na kwenda Beira na Mombasa.

Wazawa tunaona kama vile Bandari inauzwa lakini hatuko serious kwenye management.

Hata kama mkataba una matatizo, ngoja tumepata mahali pa kuanzia, matatizo yatatatuliwa baadaye. Hakuna Mkataba ambao hauwi REVIEWED wala ambao hauna mwisho.

Nilikuwa mfanyakazi wa TBL hadi mwaka 1997 wakati SAB imenunua TBL mwaka 1993. Na sisi tulipinga sana TBL isiuzwe kwa kuwa tutakosa kazi. Leo hii ni miaka 30 SAB imekuwa acquired na InBev ya USA, je kuna mtu yeyote ana doubt mapato ya TBL? Au ajira ambazo zimetegengenezwa?

Kuna mtu ana doubt na product za TBL au gawio na kodi ambayo TBL inaleta?

Je umewahi kumsikia Mtanzania yeyote akitaka TBL iwe mali ya umma tena?
Bandari kuna uozo? TPA ilipewa tuzo ya ufanisi miezi kadhaa imepita
Uzembe bandari unadanya meli zinaenda beira au mombasa? Kwa takwimu za serikali kwa miaka mitatu ya mama mizigo imeongezeka sana na mapato yameongezeka sana. Hayo sio maneno yangu ni takwimu za serikali

Umetoa mfano wa TBL, pia utoe mfano wa mashirika mengi yaliyoanguka. Ukifanya tathmini kwenye 100%, mashirika 80% yalianguka baada ya kubinafsishwa
 
Bams tuombe uzima tu Mungu atuweke hata japo tufike 2030 then tuje turudi kwenye page hii. Naamini hutapenda kusoma maandiko yako haya.

Privatisation ndiyo engine ya growth, Serikali haziwezi kufanya biashara
Serikali haiwezi kufanya biashara una maana gan? Kwa sababu serikali hufanya sana biashara duniani kote, hao DP world wenyewe ni ya serikali
 
Nimekuwekea na link hapo au hujaiona?Kuna maswali waliuliza ila TEC hawakupewa majibu.

Kwani viwanda vingine vilivyo binafsishwa na leo yamebakwi magofu,Mwambukusi alilipwa kiasi gani? Tz klikuwa na viwanda vya nguo,Nyama,Matairi vilibinafsishwa je Lissu nae alipewa kiasi gani.

Labda kama umezaliwa juzi, ila kuna viwanda leo vimebaki kama majumba ya makumbusho na walio binafsishiwa wamekopea hela na kwenda kufanya biashara nyingine na wanadunda mtaani.

Halafu si kila anayepinga ni mpinzani au ana mlengo fulani wa siasa,kuna wengine wanataka kesho bora kwa vizazi vinavyo kuja.
Kwanza mimi ni mstaafu. Ubinasishaji ulinikuta TBL, nami nilipinga kama wewe. Ila kwa vile ninafahamu TBL niliyofanya mimi na TBL ya sasa huniambii lolote kuhusu ubinafsishaji.

Pili usilazimishe kila kiwanda kilichobinfsishwa kiwepo mpaka leo. Vingine bidhaa zake zimepitwa na wakati au teknoloji imebadilika.

Kwa mfano ungweza kuiganya Bora Shoe iendelee kuzalisha viatu leo? Je ingeweza kumudu na kupambana na ubora wa viatu vya mtumba vinavyoingia nchini?
 
Juu ulijenga hoja nzuri hapa umepuyanga
Teknolojia inapokuja mpya basi na kiwanda au taasisi huendana nao, kushindwa kufanya hivyo ni kufeli kwa management. Hata hiyo TBL teknolojia waliyotumia miaka ya 90 sio wanayotumia sasa
 
Nyama imepitwa na wakati, nguo zimepita na wakati? Kweli............ matairi yamepitwa na wakati...... Unaposema teknolojia imepitwa na wakati, wakati walipo binafsishwa moja ya target ya hao wawekezaji ni kuboresha uzalishaji kwa kutumia tech za kisasa.

Labda bora ungeniambia Software ningekuwa elewa, ila hamna kilicho pitwa na wakati bali umakini haukuwepo wakati wa ubinafsishaji. Industry ambayo inayo badilika sana ni IT Industry. Ila sio hivyo viwanda tulivyokuwa navyo.
 
Serikali haiwezi kufanya biashara una maana gan? Kwa sababu serikali hufanya sana biashara duniani kote, hao DP world wenyewe ni ya serikali
Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira ya bora biashara, kutengeneza sera za biashara, kukusanya kodi, na kufanya usimamizi (regulatory).

Biashara ziachiwe sekta binafsi ila kwenye maeno nyeti Serikali iwe na hisa, period.

