Na haya ndyo maisha ninayaishi....
Najuta kuzaliwa kwenye hii Familia,lakini ni vitu ambavyo siwezi kuvibadilisha.
Siku za mwanzo nilikua najutia na kuumia sana....Kuna wakati nilitakiwa kukubali kua sikujipangia,yaani nimezaliwa na kujikuta humo hivyo siwezi kubdilisha chochote..........
Mimi ndugu Zangu hatuwasiliani,maybe Tukutane kwenye matatizo.
Hawa siyo ndugu wa mbali, Hawa ni ndugu Zangu wa damu,tumetoka kwenye kiuno cha mwanaume m,moja
Tunaombeana mabaya,wanasubili ufeli ili wakucheke
Kipindi niko secondary walimwambia baba anapoteza hela nitapata mimba tu....huku nilimalza Shule nikiwa bikira.
Mambo ni mengi, bai the Wei nawachukia ndugu zangu,
Ninaishi kama mkiwa......Kuna wakati Unapitia mambo makubwa maishani unatamani kumueleza mtu m,moja tu akusikilize lakini hayupo.
Natamani wanaume wote wanvefahamu Kua Kuzaa watoto kila mototo na mama yake ni mateso makubwa kwa mtoto
Wanawake wangejua kua kuzaa kila mtoto na baba yake ni mateso kwa mtoto
Wanawake wangejua kua kuzaa Kabla hujajipanga ni kumtesa mtoto
Wanawake wangetambua kua kuzaa Kabla ya ndoa ni mateso kwa mtoto
Basi wasingethubutu kuyafanya haya.
Maisha ninayoishi najua ni wazazi wangu waliyasababisha.
Maybe tungezaliwa baba m,moja na mama m,moja huenda tungekua na Familia yenye upendo.
Sijutii tena, kwasababu nitauumiza moyo wangu kwa vitu ambavyo siwezi kuvibadilisha
Nimejifunza kuyaishi maisha yangu bila uwepo wa ndugu yeyote,