Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.

Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?

1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?

2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?

3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?

Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.

Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafs
Watu wako busy na Mzee magoma
 
Ndugu mbona umepitwa na wakati? Yote hayo uliyandika siyo kweli. Mbona kuna mwekezaji toka India anaitwa Adani Group lachukua berth 8, 9, 10 & 11.

Halafu kuna ubaya gani DP WORLD akichukua eneo jingine kwa ajili ya kuleta ufanisi. Kwani wale watu wa Kurasini hadi Kilwa Road Police wafididiwa fedha na Serikali ikawapa eneo jingine wewe unaumia nini?

Hilo la kutokulipa kodi za nchi ni UWONGO, kajipange upya

Ndugu yangu rudi kwenye ufahamu.

Unaelewa maana ya mkataba?

Nikuoe Mfano:

Wewe na mimi tukisaini mkataba wa biashara kuwa, halafu kwenye mkataba, kukawa na kipengere mimi nikitaka ninaweza kukuondosha wewe kwenye nyumba yako, halafu nikaacha kukuondosha leo, haimaanishi kuwa sitakuondosha siku nyingine nikitaka, kwa sababu haki hiyo, kwa kadiri ya mkataba, ninayo. Mimi kama sina nia ya kukuondosha siku moja, uhakika ni kukiondoa hicho kipengere mara moja, lakini ukiona nimeng'ang'ania kisiondolewe, halafu nakuambia tu kuwa huoni mpaka leo sijakuondoa, kama una akili, lazima ujue kuna dhamira mbaya ipo, imewekwa kwenye akiba ya siku moja kuja kutumia hicho kipengere.

Jiulize jwa nini DPW hawataki kuondoa hivyo vipengere vibaya vinavyoitia nchi utmwani?
 
Akili za kilofa ni zile zinazoshindwa kuendeleza sekta mbalimbali na wanapojitokeza wawekezaji mahiri haraka sana zinakimbilia katika hoja za uzalendo na hiki cha kwetu!.

Mmoja wapo ya masharti ya kuendesha hiyo TPA hao DPW wameambiwa ni lazima wakuze uwezo wa wazawa wetu kwenye sekta nzima ya bandari.

Tunapiga makelele kuhusu uzalendo wa mali zetu lakini elimu za kisasa za kusimamia hizo mali hatuna na tumejawa na fikra za ufisadi, uzembe na uvivu.

Tubadilike kwanza, vinginevyo kwa vitendo tutaendelea kuonyesha ni kwanini serikali haikosei katika kutafuta wawekezaji.
 
Ndugu mbona umepitwa na wakati? Yote hayo uliyandika siyo kweli. Mbona kuna mwekezaji toka India anaitwa Adani Group lachukua berth 8, 9, 10 & 11.

Halafu kuna ubaya gani DP WORLD akichukua eneo jingine kwa ajili ya kuleta ufanisi. Kwani wale watu wa Kurasini hadi Kilwa Road Police wafididiwa fedha na Serikali ikawapa eneo jingine wewe unaumia nini?

Hilo la kutokulipa kodi za nchi ni UWONGO, kajipange upya

Ndugu yangu rudi kwenye ufahamu.

Unaelewa maana ya mkataba?

Nikuoe Mfano:

Wewe na mimi tukisaini mkataba wa biashara kuwa, halafu kwenye mkataba, kukawa na kipengere mimi nikitaka ninaweza kukuondosha wewe kwenye nyumba yako, halafu nikaacha kukuondosha leo, haimaanishi kuwa sitakuondosha siku nyingine nikitaka, kwa sababu haki hiyo, kwa kadiri ya mkataba, ninayo. Mimi kama sina nia ya kukuondosha siku moja, uhakika ni kukiondoa hicho kipengere mara moja, lakini ukiona nimeng'ang'ania kisiondolewe, halafu nakuambia tu kuwa huoni mpaka leo sijakuondoa, kama una akili, lazima ujue kuna dhamira mbaya ipo, imewekwa kwenye akiba ya siku moja kuja kutumia hicho kipengere.
 
Ndugu yangu rudi kwenye ufahamu.

Unaelewa maana ya mkataba?

Nikuoe Mfano:

Wewe na mimi tukisaini mkataba wa biashara kuwa, halafu kwenye mkataba, kukawa na kipengere mimi nikitaka ninaweza kukuondosha wewe kwenye nyumba yako, halafu nikaacha kukuondosha leo, haimaanishi kuwa sitakuondosha siku nyingine nikitaka, kwa sababu haki hiyo, kwa kadiri ya mkataba, ninayo. Mimi kama sina nia ya kukuondosha siku moja, uhakika ni kukiondoa hicho kipengere mara moja, lakini ukiona nimeng'ang'ania kisiondolewe, halafu nakuambia tu kuwa huoni mpaka leo sijakuondoa, kama una akili, lazima ujue kuna dhamira mbaya ipo, imewekwa kwenye akiba ya siku moja kuja kutumia hicho kipengere.
Upuuzi mtupu, tafuta kwanza elimu pana ya hiyo mikataba kabla ya kukosoa usichokifahamu.
 
