kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Asante sana ndugu kwa maoni haya. Yaani tuko masafa sawa sana kwa mtazamo. Na hakika kama ingekua sio yule mwananchi mzalendo aliyetuwekea mtandaoni ule mkataba na Dubai kuwapa bandari zetu zote waendeshe kama wamiliki tungeingizwa mkenge na hii serikali ya awamu ya sita. Vikaragosi ni pamoja na speaker wa bunge Tulia Ackison ambae kwa hila alihakikisha mkataba huo wa kihuni unapita bungeni fasta. Wananchi hatimae wakaukataa na kumlazimisha rais kutumia mbinu tofauti. Kinachoonekana baada ya raia kupiga kelele waarabu badala ya kupita mlangoni wameingizwa kupitia dirishani. Wananchi tumetaka mkeka wa mkataba na DPW uwekwe hadharani tuone nini ni makubaliano jambo ambalo serikali haitaki kufanya hadi sasa. Walisema DPW inapewa gati 2 tu ila tunasikia saa hizi wanasema gati namba moja hadi saba zote wanapewa. Umma wa tanzania kupitia serikali yao washawekeza mabilioni ya dola. Je mwekezaji huyo si yatakua yaleyalr ya TICTS ambao walivuna tu na hawakuwekeza hata senti moja.Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.
Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?
1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?
2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?
3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?
Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.
Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafsi.
Pia KIA ni ujambazi tu umefanyika kuleta kampuni ya Oman wakati kampuni ya serikali ikisimamia uwanja huo vizuri ila kuna vigogo wasiopenda serikali kuweza kitu kwa kusudi ili waweze kutoa kandarasi kwa wageni wavune ambapo hawakupanda kwa maslahi yao binafsi.
Wananchi wazalendo tugome . Kama serikali hii haiwezi kusimamia uwekezaji za umma na na kukimbilia kuwapa waarabu na wageni wengine kama vile nchi hii hakuna uwezo huku elimu ya chuo kikuu inatolewa miaka yote bora wachukue hatua mapema kujihami.