Huu unyonge wa kushindwa kuongea mnapokereka wanaume unasababishwa na nini?

Huu unyonge wa kushindwa kuongea mnapokereka wanaume unasababishwa na nini?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1634387121345.png

Mwanaume mke wako amechelewa kurudi kazini unashindwa kuongea nae na kujua kilichotokea unanuna na kwenda kulala. Masikini binti wa watu hajui hata kama umekasirika.

Huyu hapa pichani anakereka kumuona mke wake ana chart kwenye simu, anashindwa kumwambia hisia zake amebaki kujikunyata huku akichemka kwa hasira.

Matatizo mengi ya mahusiano yanasababishwa na mawasiliano mabovu. Mdomo unepewa ili uweze kuwasiliana kirahisi. Kama mwenzako ana hasira tafuta jinsi ya kufikisha ujumbe umpate na aelewe kuwa ana kukera.

Kama unashindwa kuongea nae tumia texted massage, tumia mtu unae muamini afikishe ujumbe au hata barua. Tujifunze kuwasiliana katika mahusiano.
 
Mbona iko viseverser cc tunajua KE ndo wanapenda kukaa na dukuduku moyoni unaweza ufanye kitu ambacho hakimfrahishi badala ya kukwambia utaona anavuta midomo kama kenge kwa kununa tu na inaweza pita miaka na miaka anakaa na kinyongo moyoni ila wanaume anakuchana apoapo au nasema uongo ndugu zangu??
 
Kuna wanawake wenye matatizo haya pia. Hasa mwanaume anapokuwa main breadwinner anatoa tu amri hamna muda wa kujadiliana.
 
Daaah, wale tulio moja kwa moja tunaambiwa tuna mfumo dume ujue! Wanasema hatuko romantic and caring.

Sijui nachanganya mambo hapa au vipi, ila ukivaa ovyo, nakutimua on the spot, uko kitandani una-chat mi nijikunyate? Pengine na taa inawaka, ninune? Daaah
 
Wanaume tumeumbwa na uwezo mkubwa wa kuvumilia mateso, maumivu na hata kunyamzia mambo yanayotukera,
Tumeumbwa na maneno machache na kuwa na upendo mwingi na huruma sana kwa wanawake.......
BRETHREN, INABIDI TUJITAFAKARI SANA....KAMA HATUNA HIZI SIFA BAC TUZITAFUTE SISI KAMA WANAUME
 
Ww ndio uko viseverser moja ya sifa ya mwanaume ni kuwa na kifua kutunza Siri na mwanamke huwa hawezi kutunza Siri .
Mbona iko viseverser cc tunajua KE ndo wanapenda kukaa na dukuduku moyoni unaweza ufanye kitu ambacho hakimfrahishi badala ya kukwambia utaona anavuta midomo kama kenge kwa kununa tu na inaweza pita miaka na miaka anakaa na kinyongo moyoni ila wanaume anakuchana apoapo au nasema uongo ndugu zangu??
 
Kila binadamu na tabia yake, hao ni wanaume wenye tabia ya upole ndiyo wapo hivyo na huwezi wabadilisha ila nao pia hufunguka pale inapobidi. Binafsi kwangu hilo haliwezekani nakuambia kwa mdomo siku mbili tatu hakuna mabadiliko nakuambia kwa vitendo taratibu tu mpaka tunaelewana.
 
Kutojiamni kwa mwanaume. Malezi aliyolelewa hakujengwa kusema kinachomkera ama kumfurahisha.
Ni malezi ya kukaa kimya(kuvumilia). Tena anaambiwa mwanaume lazima uwe mvumilivu.
Malezi mabaya sana

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kama hao ukute mme hawezi kufanya lolote zaidi ya kukoroma tu maana angekuwa anaweza kazi mke asingejichelewesha hivyo anaona bora apoteze muda kidogo ili akifika tu asichelewe mbavu zikamuuma bure
 
Back
Top Bottom