Huu umilikishwaji wa vitega uchumi muhimu vya nchi kwa waarabu, ni uwekezaji au uvunaji?

Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.

Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?

1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?

2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?

3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?

Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.

Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafsi.
Asante sana ndugu kwa maoni haya. Yaani tuko masafa sawa sana kwa mtazamo. Na hakika kama ingekua sio yule mwananchi mzalendo aliyetuwekea mtandaoni ule mkataba na Dubai kuwapa bandari zetu zote waendeshe kama wamiliki tungeingizwa mkenge na hii serikali ya awamu ya sita. Vikaragosi ni pamoja na speaker wa bunge Tulia Ackison ambae kwa hila alihakikisha mkataba huo wa kihuni unapita bungeni fasta. Wananchi hatimae wakaukataa na kumlazimisha rais kutumia mbinu tofauti. Kinachoonekana baada ya raia kupiga kelele waarabu badala ya kupita mlangoni wameingizwa kupitia dirishani. Wananchi tumetaka mkeka wa mkataba na DPW uwekwe hadharani tuone nini ni makubaliano jambo ambalo serikali haitaki kufanya hadi sasa. Walisema DPW inapewa gati 2 tu ila tunasikia saa hizi wanasema gati namba moja hadi saba zote wanapewa. Umma wa tanzania kupitia serikali yao washawekeza mabilioni ya dola. Je mwekezaji huyo si yatakua yaleyalr ya TICTS ambao walivuna tu na hawakuwekeza hata senti moja.
Pia KIA ni ujambazi tu umefanyika kuleta kampuni ya Oman wakati kampuni ya serikali ikisimamia uwanja huo vizuri ila kuna vigogo wasiopenda serikali kuweza kitu kwa kusudi ili waweze kutoa kandarasi kwa wageni wavune ambapo hawakupanda kwa maslahi yao binafsi.
Wananchi wazalendo tugome . Kama serikali hii haiwezi kusimamia uwekezaji za umma na na kukimbilia kuwapa waarabu na wageni wengine kama vile nchi hii hakuna uwezo huku elimu ya chuo kikuu inatolewa miaka yote bora wachukue hatua mapema kujihami.
 
Miaka iliyopita, tukisikia wawekezaji, tunajua ni watu wenye mitaji na tekinolojia, wanakuja kujenga na kuendesha miradi yao waliyoijenga wenyewe.

Lakini, kwa sasa, ghafla maana ya uwekezaji imebadilika. Hao wawekezaji wa sasa, wanakuja wanachukua rasilimali za nchi ambazo tayari zimejengwa au kuendelezwa. Wanapewa, na kuanza kukusanya mapato. Hivi hawa ni wawekezaji au Wavunaji?

1) Marehemu Magufuli aliwakataa wawekezaji wa Kichina ambao wangejenga bandari mpya Bagamoyo, na ambayo wangeiendesha wenyewe. Tuliwakataa waliotaka kujenga bandari mpya. HALAFU? Kupitia mkataba wa IGA, mkataba wa hovyo kabisa kuwahi kutokea Duniani, DPW wakapewa bandari mama ya Dar es Salaam ambayo tayari nchi imekwishawekeza zaidi ya dola bilioni 10, na mwushoni kabisa, kwa mkupuo nchi imewekeza dola bilioni 1. DPW tunaambiwa eti atawekeza dola nusu billion. Katika hali ta kawaida, tujiulize, hivi sisi tuna utimamu wa akili? Unamkataa anayekuja kuwekeza mradi mpya, halafu unamkubalia mvunaji!! Huu ni uporaji wa kitegauchumi cha Taifa. Waliowezesha uporaji huu, wanalitakia nini Taifa hili?

2) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha, tayari ulikwishajengwa, tayari ulikuwa unafanya kazi, sasa amepewa mwarabu!! Hivi aliyepewa huo uwanja ni mwekezaji au mvunaji? Kama ni mwekezaji kwa nini hakupewa eneo akajenge uwanja wa kwake?

3) Kuna makampuni mengine toka Uarabuni yamepewa mbuga za wanyama na hifadhi za misitu. Hivi hawa ni wawekezaji au wavunaji/waporaji? Kama ni wawekezaji, wameleta pundamilia, twiga, fisi na ngiri wangapi kwenye hizo hifadhi? Au wamepanda mininga na mitundu mingapi kwenye hiyo misitu hadi waitwe wawekezaji?

Hivi tumefikia mahali pa kuwapa waarabu karibia kila rasilimali tulizozitolea jasho kwa miaka mingi, kwa lengo gani? Mtu yeyote ambaye hana uchumi ni mtu duni na automatically atakuwa mtumwa wa mwenye uchumi. Tunapowapa kila mlango wa uchumi waarabu, automatically tunatengeneza mazingira ya kuwafanya Watanganyika huko mbeleni kuwa watumwa wa waarabu ndani ya Taifa lao.

