Huu undugu wa kukutana kwenye misiba tu haufai

Huu undugu wa kukutana kwenye misiba tu haufai

Unakuta ndugu zako kabisa wa kuzaliwa nao, achilia mbali hao wa upande wa baba au mama mnakuwa hamna maelewano mazuri; kupeana fursa hakuna, wakati mwingine ata kujuliana hali mpaka mtafutane sana.

Ila ukitokea msiba sasa, ndio mnaanza kutafutana na kwenda kwa mbwembwe.

Kwa mtazamo wangu, undugu wa namna hii haufai; piga chini ujipambanie mwenyewe.​
KWA WAKRISTO WATANIELEWA

Waebrania 9:16-17
[16]Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
[17]Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.


Kwahiyo msifikiri mnajikusanya wenyewe! Mauti yoyote ndani ya familia na ukoo hasa hasa kifo cha mkuu wa kaya au kiongozi wa kimila, kuna kukabidhiana maagano yaliyojengwa juu ya mizimu na mashetani ambayo wakuu wa familia au ukoo wanajua. Wewe unaweza kuwa unaendesha maisha yako ama mazuri au mabaya! Sasa subiri patokee msiba wa kifamilia au kiukoo hautakuwa kama ulivyo! Mnapokusanyika mkala na kunywa na kucheza au kulia kuna maroho ya maagano ya mizimu na mashetani yanawavaa! Mengine yanaambatana na magonjwa ya kurithi, dhambi na tabia za kurithi kama ulevi, umalaya, ugomvi, manuksi, au mtu wa kukaa katika hiyo nafasi ya aliyekufa! NDO MAANA KWENYE MSIBA USIPOONEKANA WANAFAMILIA AU UKOO WANAKUTENGA! Haya mambo yako kwa makabila yoote hila WACHAGGA wanaongoza ndo maana kwa wachaga misiba ni ibada na sherehe!
 
Bora msibani unawaona

M kaka yanguuu akisiikia misibaaa haji anauliza min sh ngapi anawarushia mchango sikuhiohio mkipiga yoyote akijua namba zenu apokei..ngooo
Kuna jamaa yetu nae alikuwa kama kaka yako siku ya msiba wake nae alirushiwa hela tu.

Tokea siku hio amekuwa wa mbele kwenye kila shughuli🤣🤣🤣
 
KWELI KIUNA BAADHI YA NDUGU WANAUDHI SANA MNNILIKUWA KWA MCHANGO MMOJA WA SEND OFF MAJUZI

NAFIKA NASOMA KARATASI NAKUTA NDUGU MIN 100000 NKANGLIA BAJETI MIL 27

HIYU MPUUZI ANAKAA KWA NYUMBA YA KUPANGA CHUMBA CHA 50K KWA MWEXI ANATAKA LAANA...

SASA KUMBE NDAN KUNA WAPIGAJI WAMEJIPANGA..NKAANZA KUTOA USHAURI KUNAVITU MKIANDJKA WAKIONA WATU WANAWEZA WASIRUDI

KAREKEBISHEN BEI YA UKUMBI NA MENGINE NILIWAMBIA AISEE SIKUWA NA DATA KUFIKA NYUMBAN WASHA HIZO MSG ZAO NIMEKOMA NDUGU

MWINGINE AKAANDKKA USISEME SINA SEMA HUNA UKIJISIKIA TOA USIPOJISIKIA USITKE HAITUSAIDII MTOTO WA MAMA MDOGO NA MKUBWA HUYOO

SINA HAMU
 
Tatizo ni vijiba na viroho vya kinyongolilo. Familia ambazo zinajiweza huwezi shuhudia haya matatizo ila pale ambapo kuna magepu ndio shida huanzia.

Wabongo roho za kichawi tumeumbwa nazo by default tu. Baba mkubwa akiwa na shavu watoto wanasoma international watoto wa mdogo wake wa kiume wapo kayumba watoto wa dada yake kayumba. Mke wa baba mkubwa anaanza visa hataki watu wasogelee mume wake sababu watakula vya mumewe. Kila mtu anaikacha ile familia kwa kuona kwamba wanaringa sababu wana hela kumbe tatizo ni choyo ya mke.

Nasema hili nikiwa na uhakika sababu kabla ya ndugu kuanzisha familia huwa wanaelewanaga sana ila akishaingia mwanamke tu kati yao lazma mifarakano ianze. Upande wa mashangazi huwa sio pagumu sana maana wanaume wengi hatunaga viroho vya kisokolokwinyo kwenye kutoa misaada.
 
