Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

1. Nunua maeneo/plots kwenye maeneo yanayokuwa, then uza baada ya kupanda thamani. Actually mwajiriwa anaweza kuwekeza kwenye real estate na kuona thamani ya uwekezaji wake.

2. Jenga nyumba za biashara, lodges, frames za biashara, halls na hata bars then kodishia watu wakupe pesa(considering huna mda wa kusimamia)

3. Fixed account, government bond na hizo UTT.

...usifungue duka la kuchuuza, utalizwa
 
Mkuu umenifumbua jambo,hili la kujenga lodge,bar na kuzikodisha sikuwahi kuliwaza.
Uwekezaji wa nyumba za biashara bado nafikiria,inaonekana return ya pesa ni ngumu sana na uwekezaji ni mkubwa.
 
Mwajiriwa Tanzania kama anajijuwa ni pesa za halali awekeze kwenye majengo tu.
Majengo yanakurudishia pesa taratibu sana,wanaokuja kula faida si wewe,ni watoto wako. Bado usumbufu wa wapangaji. Au unaweza kufafanua vizuri namna gani uwekezaji wa majengo unaweza kukulipa?
 
Majengo yanakurudishia pesa taratibu sana,wanaokuja kula faida si wewe,ni watoto wako. Bado usumbufu wa wapangaji. Au unaweza kufafanua vizuri namna gani uwekezaji wa majengo unaweza kukulipa?
Thamani ya jengo ni jengo lenyewe linapanda bei, na eneo linapanda bei.

Tanzania bado hatujafikia viwango vya thamani kushuka kwenye real estate.

Ni ngumu san kumfahamisha mfanyuakazi kufanya biashara.

Sikushangai:

Ukimwekea nyani pesa na ndizi atachaguwa ndizi. Haelewi kuwa pesa zitanunuwa ndizi nyingi zaidi.

Ukimuonesha mfanyakazi biashara na kazi atachaguwa kazi. Haelewi kuwa biashara itazalisha kazi nyingi zaidi.
 
Nakuelewa lakini nilitaka mchezo wa namba. Mfano umejenga nyumba ya wapangaji kwa milion 70, hapa umeweka wapangaji watatu kila mmoja anakupa 150k per month,jumla unapata 450k per month kwa uwekezaji wa milion 70.
Kwa mwaka hii nyumba itakuingizia 5.4 milioni. Itachukua miaka 13 mpaka pesa yako irudi yote,alafu ndio uanze kula faida. Hapo hujaweka gharama za ukarabati mdogo na mkubwa,hujaweka usumbufu wa kulipwa kwa kuchelewa na baada ya miaka hiyo 13 nyumba inakuwa imeshachakaa inahitaji ukarabati..
 
Msaada ,,sasa ijho UTT ndo nini mzee,?
Nenda google rafiki angu, kuna nyuzi nyingi hata humu jamii forum zinazoelezea kuhusu UTT. Kiufupi ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, unaweka hela yako, UTT wanawekeza hiyo hela alafu faida mnagawana, wewe unapata asilimia 10 ya hela uliyoweka kila mwezi. Ni uhakika hakuna utapeli sababu uko chini ya serikali.
 
Eeeh wanakupa 10% kila mwezi...aisee yaani nikiweka million mia kila mwezi wananipa ten million au nimeelewa vibaya
 
Biashara nimeshajaribu tatu na zote zilinishinda,ni hela nilipoteza. Kwenye viwanja nakubaliana na wewe,lakini kwenye majengo nadhani ni mada fikirishi bado..Unaweka milion 60 yako kwenye nyumba,je ni lini utaona faida ya hiyo hela ulowekeza?
Naamini ujenzi wa nyumba za kupangisha hasa location ikiwa nzuri zina faida nzuri. Kwanza kodi za kila mwezi chukulia ni faida, jengo ulilojenga thamani yake inaendelea kupanda kila siku na pia unaweza kulitumia kama dhamana ya mkopo.
 
Ukisoma huu Uzi utaamini kuwa nchi yetu Ina gap la elimu ya fedha na uchumi Kwa raia wake walau Kwa level ya chini kabisa.

Watu hawajui maana ya uwekezaji na biashara. Watu wanashindwa kutofautisha Mutual funds kama UTT Amis,Fixed Deposit,Government Bonds. Na real estate.

Financial literacy ni muhimu sana sana sana.

Maoni yangu.

Sio Kila mtu anaweza kufanya BIASHARA ila Kila mtu anaweza KUWEKEZA. Cha msingi ni kujua eneo Gani zuri la kuwekeza.

Jambo la msingi iwe kwenye uwekezaji au biashara ni kuangalia inflation rate za nchi. Kabla hujaweka Hela lolote angalia inflation rate ya Hela yako. Kwa lugha ya kawaida inflation rate ni kushuka thamani fedha ya nchi. Kwa mujibu wa BOT inflation rate ya Tanzania ni 3.1%. Maana yake kama unaweka Kwa mwaka 1,000,000 baada ya mwaka hiyo milion 1 itakuwa imeshuka Kwa 3.1%.