Jamani, tuwaache walio na tamaa za ajabu waendelee kushangilia na kufurahia hadaa wazifanyazo kwa Taifa, wao wakirushiwa hata dola laki 1, wapo tayari hata kuua matumaini ya vizazi vyote vijavyo, LAKINI walio na hekima ni lazima tuendelee kupaza sauti zetu na kusema kuwa huu uovu, kama umma wa watu wazalendo, tunasema HAPANA. Nchi inawahitaji wawekezaji wa ndani na nje, lakini wavunaji wa wa nje wa mazao ya uwekezaji wetu, tuseme, hapana. Tuongozwe na uzalendo na sio tamaa ya mapato binafsi.
Unaposema Mwarabu unaharibu mantiki ya mada yako. Je angekuwa ni Mzungu kutoka America au Europe ungeandika hiyo mada?

Munakosea mnapoleta ubaguzi kwenye biashara. Kwa hiyo ungeona Wazungu wemeshinda zabuni ungesikia raha?

Pesa ziko Uarabuni ndiyo maana hata Waingereza wenyewe wame surrender clubs zao za EPL kwa waarabu. Angalia Newcastle, Mancity, Arsenal etc.

Hata bandari ya Portsmouth pale Uingereza inaendeshwa na DP WORLD, wewe ni nani udharau Waarabu
 
Hapa mjinga ni wewe,ndiye uliyeonekana kuwa huwezi soma na kuelewa ulichosoma,mada inasema haikupaswa mwarabu apewe bandari Bali ajenge Kama ambavyo mchina angejenga bagamoyo,ndiyo nikaleta mifano ya hayo mashirika ya umma ambayo wazungu waliwekeza na bado wapo na Wala hampigi kelele,alikuwepo dowans, mwarabu,mkapiga kelele,akaja symbion kuwekeza palepale Kwa dowans,mkatulia,sijui mnafundishana nini huko kanisani!!
Uwezo wako wa kufikiri mdogo sana.
 
Unaposema Mwarabu unaharibu mantiki ya mada yako. Je angekuwa ni Mzungu kutoka America au Europe ungeandika hiyo mada?

Munakosea mnapoleta ubaguzi kwenye biashara. Kwa hiyo ungeona Wazungu wemeshinda zabuni ungesikia raha?

Pesa ziko Uarabuni ndiyo maana hata Waingereza wenyewe wame surrender clubs zao za EPL kwa waarabu. Angalia Newcastle, Mancity, Arsenal etc.

Hata bandari ya Portsmouth pale Uingereza inaendeshwa na DP WORLD, wewe ni nani udharau Waarabu
Usifikiri masharti ya DPW kwa waingereza ni sawa na yale wanatoa kwetu. Mbona kuna cases hao DPW licha ya kupata kandarasi kuendesha bandari mbili huko marekani hatimaye wakagomewa hawakupewa. Hapo djibuti kandarasi ilivyunjwa baada ya ushahidi walihonga. Kwanza naamini DPW ni kampuni ya kimataifa ya dubai. Hisa nyingi bila shaka za matajiri wa kiarabu. Kuna wanahisa kimataifa. Ni biashara ukizubaa wanakupiga hata kukunyang'anya chako.
 
Yaani kila mahali wanaiba haswa
Hata wapewe mishahara mikubwa kiasi gani bado wanaona hazitoshi
Wizi umeota mizizi na hakuna wa kuwaambia basi
Tukiendelea hivi tunakuja kuwarithisha watoto wetu na hao "wevi" kuwa watumwa nchi kwetu , Kwani tatizo likiota mizizi tuta feli kila kitu ndio hapo watu WA nje watakapo kuja kututawala na hivyo vitukuu nitakuwa havijui Maisha mengine zaidi ya kurithi vya wizi , watashindwa Mapambano.
Kuna clip moja jamaa anaizungumzia IMF na mikopo Kwa Kenya-Ya hii bajeti ya Euro, anasema IMF, wanapokukopesha haja Yao na masharti yao sio uwalipe, Bali kupata Mema ya Nchi yako. Matokeo yake Leo ukienda YouTube kuna clip za viongozi WA IMF kuwaomba Radhi wa Kenya.
Yeye anapigia chapuo mikopo toka china etc isiyo na masharti, ingawa nayo ya china kama viongozi wetu wakiweka chao juu, Naye Mchina atatula Kichwa. Cha misingi tujue tunatoka wapi , na tunaenda wapi.
 
