Mwanaume mke wako amechelewa kurudi kazini unashindwa kuongea nae na kujua kilichotokea unanuna na kwenda kulala. Masikini binti wa watu hajui hata kama umekasirika.
Huyu hapa pichani anakereka kumuona mke wake ana chart kwenye simu, anashindwa kumwambia hisia zake amebaki kujikunyata huku akichemka kwa hasira.
Matatizo mengi ya mahusiano yanasababishwa na mawasiliano mabovu. Mdomo unepewa ili uweze kuwasiliana kirahisi. Kama mwenzako ana hasira tafuta jinsi ya kufikisha ujumbe umpate na aelewe kuwa ana kukera.
Kama unashindwa kuongea nae tumia texted massage, tumia mtu unae muamini afikishe ujumbe au hata barua. Tujifunze kuwasiliana katika mahusiano.