Ndugu yangu rudi kwenye ufahamu.

Unaelewa maana ya mkataba?

Nikuoe Mfano:

Wewe na mimi tukisaini mkataba wa biashara kuwa, halafu kwenye mkataba, kukawa na kipengere mimi nikitaka ninaweza kukuondosha wewe kwenye nyumba yako, halafu nikaacha kukuondosha leo, haimaanishi kuwa sitakuondosha siku nyingine nikitaka, kwa sababu haki hiyo, kwa kadiri ya mkataba, ninayo. Mimi kama sina nia ya kukuondosha siku moja, uhakika ni kukiondoa hicho kipengere mara moja, lakini ukiona nimeng'ang'ania kisiondolewe, halafu nakuambia tu kuwa huoni mpaka leo sijakuondoa, kama una akili, lazima ujue kuna dhamira mbaya ipo, imewekwa kwenye akiba ya siku moja kuja kutumia hicho kipengere.

Jiulize jwa nini DPW hawataki kuondoa hivyo vipengere vibaya vinavyoitia nchi utmwani?
Mkuu Bandari kuna uozo sana unless huna habari watu wanavyojizolea mahela na kujenga nyumba na kuishi maisha ya kifahari. Bandari kuna uzembe ambao unakimbiza meli zinaacha kuja kwetu na kwenda Beira na Mombasa.

Wazawa tunaona kama vile Bandari inauzwa lakini hatuko serious kwenye management.

Hata kama mkataba una matatizo, ngoja tumepata mahali pa kuanzia, matatizo yatatatuliwa baadaye. Hakuna Mkataba ambao hauwi REVIEWED wala ambao hauna mwisho.

Nilikuwa mfanyakazi wa TBL hadi mwaka 1997 wakati SAB imenunua TBL mwaka 1993. Na sisi tulipinga sana TBL isiuzwe kwa kuwa tutakosa kazi. Leo hii ni miaka 30 SAB imekuwa acquired na InBev ya USA, je kuna mtu yeyote ana doubt mapato ya TBL? Au ajira ambazo zimetegengenezwa?

Kuna mtu ana doubt na product za TBL au gawio na kodi ambayo TBL inaleta?

Je umewahi kumsikia Mtanzania yeyote akitaka TBL iwe mali ya umma tena?
 
Ndugu yangu rudi kwenye ufahamu.

Unaelewa maana ya mkataba?

Nikuoe Mfano:

Wewe na mimi tukisaini mkataba wa biashara kuwa, halafu kwenye mkataba, kukawa na kipengere mimi nikitaka ninaweza kukuondosha wewe kwenye nyumba yako, halafu nikaacha kukuondosha leo, haimaanishi kuwa sitakuondosha siku nyingine nikitaka, kwa sababu haki hiyo, kwa kadiri ya mkataba, ninayo. Mimi kama sina nia ya kukuondosha siku moja, uhakika ni kukiondoa hicho kipengere mara moja, lakini ukiona nimeng'ang'ania kisiondolewe, halafu nakuambia tu kuwa huoni mpaka leo sijakuondoa, kama una akili, lazima ujue kuna dhamira mbaya ipo, imewekwa kwenye akiba ya siku moja kuja kutumia hicho kipengere.
Bams tuombe uzima tu Mungu atuweke hata japo tufike 2030 then tuje turudi kwenye page hii. Naamini hutapenda kusoma maandiko yako haya.

Privatisation ndiyo engine ya growth, Serikali haziwezi kufanya biashara
 
Kuanzia Canary Wharf mpaka Shard imenunuliwa na Qatar
Nusu ya majengo london wanamiliki wao leo

Na sisi hatuna hiyana nao huwezi sikia mtu analalamika

Ardhi wamechukua sana
Kuna sehemu naijua West Sussex mwarabu wa Saudia kabeba eka 500 na hakuna chochote anachofanya
Anaweza akawa amesahau kama alilinunua eneo hilo
Lina miti tu hata jengo hakuna

Maadamu wanalipa kodi sawa tu
Sisi halmashauri wakikupa kusimamia Choo cha stand kukusanya 200 unapitia zote itakuwa msimamie bandari
Uongo tu, heka 500 mzungu akupe kifala na ukae nazoo tu, shabash blood fakeni. thanks
 
Uongo tu, heka 500 mzungu akupe kifala na ukae nazoo tu, shabash blood fakeni.
Umeona ubishe tu kwa kutokuelewa au kujitoa ufahamu
Unatukana kwa ujinga wako
Kwa kuwa huna ufahamu na dunia hii
Acha nikutoe ushamba kidogo dogo kuwa ardhi ipo chini ya King lakini inaweza kukodishwa
Mwarabu wa Dubai kama unajua kizungu msome hapa
Hata mimi naweza kumiliki kama nina hela acha ujuaji wa kijinga
Nidanganye ili iweje?
Ngoje wenye akili wqje
Screenshot_20240718_065800_Google~2.png
 
