Huu upatu wa MTFE ni fursa kweli au mimi ndio naenda kugeuzwa fursa?

Naomba kuuliza je ni wote waliowekeza hela wamepigwa au kuna waliofanikiwa kuwithdraw? Kuna mshikaji wangu aliwekeza anasema yeye jana alifanikiwa kuwithdraw hajapigwa et baadhi ndio wamepigwa. Nimehisi anaficha nisimuone kalizwa
HAJATOA HATA 100 NAKUHAKIKISHIA.. lengo usimuonee Mjingaa wakati kiukweli ni Mjinga wa karneee kapigwaaa huyooo
 
Kila wakati huwa wanaanza na mbinu kama za kumtongoza mwanamke
Mara vizawadi, mara outing nk ila ukila mzigo na zawadi zinakata

Sasa na nyie mnaoingia hii biashara ni kuwa kwanza mnakuwa Chambo unarudishiwa vihela kwa mda ili na wewe ulete wengine na wao wanapewa pia wanaleta wengine na wewe unaamua kuongeza dau ili ziwe nyingi

Mchezo utaendelea ila jamaa wakishafika malengo yao na kujua sasa target imefika wanaanza kuzima data na ukituma email huwapati na watawazungusha mwisho wa siku unabaki na Jina la kampuni tu hata majina yao huyajui na ofisi zao huzijui

Watu wanalizwa kila leo ila wanaibuka wapya tena yaani wajinga hawaishi duniani
Kama sina hofu ya Mungu ningewaliza kila mwaka
 
Kweli nimeamini ukisikia kitu au mtu anasemwa huku soon kinahappen.Mtoa mada una machale
 
Watu hawaelewi, pamoja na kuibiwa Sana bado wanaendekeza ujinga. Kweli mjinga ni Faida ya mjanja.
 
Inatuvunja moyo [emoji174][emoji24] kutangaza kuwa tumetapeliwa. Matukio ya hivi majuzi na kukatizwa kwa huduma kwenye jukwaa kumezua wasiwasi mwingi miongoni mwa wafuasi wetu, hata hivyo tumehakikishiwa na viongozi wetu (Maafisa Mtendaji Mkuu na Wakaguzi wa Hesabu) kwamba masuala hayo yalisababishwa na uboreshaji.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukipata mapato kwenye jukwaa hili na hakuna kitu kilichokwenda kusini hadi tarehe 3 Agosti tulipojaribu kuondoa uondoaji wetu wa kila mwezi, na kufuatiwa na malalamiko mengine mengi kama haya duniani kote.

Tunawahimiza wawekezaji wasiwekeze tena katika MTFE na tunatafuta chaguo za kurejesha uwekezaji wetu uliofanywa na jumuiya ya Maldivian.

Tutaweka sasisho hapa pindi zitakapofika.

Chanzo kisicho rasmi kimetuthibitishia mmiliki halisi wa MTFE ni Masud Al Islam (jina linaweza kuwa pak), anayeishi Dubai, UAE. Mashirika mengi na watu binafsi wanaanza uchunguzi wao wenyewe kwenye jukwaa tunapochapisha hili.

Tunahimiza kila mtu asiwekeze tena katika MTFE.
[emoji17][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
I sincerely sympathize with those who lost their monies with this scheme. But since there was an 'office' based in Dar-es-Salaam can't they be sued for the loses? An apology does not sound appropriate??
 
Mheshimiwa Tajiri Karibu Jukwaani kwa Mrejesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…