Sasa kwa mfano Magufuli akaileta SUMA ikaanza kufanya kazi za mabaa na kumbi za harusi, clearing and forwarding. NONSENSE
 
Juu ulijenga hoja nzuri hapa umepuyanga
Teknolojia inapokuja mpya basi na kiwanda au taasisi huendana nao, kushindwa kufanya hivyo ni kufeli kwa management. Hata hiyo TBL teknolojia waliyotumia miaka ya 90 sio wanayotumia sasa
Kwa vile huelewi na kuna vitu umekariri lakini dynamics za uchumi zinakataa
 
Kuanzia Canary Wharf mpaka Shard imenunuliwa na Qatar
Nusu ya majengo london wanamiliki wao leo

Na sisi hatuna hiyana nao huwezi sikia mtu analalamika

Ardhi wamechukua sana
Kuna sehemu naijua West Sussex mwarabu wa Saudia kabeba eka 500 na hakuna chochote anachofanya
Anaweza akawa amesahau kama alilinunua eneo hilo
Lina miti tu hata jengo hakuna

Maadamu wanalipa kodi sawa tu
Sisi halmashauri wakikupa kusimamia Choo cha stand kukusanya 200 unapitia zote itakuwa msimamie bandari
Una wasiwasi mtanzania kuendelea kusimamia bandari, but huna wasiwasi mtanzania kuendelea kusimamia TRA, BOT?
Hiko kinakokusanywa huko na hao unaosema ni wawekezaji jua kuwa kinaenda kupelekwa kwa huyo huyo mtanzania ambae ww humuamini. Unakua umefanya nn sasa?
 
Kwa vile huelewi na kuna vitu umekariri lakini dynamics za uchumi zinakataa
Naelewa vizuri, usikimbie kwa jibu la jumla. Teknolojia inapokuja mpya taasisi yoyote makini huendana nayo, ukishindwa kuendana nayo ni kufeli kwa management na kufeli kwa huyo mwekezaji mpya. Nimetoa mfano wako wa tbl hata hiyo teknolojia wanayotumia sasa sio waliyotumia hiyo miama ya 90, Kama kuna taasisi ilibinafsishwa ikashindwa kuendana na teknolojia mpya hapo tatizo ni kufeli kwa huyo mwekezaji
 
Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira ya bora biashara, kutengeneza sera za biashara, kukusanya kodi, na kufanya usimamizi (regulatory).

Biashara ziachiwe sekta binafsi ila kwenye maeno nyeti Serikali iwe na hisa, period.

Sasa kwa mfano Magufuli akaileta SUMA ikaanza kufanya kazi za mabaa na kumbi za harusi, clearing and forwarding. NONSENSE
Hili unaongea kwa unavyoona au vile unatamani au ndio inatakiwa kuwa hivyo? Sababu serikali zilizoendelea na hata hizi zetu zinazoendelea zinafanya biashara sana
Ni wapi serikali haifanyi biashara? Naomba unitajie list ya nchi za ulimwengu wa kwanza ambazo serikali haifanyi biashara
 
Upuuzi mtupu, tafuta kwanza elimu pana ya hiyo mikataba kabla ya kukosoa usichokifahamu.

Wewe inaonekana ni zero katika masuala ya mikataba.

Mimi nimeshiriki kuandaa mikataba mingi ya kibiashara ya kimataifa. Ninaelewa ninachokiongea.

Sina shaka nabishana na layman, asiyejua chochote. IGA ile ya kishenzi iliyoiingiza DPW, siyo ya kutafuta. Iliwekwa public, na ilichambuliwa kitaalam na Tanganyika Law Society. Na mahakama ikakiri IGA ipo kinyume na sheria za nchi na za kimataifa, lakini ikasema haiwezi kutengua maamuzi ya mhimili wa Bunge. Halafu wewe usiyetambua wala kujielewa, umebakia na uchawa utakaoumiza vizazi vijavyo.
 
Nyama imepitwa na wakati, nguo zimepita na wakati? Kweli............ matairi yamepitwa na wakati...... Unaposema teknolojia imepitwa na wakati, wakati walipo binafsishwa moja ya target ya hao wawekezaji ni kuboresha uzalishaji kwa kutumia tech za kisasa.

Labda bora ungeniambia Software ningekuwa elewa, ila hamna kilicho pitwa na wakati bali umakini haukuwepo wakati wa ubinafsishaji. Industry ambayo inayo badilika sana ni IT Industry. Ila sio hivyo viwanda tulivyokuwa navyo.
Unaamini kuwa Tanganyika Packers wangeweza kuuza nyama? You are wrong youngman. Kwanza tambua kuwa market ya products za Tanganyika Packers haikuwa Tanzania. Mmiliki wake ambaye alikuwa ni Lornho hakupendezwa na Azimio la Arusha ambapo Baba wa Taifa JKN alitaifisha viwanda na mali za wafanya biashara wageni.