Nadhani wenzetu hawa watu wa Asia wameweza kulikwepa hili kwa kuishi na familia zao kwenye boma moja, hii nadhani inaondoa ule ubinafsi ambao huku kwetu umetawala. Nasi kama tutaweza kuishi na watoto wetu kwenye boma moja, waoe na waolewe na waishi pale pale hii dhambi ya kutofautiana tunaweza kuikimbia.
Asia walilikwepa kasumba hapa bongo unajua kwa nn hii ishu ?

Sikiliza ndugu yangu hapa bongo palikuwa na kasumba wala hakuna ushahidi eti kufanya kazi mkoa wa nyumbani utapata tabu , hakuna ushahidi ni imani za kijinga mara utasikia utarogwa huyo ni msomi anaamini kwamba atarogwa .

Hii kasumba ilisababisha watu wengi kutokomea mpaka nje cha nchi wale waliopata elimu mwanzoni , wengine kukimbilia mikoani ..Ajabu hata wabunge wengi hawaishi kweny majimbo yao wanaishi mbali kabisa .

Mimi upande wa mama wanaishi eneo moja wote wamesoma kwa elimu ya zamani ni mmoja tu mama hakufika mbali , ila wengine wote wapo serikalini wapo wanne , wanaishi mkoa mmoja japo walipangiwa vituo mikoani ila waliomba kurudi kwao wana maendeleo ..Watatu wanakaa sehemu moja si unajua zamani watu walikuwa wanapewa viwanja bure hata hekari 7 kikubwa usafirishe tu.

Basi ndani ya hekari saba babu kawapa wanae wamejenga wanaishi hapo , kila siku lazima wasalimiane .

Huku kwa baba ndio wameiga tabia za upareni kila mtu kakimbia kwake ,kiufupi hawajielewi.​
 
Cha Msingi Kuombe Dua sanaa

Imagine Mimi Na ndugu yetu wakike aliondoka home Tangu 2004 Mpaka leo Hatujui yuko wapi,Kapatwa na nn Na anafanya nn?
Tumeishasubiri Tuone kama atarudi lakini bado.
Babu mzaa baba yangu alizaliwa na wadogo zake wawili walikuwa mapacha , hapa mjini alibaki na mmoja ambaye aliolewa yule wmingine aliondoka kipind cha Waingereza miaka ya 50's huko maana alisomeshwa mpaka kwenda mpaka hapo hawakuwahi kuonana tena .

Alibaki na mmoja(Doto) ambaye alikufa mwaka 2003.
 
Na haya ndyo maisha ninayaishi....
Najuta kuzaliwa kwenye hii Familia,lakini ni vitu ambavyo siwezi kuvibadilisha.
Siku za mwanzo nilikua najutia na kuumia sana....Kuna wakati nilitakiwa kukubali kua sikujipangia,yaani nimezaliwa na kujikuta humo hivyo siwezi kubdilisha chochote..........

Mimi ndugu Zangu hatuwasiliani,maybe Tukutane kwenye matatizo.

Hawa siyo ndugu wa mbali, Hawa ni ndugu Zangu wa damu,tumetoka kwenye kiuno cha mwanaume m,moja

Tunaombeana mabaya,wanasubili ufeli ili wakucheke

Kipindi niko secondary walimwambia baba anapoteza hela nitapata mimba tu....huku nilimalza Shule nikiwa bikira.

Mambo ni mengi, bai the Wei nawachukia ndugu zangu,

Ninaishi kama mkiwa......Kuna wakati Unapitia mambo makubwa maishani unatamani kumueleza mtu m,moja tu akusikilize lakini hayupo.

Natamani wanaume wote wanvefahamu Kua Kuzaa watoto kila mototo na mama yake ni mateso makubwa kwa mtoto

Wanawake wangejua kua kuzaa kila mtoto na baba yake ni mateso kwa mtoto

Wanawake wangejua kua kuzaa Kabla hujajipanga ni kumtesa mtoto

Wanawake wangetambua kua kuzaa Kabla ya ndoa ni mateso kwa mtoto

Basi wasingethubutu kuyafanya haya.

Maisha ninayoishi najua ni wazazi wangu waliyasababisha.

Maybe tungezaliwa baba m,moja na mama m,moja huenda tungekua na Familia yenye upendo.

Sijutii tena, kwasababu nitauumiza moyo wangu kwa vitu ambavyo siwezi kuvibadilisha

Nimejifunza kuyaishi maisha yangu bila uwepo wa ndugu yeyote,
Wew ni kabila gan
 
Back
Top Bottom