Umeona ubishe tu kwa kutokuelewa au kujitoa ufahamu
Unatukana kwa ujinga wako
Kwa kuwa huna ufahamu na dunia hii
Acha nikutoe ushamba kidogo dogo kuwa ardhi ipo chini ya King lakini inaweza kukodishwa
Mwarabu wa Dubai kama unajua kizungu msome hapa
Hata mimi naweza kumiliki kama nina hela acha ujuaji wa kijinga
Nidanganye ili iweje?
Ngoje wenye akili wqjeView attachment 3045226
Achana na huyu bwege Chatta g yuko huko sweken Nangurukuru anataka kubishana na watu walio mbele. Wana very poor arguments kwa kuwa hawana exposure
 
Huwa sipendi kubishana na wapumbavu kama hao
Ambao Google wanatumia kuangalia ngono tu na tiktok
Kweli unamshambulia mtu bila kuwa na uhakika
What a cunt he is
 
warabu wanamiliki London kwa sasa itakuja kuwa Tanzania. Muwekezaji ni mwenye hela na hela iko kwa warabu. Wewe unaongea airport ya KIA wakati warabu tayari wanamiliki % Heathrow.
Mkataba walio ingia London ndio ulio uingia wewe? Ukitaka kujua kalitizame bunge la UK hata kwa wiki moja uone mijadala ya nchi yao inavyo endeshwa,uone jinsi walivyo kuwa na projection ya vizazi vyao miaka mia ijayo, uone watu wanavyo bishana kwa hoja bila kutishwa wala kukatizwa katizwa.

Hamna mtu anaye kataa uwekezaji bali watu wanacho kataa ni mikataba ya hovyo tunayo ingia kwani watakao umia ni vizazi vijavyo, ukifanya masihala Tembo watakuwa wanawatizama kwenye Zoo.
 
Tuna mazingira tofauti, mtaba wa Tanzania hauwezi kuwa sawa na wa UK. Pili tambua kuwa hata mkataba huwa REVIWED anytime kama moja ya pande haiko contented na performance. Ila nikikuuliza ni kipengele gani cha mkataba ni kibaya huwezi kutaja zaidi ya kukariri maneno ya akina Mwabukusi na Lissu
 
Mazingira ni tofauti, ila maslahi ni the same japo approach inaweza kuwa tofauti. Ila mikataba yote ni kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi.

Kuna maswali waliulizwa hila haya kujibiwa. Halafu kwani mashirika mengine yalivyo binafsishwa,wakina Mwabukusi na Lissu walikuwepo kwenye ulingo wa kisiasa.

Halafu Mwambukusi na Lissu ni raia na wana haki ya kutoa maoni na mtizamo wao,kwani hii ni nchi ya kidemokrasia.Ukiona watu wanaongea jua kuna vitu wameviona wanataka kama taifa tuviepuka,kwani yale mashirika mengine yaliyo binafsishwa leo hii yapo wapi?
 
Mwabukusi ni kwamba MWABUKUSI alipewa Tsh 400 Millioni na wenye masilahi na TICTS ili aipinge DP WORLD isiingie mkataba na Tanzania. Ndipo kajifanya mzalendo wa kutaka Tanganyika na Katiba Mpya.

Akaweza kuungana na Dr Slaa na Mdude_Nyagali ili kuipa presha Serikali.

Niliingia kwenye page yake ya Twitter nikaandika hii taarifa, akani BLOCK immediately
 
Nimekuwekea na link hapo au hujaiona?Kuna maswali waliuliza ila TEC hawakupewa majibu.

Kwani viwanda vingine vilivyo binafsishwa na leo yamebakwi magofu,Mwambukusi alilipwa kiasi gani? Tz klikuwa na viwanda vya nguo,Nyama,Matairi vilibinafsishwa je Lissu nae alipewa kiasi gani.

Labda kama umezaliwa juzi, ila kuna viwanda leo vimebaki kama majumba ya makumbusho na walio binafsishiwa wamekopea hela na kwenda kufanya biashara nyingine na wanadunda mtaani.

Halafu si kila anayepinga ni mpinzani au ana mlengo fulani wa siasa,kuna wengine wanataka kesho bora kwa vizazi vinavyo kuja.
 
Si unajua wapemba uzani na wao ni waarabu [emoji81][emoji81]kuna mmoja pale Top 1, aliwahi diriki kwenda kumsalimia babu yake wa ukoo kizaa nani nani sijui pale Oman ..

Tuna lipia fadhila kwa ardhi yetu kwa ujinga wa watu wachache
 
Magu ali kaza 6 years .kaja uyu sio mchoyo ajui kukataa kaachia zote in less than 3 years .
 
Back
Top Bottom