Usifikiri masharti ya DPW kwa waingereza ni sawa na yale wanatoa kwetu. Mbona kuna cases hao DPW licha ya kupata kandarasi kuendesha bandari mbili huko marekani hatimaye wakagomewa hawakupewa. Hapo djibuti kandarasi ilivyunjwa baada ya ushahidi walihonga. Kwanza naamini DPW ni kampuni ya kimataifa ya dubai. Hisa nyingi bila shaka za matajiri wa kiarabu. Kuna wanahisa kimataifa. Ni biashara ukizubaa wanakupiga hata kukunyang'anya chako.
Kwanza kinachowekezwa bongo ni kile kile kilicho toka hapo hapo Bandari na sehemu nyingine humu humu nchi . Maana Kwa nchi za wezenzetu kwenye soko la mitaji , hawa wana hisa wanajulikana lakini huko Dubai, ni chaka la kuficha madudu ya watu.
 
Usifikiri masharti ya DPW kwa waingereza ni sawa na yale wanatoa kwetu. Mbona kuna cases hao DPW licha ya kupata kandarasi kuendesha bandari mbili huko marekani hatimaye wakagomewa hawakupewa. Hapo djibuti kandarasi ilivyunjwa baada ya ushahidi walihonga. Kwanza naamini DPW ni kampuni ya kimataifa ya dubai. Hisa nyingi bila shaka za matajiri wa kiarabu. Kuna wanahisa kimataifa. Ni biashara ukizubaa wanakupiga hata kukunyang'anya chako.
Mumekariri shortcomings za Djibouti tu na kukosa hiyo kandarasi ya USA. LAKINI hamusemi kuhusu hizo ports zingine ambazo zaidi ya 70 ambazo DP WORLD ana operate successfully all over the world. Very low argument from mediocre minds
 
Celtel, Zain, Airtel,crdb,nmb, TRL (TRC),ticts,atcl(ATC)...ukisoma hayo majina unapata chochote,au chuki kwa waarabu zimekujaa Hadi puani!?.
Binafsi Waarabu siwapendi kwanza hawana hela wao wenyewe Masikini tu pili wana roho mbaya mno hao jamaa bora Mzungu mara buku
 
Kuongoza wajinga ni kazi rahisi sana...
Kwao masuala ya Yanga au Simba au Euro ni muhimu zaidi kwao kuliko mienendo ya serikali, utu, haki na uhuru!
 
Mumekariri shortcomings za Djibouti tu na kukosa hiyo kandarasi ya USA. LAKINI hamusemi kuhusu hizo ports zingine ambazo zaidi ya 70 ambazo DP WORLD ana operate successfully all over the world. Very low argument from mediocre minds
Umeona mikataba ya hizo ports zaidi ya 70?
Nazo ziliandikwa kienyejically kama huu wa kwetu?
 
Binafsi Waarabu siwapendi kwanza hawana hela wao wenyewe Masikini tu pili wana roho mbaya mno hao jamaa bora Mzungu mara buku
Acha upumbavu wako. Uwekezaji siyo ukoloni. Mwenye fedha sasa hivi ni muarabu kutoka Qatar, UAE na Saudia. Mwingereza mwenyewe kashindwa kumzuia maana timu zake za Mancity, Newcastle, PSG (France) zinamilikiwa na Mwarabu
 
Umeona mikataba ya hizo ports zaidi ya 70?
Nazo ziliandikwa kienyejically kama huu wa kwetu?
Kwani mkataba wetu una shida gani? Au bado umekaririshwa maneno machafu ya Dr Slaa na Mwabukusi?
 
kazi zimewashinda, vijana wamebaki kubet, kulewa na ubishi wa simba na yanga. Wanakuja wanao jielewa na kuendeleza mashirika yalio washinda halafu mnakaa humu kubwabwaja kuhusuiana na dini na ukabila. Huu ni upumbavu mkubwa sana.
 
Tukiendelea hivi tunakuja kuwarithisha watoto wetu na hao "wevi" kuwa watumwa nchi kwetu , Kwani tatizo likiota mizizi tuta feli kila kitu ndio hapo watu WA nje watakapo kuja kututawala na hivyo vitukuu nitakuwa havijui Maisha mengine zaidi ya kurithi vya wizi , watashindwa Mapambano.
Kuna clip moja jamaa anaizungumzia IMF na mikopo Kwa Kenya-Ya hii bajeti ya Euro, anasema IMF, wanapokukopesha haja Yao na masharti yao sio uwalipe, Bali kupata Mema ya Nchi yako. Matokeo yake Leo ukienda YouTube kuna clip za viongozi WA IMF kuwaomba Radhi wa Kenya.
Yeye anapigia chapuo mikopo toka china etc isiyo na masharti, ingawa nayo ya china kama viongozi wetu wakiweka chao juu, Naye Mchina atatula Kichwa. Cha misingi tujue tunatoka wapi , na tunaenda wapi.
Mkuu
Wizi unaanzia mashuleni wanaiba kalamu na mwalimu hakuna wa kuliongelea kwani wao pia wamekulia wizi

