Huu upepo wanaJF wa kurudisha watoto kayumba kutoka EM wala sio maamuzi binafsi ni basi tu ukata umekuwa mkali

Wameshtuka mapema
 
Mdogo wangu we kama unataka kumrudisha mtoto wako Kayumba wewe mrudishe tu hujachelewa na Hakuna ubaya wowote . Na mtoto wako atafika Hadi Chuo kikuu,sema Amen
Never bro, never.

Siwezi temebelea fortuner alafu eti anasoma matomboleee praimariii eti kisa jf nilipata ushauri hahahahahahahh
 
We kweli kiazi kwaiyo unadhani kuna sehemu utakuta watoto Bakhresa wanapanga foleni kwenye interview ya kuomba ajira ya mshahara wa laki 7 au wanalilia Boom pale Udsm kama nyie.
Huo mfano badilisha.
Wew somesha EM umenyeke kisawasawa alafu badae mtoto aje kuwa Winga kama mimi apa.
Ila Uwinga unalipa😀
 
Ofcoz mimi ni kiazii, lakini sizidi anaetoa mtoto em anapeleka kayumba wakati anaetembelea gari zuri na aanakula malaya bar
 
100% Fact. Mtoa Mada ameshindwa kufikiria kuhusu hili.

Kusomesha EM Sio kipimo cha utajiri
huwezi kufaham mtoa mada ameshafanya uchunguzi viongozi wote wa nchi na mabolozi wamepitia huko EM ndo maana anajaribu kutukumbusha...kwa tathmin aliyoifanya amegundua ukimsomesha mtoto EM kutoboa maisha ni kama kumsukuma mlevi..ila kama analenga matumizi ya pesa tu na kujitofautisha na waviwango vya chini hapo katumia matako kufikiri kuliko kichwa.
 
Hivi unafikiri hao decision makers wengi wao walisoma English Medium au International Schools? Angalia historia ya viongozi wengi wa serikali wengi wao wamesomea vijijini.
 
Niandikie majina ya hao wazazi nikawaandikishe baby class niwalipie ada niwasomeshe wao na watoto wao
 
Unampeleka mtoto EM alafu baadae anaungana na waserekale kwenye vyuo vya hapa ndani.

Kitu cha ziada ambacho atakuwa nacho ni kiingereza cha wastani.
 
Kiuhalisia hakuna CONNECTION yoyote atapata wewe kama huna hela usijisumbue kujitutumua misuli bure. Watu wakimaliza shule kila mtu anaelekea ustaarabu wake mwanao atabaki anasimulia tu nilisoma na fulani😀😀😀

Wekeza katika ujuzi, mtoto aende VETA kwenye hizi likizo za kumaliza darasa la saba,form 4,form 6 akachukue ujuzi( kulingana mfumo wetu wa maisha huu muda wa kusubir matokeo sio muda wa kupoteza muda na mapreform 1,5 au unakuta mwanafunzi mhitimu wa form 6 yupo tu mtaani anizurura badala ya kwenda VETA kuchukua ujuzi huu muda huwa ni LULU na ukiupoteza ndo imeisha hiyo).

Dunia ya leo ni ya watu wenye ujuzi.Kwenda nje ya nchi ni swala la maamuzi tu hakutegemei na kwamba ulisoma Feza au st. Kayumba.

Waandalie watoto urithi kwa kuwanunulia viwanja na mashamba ya miti ya mbao na matunda.Wanunulie watoto HISA na BONDS katika makampuni mbalimbali huu ndo utajiri wa kurithishana kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.Na sio kupoteza rasilimali kisha kuja kuomba ajira za serikali.

Mtaendelea kuona wahindi na waarabu kama magenius ila hawa watu ni wa kawaida tu sema wanafikra tofauti kuhusu mali na utajiri.
 
Hawana fedha hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…