Tanganyika Packers ilikuwa inauza biðhaa zake by 90% huko European Union hadi miaka ya mwazo mwa 1970. Baada ya kutoridhika na ubinafsishaji wakafanya sabotage kwa Tanganyika Packers. Walitengeneza picha zinazoonyesha kuwa ng'ombe wa Tanzania wana ugonjwa wa kimeta. Kwa hiyo wakazi alert nchi zote 12 za EU wakati huo kuwa "there's reported anthrax outbreak in Tanzania, you will be therefore importing the beef products from this country at your own peril".

Hapo ndipo ukawa mwisho wa Tanganyika Packers japo iliendelea kuzalisha kwa ajili ya soko la TPDF na kusindika maharage hadi katikati ya miaka ya 1990s.
 
Una wasiwasi mtanzania kuendelea kusimamia bandari, but huna wasiwasi mtanzania kuendelea kusimamia TRA, BOT?
Hiko kinakokusanywa huko na hao unaosema ni wawekezaji jua kuwa kinaenda kupelekwa kwa huyo huyo mtanzania ambae ww humuamini. Unakua umefanya nn sasa?
Mkuu wala sifurahii haya
Angalia kila leo wanaandika kufuru wanayofanya TRA baadhi yao wamekamatwa na b za kutosha

Wakichunguzwa wote na kufungwa naona hela nyingi zingepatikana
Ipo siku huenda tukajielewa na kusimamia kila kitu
 
Hizo za TRA, BOT, TCRA ni sekta nyeti huwezi ukabinafsisha. Shughuli zankupakua na kupakia mizigo any Tom and Jerry can do
 
Unaamini kuwa Tanganyika Packers wangeweza kuuza nyama? You are wrong youngman. Kwanza tambua kuwa market ya products za Tanganyika Packers haikuwa Tanzania. Mmiliki wake ambaye alikuwa ni Lornho hakupendezwa na Azimio la Arusha ambapo Baba wa Taifa JKN alitaifisha viwanda na mali za wafanya biashara wageni.

Tanganyika Packers ilikuwa inauza biðhaa zake by 90% huko European Union hadi miaka ya mwazo mwa 1970. Baada ya kutoridhika na ubinafsishaji wakafanya sabotage kwa Tanganyika Packers. Walitengeneza picha zinazoonyesha kuwa ng'ombe wa Tanzania wana ugonjwa wa kimeta. Kwa hiyo wakazi alert nchi zote 12 za EU wakati huo kuwa "there's reported anthrax outbreak in Tanzania, you will be therefore importing the beef products from this country at your own peril".

Hapo ndipo ukawa mwisho wa Tanganyika Packers japo iliendelea kuzalisha kwa ajili ya soko la TPDF na kusindika maharage hadi katikati ya miaka ya 1990s.
Vp kwa hivyo vingine vilivyo binafsishwa maana unabinafsisha kitu manake anaye kuja atakiimprove ktk nyanja zote za kiteknolojia. Sawa vip vingine.......

Sawa mfano waliopewa Vitalu uwindaji ww unavyo ona wata improve nini?
 
Mkuu wala sifurahii haya
Angalia kila leo wanaandika kufuru wanayofanya TRA baadhi yao wamekamatwa na b za kutosha

Wakichunguzwa wote na kufungwa naona hela nyingi zingepatikana
Ipo siku huenda tukajielewa na kusimamia kila kitu
Hujajibu swali langu, umeadvocate bandari kupewa mwekezaji sababu mtanzania akipewa hata stand tu ya kukusanya sh 200 anaiba. Lakini hao unaosema wanaweza na wapewe bandari like wanachokipata huko wanapeleka kwa hao hao watanzania ambao ww huwaamini, hapo unakua umefanya nini? Ndio maana nikakuuliza huwaamini watanzania kwenye bandari Ila unawaamini watanzania kwenye TRA na BOT?
Kama huko napo huwaamini basi hata huo uwekezaji unaoutaka hauna maana na hautaleta matokeo yoyote

Au lengo la kuwekeza ni nini? Kama ili tupate faida, hiyo hiyo faida inarudi kukusanywa na kupangiwa matumizi na huyo huyo mtanzania ambae bado ataiba na kufuja vilevile
 