Tabia inaanzia chini wanangu marufuku kuzurura na watoto wala kwenda makwao
Ukiwadhibiti na kuangalia mabegi yao na mienendo yao na pia kuwafundisha maadili basi utashinda

Na mchina ndio mwizi mkubwa ameishataifisha vitu vingi Afrika na anaenda kwenye mashamba sasa
 
kazi zimewashinda, vijana wamebaki kubet, kulewa na ubishi wa simba na yanga. Wanakuja wanao jielewa na kuendeleza mashirika yalio washinda halafu mnakaa humu kubwabwaja kuhusuiana na dini na ukabila. Huu ni upumbavu mkubwa sana.
Ni upumbavu sana Bro majebere ! Mwarabu anatumia mtaji ila management ameweka wazungu. Hata wanao manage Emirates Air au Qatar Air siyo waarabu bali ni wazungu tu.

Tunaona wenyewe kinachofanyika TRA japo hatuwezi kubinafsisha TRA. Vijana wadogo wana miaka 5 toka wame graduate lakini wana miliki maghorofa Goba, Mivumoni na Mabwepande
 
Mkuu
Wizi unaanzia mashuleni wanaiba kalamu na mwalimu hakuna wa kuliongelea kwani wao pia wamekulia wizi

Tabia inaanzia chini wanangu marufuku kuzurura na watoto wala kwenda makwao
Ukiwadhibiti na kuangalia mabegi yao na mienendo yao na pia kuwafundisha maadili basi utashinda

Na mchina ndio mwizi mkubwa ameishataifisha vitu vingi Afrika na anaenda kwenye mashamba sasa
Tatizo sio Mtoto wako au wangu, tatizo baada ya kutoka kwako na tabia njema , akienda kazini , anakutana na system Gani ? Iliyooza toka kichwani au iliyoanzia kwenye mkia. Kumbuka usemi wa moja akioza wote wameoza. Labda apate kazi shirika au mwajiri mwenye kujielewa. Na ndio maana licha ya vivutio vya uwekezaji, hakuna mwekezaji mahiri atakuja bongo, sababu ya mazingira yetu hayatoi fursa sawa. Bali fursa Kwa wevi
 
Toka tumeanzisha sera ya ubinafsishaji na hii kitu inaitwa uwekezaji, watu wetu wako busy kukuza mifuko na matumbo yao kuliko kuangalia maslahi mapana ya Taifa, Hali imeanza toka awamu ya pili mpaka Leo.

Hakuna uwekezaji Tanzania ambao umeweza kuleta faida kwa watanzania kuliko wawekezaji wenyewe na madalali wao, kuanzia kwenye madini, gani, nishati nk.
Tamaa binafsi na kukosa uzalendo vimetumiwa na wekezaji kuendelea kuwakoloni Watanzania katika ardhi yao na matokeo yake kuwaacha masikini ilihali wanarasilimari Kila mahala.

Watu wabadirike tu sasa na kuipenda zaidi nchi yao na watanzania wenzao.
hawatakuelewa hadi gt. waamke halafu tulaumiane.
 
Ni upumbavu sana Bro majebere ! Mwarabu anatumia mtaji ila management amweka wazungu. Hata wanao manage Emirates Air au Qatar Air siyo waarabu bali ni wazingu tu.

Tunaona wenyewe kinachofanyika TRA japo hatuwezi kubinafsisha TRA. Vijana wadogo wana miaka 5 toka wame graduate lakini wana miliki maghorofa Goba, Mivumoni na Mabwepande
system inaruhusu huo ujinga ndiyo maana unaendelea.
 
warabu wanamiliki London kwa sasa itakuja kuwa Tanzania. Muwekezaji ni mwenye hela na hela iko kwa warabu. Wewe unaongea airport ya KIA wakati warabu tayari wanamiliki % Heathrow.
Hiyo Heathrow walipewa bure kama sisi tunavyo gawa hizi za kwetu? Maana DPW mpaka sasa hajaweka hata shillingi moja ila amepewa bandari na anaanza kula hela bora wale wachina + Quatar waliokuwa wanakuja na hela zao kujenga Bagamoyo na viwanda vyake tungepata hata ajira sio hii ya DPW.
 
Back
Top Bottom