Baltazar Engongo
JF-Expert Member
- May 6, 2024
- 604
- 932
Bandari kuna uozo? TPA ilipewa tuzo ya ufanisi miezi kadhaa imepitaMkuu Bandari kuna uozo sana unless huna habari watu wanavyojizolea mahela na kujenga nyumba na kuishi maisha ya kifahari. Bandari kuna uzembe ambao unakimbiza meli zinaacha kuja kwetu na kwenda Beira na Mombasa.
Wazawa tunaona kama vile Bandari inauzwa lakini hatuko serious kwenye management.
Hata kama mkataba una matatizo, ngoja tumepata mahali pa kuanzia, matatizo yatatatuliwa baadaye. Hakuna Mkataba ambao hauwi REVIEWED wala ambao hauna mwisho.
Nilikuwa mfanyakazi wa TBL hadi mwaka 1997 wakati SAB imenunua TBL mwaka 1993. Na sisi tulipinga sana TBL isiuzwe kwa kuwa tutakosa kazi. Leo hii ni miaka 30 SAB imekuwa acquired na InBev ya USA, je kuna mtu yeyote ana doubt mapato ya TBL? Au ajira ambazo zimetegengenezwa?
Kuna mtu ana doubt na product za TBL au gawio na kodi ambayo TBL inaleta?
Je umewahi kumsikia Mtanzania yeyote akitaka TBL iwe mali ya umma tena?
Uzembe bandari unadanya meli zinaenda beira au mombasa? Kwa takwimu za serikali kwa miaka mitatu ya mama mizigo imeongezeka sana na mapato yameongezeka sana. Hayo sio maneno yangu ni takwimu za serikali
Umetoa mfano wa TBL, pia utoe mfano wa mashirika mengi yaliyoanguka. Ukifanya tathmini kwenye 100%, mashirika 80% yalianguka baada ya kubinafsishwa