Mkuu umenifumbua jambo,hili la kujenga lodge,bar na kuzikodisha sikuwahi kuliwaza.1. Nunua maeneo/plots kwenye maeneo yanayokuwa, then uza baada ya kupanda thamani. Actually mwajiriwa anaweza kuwekeza kwenye real estate na kuona thamani ya uwekezaji wake.
2. Jenga nyumba za biashara, lodges, frames za biashara, halls na hata bars then kodishia watu wakupe pesa(considering huna mda wa kusimamia)
3. Fixed account, government bond na hizo UTT.
...usifungue duka la kuchuuza, utalizwa
Majengo yanakurudishia pesa taratibu sana,wanaokuja kula faida si wewe,ni watoto wako. Bado usumbufu wa wapangaji. Au unaweza kufafanua vizuri namna gani uwekezaji wa majengo unaweza kukulipa?Mwajiriwa Tanzania kama anajijuwa ni pesa za halali awekeze kwenye majengo tu.
Thamani ya jengo ni jengo lenyewe linapanda bei, na eneo linapanda bei.Majengo yanakurudishia pesa taratibu sana,wanaokuja kula faida si wewe,ni watoto wako. Bado usumbufu wa wapangaji. Au unaweza kufafanua vizuri namna gani uwekezaji wa majengo unaweza kukulipa?
Nakuelewa lakini nilitaka mchezo wa namba. Mfano umejenga nyumba ya wapangaji kwa milion 70, hapa umeweka wapangaji watatu kila mmoja anakupa 150k per month,jumla unapata 450k per month kwa uwekezaji wa milion 70.Thamani ya jengo ni jengo lenyewe linapanda bei, na eneo linapanda bei.
Tanzania bado hatujafikia viwango vya thamani kushuka kwenye real estate.
Ni ngumu san kumfahamisha mfanyuakazi kufanya biashara.
Sikushangai:
Ukimwekea nyani pesa na ndizi atachaguwa ndizi. Haelewi kuwa pesa zitanunuwa ndizi nyingi zaidi.
Ukimuonesha mfanyakazi biashara na kazi atachaguwa kazi. Haelewi kuwa biashara itazalisha kazi nyingi zaidi.
Msaada ,,sasa ijho UTT ndo nini mzee,?Nakubaliana na wewe mkuu,mimi nina akaunti UTT na biashara nilishajaribu....bado UTT ni bora sana.
Nenda google rafiki angu, kuna nyuzi nyingi hata humu jamii forum zinazoelezea kuhusu UTT. Kiufupi ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, unaweka hela yako, UTT wanawekeza hiyo hela alafu faida mnagawana, wewe unapata asilimia 10 ya hela uliyoweka kila mwezi. Ni uhakika hakuna utapeli sababu uko chini ya serikali.Msaada ,,sasa ijho UTT ndo nini mzee,?
Eeeh wanakupa 10% kila mwezi...aisee yaani nikiweka million mia kila mwezi wananipa ten million au nimeelewa vibayaNenda google rafiki angu, kuna nyuzi nyingi hata humu jamii forum zinazoelezea kuhusu UTT. Kiufupi ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, unaweka hela yako, UTT wanawekeza hiyo hela alafu faida mnagawana, wewe unapata asilimia 10 ya hela uliyoweka kila mwezi. Ni uhakika hakuna utapeli sababu uko chini ya serikali.
Naamini ujenzi wa nyumba za kupangisha hasa location ikiwa nzuri zina faida nzuri. Kwanza kodi za kila mwezi chukulia ni faida, jengo ulilojenga thamani yake inaendelea kupanda kila siku na pia unaweza kulitumia kama dhamana ya mkopo.Biashara nimeshajaribu tatu na zote zilinishinda,ni hela nilipoteza. Kwenye viwanja nakubaliana na wewe,lakini kwenye majengo nadhani ni mada fikirishi bado..Unaweka milion 60 yako kwenye nyumba,je ni lini utaona faida ya hiyo hela ulowekeza?
Ttzo ulilonalo au tulilonalo linaanzia hapo kwenye kuelewaNakuelewa lakini nilitaka mchezo wa namba. Mfano umejenga nyumba ya wapangaji kwa milion 70, hapa umeweka wapangaji watatu kila mmoja anakupa 150k per month,jumla unapata 450k per month kwa uwekezaji wa milion 70.
Kwa mwaka hii nyumba itakuingizia 5.4 milioni. Itachukua miaka 13 mpaka pesa yako irudi yote,alafu ndio uanze kula faida. Hapo hujaweka gharama za ukarabati mdogo na mkubwa,hujaweka usumbufu wa kulipwa kwa kuchelewa na baada ya miaka hiyo 13 nyumba inakuwa imeshachakaa inahitaji ukarabati..
Nilieleza umuhimu wa location ya nyumba, zaidi design ya nyumba ni muhimu pia. Kuna watu wanapiga parefu tu kwenye nyumba za kupanga (apartments).Biashara ya bar nimefanya pia, hii nayo unahitaji location nzuri na wadada flan hivi kama wahudumu.Kuna nyumba nilipewa nikarabati halafu nichukue kodi.
Ukarabati ulichukua Mil 8.
Ilinichukua miaka mi 3 kurudisha mil 8 kamili bila faida hata..!!!
Wakati huohuo nikafungua biashara ya Bar kwa mtaji wa mil 6 (nilishaifunga) ila mpaka inafungwa nilikuwa nimekusanya mil 15 (baada ya kutoa gharama zotee jumlisha kuhonga maaskari na maafisa wa serikali kama bwana afya) na kuiuza (kuifunga) kwa mil 6.7 kwa miaka miwili 2..!!!
Rudia tena statement yako???
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Aisee biashara ni ngumu mkuu nina mwaka wa 6 hata kibanda sina zaidi ya gofuMwanangu kaza.
Niko ajirani miaka 12
Niko biasharani miaka 5 (kubwa)
Ila biashara kama biashara nilianza 2015 ila ile kubwaa yenye faida kubwa ni 2019.
Nakiri, biashara ina upepo, kuna siku unauza balaaa, kuba siku majanga.
Ila si hata ajira, kuna miezi inapita ulambi posho.
Mzee baba mimi hapa na save itimie mil 30 nikimbie ajira ya CCM niwe full time enterpreneur.
We niwekee siti kitaa huko nakuja..!!!
#YNWA
#YANGA_BINGWA
kama Biashara gani boss?Kuna biashara zinalipa Balaaaaaa.
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Uko Mkoa gani?Sijui lolote kuhusu UTT, nikitaka kuwekeza naanzia wapi? Naenda benk au vipi..
Mkuu uko serious kweli?10 % kila mwezi?Nenda google rafiki angu, kuna nyuzi nyingi hata humu jamii forum zinazoelezea kuhusu UTT. Kiufupi ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, unaweka hela yako, UTT wanawekeza hiyo hela alafu faida mnagawana, wewe unapata asilimia 10 ya hela uliyoweka kila mwezi. Ni uhakika hakuna utapeli sababu uko chini ya serikali.
Hatari kweli kweli🤣🤣
Tuendelee kuwapa elimu.
#YNWA
#YANGA_BINGWA