Naelewa vizuri, usikimbie kwa jibu la jumla. Teknolojia inapokuja mpya taasisi yoyote makini huendana nayo, ukishindwa kuendana nayo ni kufeli kwa management na kufeli kwa huyo mwekezaji mpya. Nimetoa mfano wako wa tbl hata hiyo teknolojia wanayotumia sasa sio waliyotumia hiyo miama ya 90, Kama kuna taasisi ilibinafsishwa ikashindwa kuendana na teknolojia mpya hapo tatizo ni kufeli kwa huyo mwekezaji
Do you think Serikali ingeweza ku transform teknolojia ya TBL ? Kwa taarifa yako TBL ilikuwa mali ya East African Breweries (Wanao manage Kenya Breweries siku hizi wanaitwa Diageo). Nyerere alipotaifisha akakiweka chini ya NDC, halafu baadaye wakabadili sheria ikawa Kampuni inayojitegemea. Toka ibinafsishwe mwaka 1967, niliona ni mwaka 1990 ndipo walibadili packaging line.

Bureaucracy ya serikali kwenye decision making, procurement regulations na compliance kwenye financial management zinacheleweaha sana mashirika au viwanda ku cope na technology
 
Mkuu Bandari kuna uozo sana unless huna habari watu wanavyojizolea mahela na kujenga nyumba na kuishi maisha ya kifahari. Bandari kuna uzembe ambao unakimbiza meli zinaacha kuja kwetu na kwenda Beira na Mombasa.

Wazawa tunaona kama vile Bandari inauzwa lakini hatuko serious kwenye management.

Hata kama mkataba una matatizo, ngoja tumepata mahali pa kuanzia, matatizo yatatatuliwa baadaye. Hakuna Mkataba ambao hauwi REVIEWED wala ambao hauna mwisho.

Nilikuwa mfanyakazi wa TBL hadi mwaka 1997 wakati SAB imenunua TBL mwaka 1993. Na sisi tulipinga sana TBL isiuzwe kwa kuwa tutakosa kazi. Leo hii ni miaka 30 SAB imekuwa acquired na InBev ya USA, je kuna mtu yeyote ana doubt mapato ya TBL? Au ajira ambazo zimetegengenezwa?

Kuna mtu ana doubt na product za TBL au gawio na kodi ambayo TBL inaleta?

Je umewahi kumsikia Mtanzania yeyote akitaka TBL iwe mali ya umma tena?

Uzembe, wizi, ufisadi, huko bandarini, kama ilivyo kwenye Serikali nzima na taasisi zake, hakuna anayepinga wala kukataa. Lakini tusitafute suluhisho linalotupeleka kwenye matatizo makubwa zaidi kupitia ufisadi mkubwa unaofanywa na watawala wetu kupitia mikataba.

Kama dhamira ni njema, kwa nini tusiingie kwenye JV kwa kupitia mkataba mzuri bila ya kupoteza sovereignity yetu? Kama hatuna watu wenye akili na uwezo huko Serikalini kwenye masuala ya mikataba kwa nini hata tusi-copy na ku-paste e.g.mkataba wa Uingereza na DPW? Kwa nini tunaruka majivu na kukanyaga moto?

Uchafu uliopo bandarini na taasisi nyingine za Serikali ni picha halisi ya Serikali nzima ilivyo. Je, tuwape DPW waendeshe na serikali yetu kwa sababu imejaa mafisadi, majizi, wala rushwa, wazembe na walaghai? Polisi na mahakama, kupitia reports za kila mwaka, ni taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Je tuwape DPW wasimamie polisi na mahakama zetu?

Kushamiri kwa rushwa, wizi, uzembe na ufisadi ndani ya Serikali na taasisi zake, kama bandari, ndiyo ushahidi halisia kuwa Serikali imefeli kabisa, kwa sababu hizo taasisi zote, msimamizi mkuu ni Serikali. Na inafeli kwa sababu na yenyewe ni sehemu ya huo uchafu.
 
Hili unaongea kwa unavyoona au vile unatamani au ndio inatakiwa kuwa hivyo? Sababu serikali zilizoendelea na hata hizi zetu zinazoendelea zinafanya biashara sana
Ni wapi serikali haifanyi biashara? Naomba unitajie list ya nchi za ulimwengu wa kwanza ambazo serikali haifanyi biashara
Hilo chukua mwenyewe GOOGLE utakuta tu. Angalia hata USA wala hawamiliki American Airways au UK hawamiliki British Air kama majority shareholders.
 
Hizo za TRA, BOT, TCRA ni sekta nyeti huwezi ukabinafsisha. Shughuli zankupakua na kupakia mizigo any Tom and Jerry can do
Ni sekta nyeti lakini bado zi zinaendeshwa na watanzania ambao ww umesema hawawezi hawana ufanisi na wezi.

Au tunakubaliana kuwa huko TRA BOT hakuna wezi na wazembe?
 
Back
Top Bottom