Kabisa kumsomesha mtoto EMs ukimlipia ada mamilioni halafu mwisho WA siku anakuja kufanya mitihani inayosimamiwa na NECTA, halafu elimu ya chuo kikuu anaenda kuitafuta kwenye chuo kinachosimamiwa na TCU ni sawa tu kujenga gorofa kwenye hifadhi ya barabara au kando kando ya mto mkubwa, mwisho WA siku utalipoteza tu Hilo gorofa na hatimae utakuwa sawa tu wale ambao hawana nyumba.
Huku mitaaan waliosoma EMs na waliosoma government schools a.k.a kayumba schools, tofauti Yao ni kingereza tu Cha ku-comment mitandaoni.
Mtu kama ameamua kumpa mtoto wake elimu iliyo Bora basi ampe kilicho Bora mwanzo mwisho, yaani mtoto Yuko kindergarten tayari wewe mzazi huko unamuandalia kuja kusoma Stanford university au akishindwa sana basi hata Witwatersrand hapo south Africa... Mtu akienda na huu mlolongo kielimu sio rahisi kuja kuteseka.
Sasa wewe leo hii unajinadi mtoto wako hasomi Kayumba anasoma EMs halafu mwisho WA siku anakuja kuishia Udom au Teofilo Kisanji, kisha akitoka hapo na yeye anaanza kugombania ajira za TRA na hao waliosoma Kayumba sasa ni akili hiyo???