Sasa jambo la msingi ni wewe kujua huo uuwekezaji wako utaitunza pesa yako ibaki na thamani ile ile Baada ya mwaka ? ... Hapo ndio tunaangalia interest rate unazolipwa kwenye huo uuwekezaji.

Kwa mfano Government Bonds wanalipa 12% Kwa mwaka Kwa kiasi ulichowezeka. Maana yake hata kama Kuna inflation ya 3.1%. ila wao watakupa gawio la 12% maana yake hapo ni faida ya 9%. Hii inakuwa imesaidia Hela yako kutoliwa na inflation.

Sasa uwekezaji ni lazima ujue haya. Usije kuweka hela sehemu inakuwa inaliwa na inflation kwasababu shilingi Kila siku inashuka thamani dhidi ya dollar. Huo uuwekezaji utalinda thamani ya shilingi yako ? Maana milion ya Leo 2024 haitakuwa na thamani mwaka 2030.

Same applied to business.

Kwenye biashara Kwa Tanzania, ushauri wangu;

Kwanza mjue katika biashara 10 mpya ni biashara 1 au 2 na zikizidi sana ni 3 ndio zinaweza kusimama zingine zote huishia kufeli baada ya miaka kadhaa. Hili kabisa mjue.

Nitaendelea
 
Mwaka jana biashara ilipamba moto nikaona bora nikomae na biashara niachane na mambo za kuajiriwa

Mwaka huu upepo umegeuka biashara ngumu kuliko jiwe hadi natamani ajira. Nishaurini wakuu

Ninaingiza net profit ya 800k kwa mwezi(hapo nimetoa gharama zote) niendelee kukaza au niajiriwe?
 
Nakuelewa lakini nilitaka mchezo wa namba. Mfano umejenga nyumba ya wapangaji kwa milion 70, hapa umeweka wapangaji watatu kila mmoja anakupa 150k per month,jumla unapata 450k per month kwa uwekezaji wa milion 70.
Kwa mwaka hii nyumba itakuingizia 5.4 milioni. Itachukua miaka 13 mpaka pesa yako irudi yote,alafu ndio uanze kula faida. Hapo hujaweka gharama za ukarabati mdogo na mkubwa,hujaweka usumbufu wa kulipwa kwa kuchelewa na baada ya miaka hiyo 13 nyumba inakuwa imeshachakaa inahitaji ukarabati..
Ttzo ulilonalo au tulilonalo linaanzia hapo kwenye kuelewa
Kuna biashara Na kuna uwekezaji...sasa unapoamua nini cha kufanya kati ya biashara Na uwekezaji Na ndo ujue namna ya faida inavyopatikana
Kwenye uwekezaji ni mbio ndefu Na biashara Na mbio fupi

Turudi kwenye hizo hesabu za nyumba ,kwanza tukubaliane kuwa nyumba ni uwekezaji Na thamani yake ni kwenye jengo Na ardhi iliyobeba jengo......hivyo kadiri unavyopokea kodi hesabu ndo faida ya uwekezaji wako kwa kipindi kilichopo .Suala la kuirudisha fedha uliyowekeza ni pale utakapouza hilo jengo Na si ktk makusanyo ya kodi za pango

Mfano mzuri wa kukuonyesha huo uwekezaji unalipia na ni mzuri ni kwamba ulikusanya mapato ya miaka mitano Na baada ya hapo ukaamua kuliuza unahisi utaliuza kwa milioni 70 ulizojengea !? Na ikiwa utaliuza zaidi ya gharama uliyowekeza Na ilhali ulishakusanyavzaidi ya 30% ya gharama za uwekezaji huoni kuwa ni Jambo lenye faida!??

Karibu kwenye real estate Na hutojutia,tunafanya maajabu sana kwenye huo uwekezaji
 
Kuna nyumba nilipewa nikarabati halafu nichukue kodi.
Ukarabati ulichukua Mil 8.
Ilinichukua miaka mi 3 kurudisha mil 8 kamili bila faida hata..!!!

Wakati huohuo nikafungua biashara ya Bar kwa mtaji wa mil 6 (nilishaifunga) ila mpaka inafungwa nilikuwa nimekusanya mil 15 (baada ya kutoa gharama zotee jumlisha kuhonga maaskari na maafisa wa serikali kama bwana afya) na kuiuza (kuifunga) kwa mil 6.7 kwa miaka miwili 2..!!!

Rudia tena statement yako???

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Nilieleza umuhimu wa location ya nyumba, zaidi design ya nyumba ni muhimu pia. Kuna watu wanapiga parefu tu kwenye nyumba za kupanga (apartments).Biashara ya bar nimefanya pia, hii nayo unahitaji location nzuri na wadada flan hivi kama wahudumu.
 
Mwanangu kaza.
Niko ajirani miaka 12
Niko biasharani miaka 5 (kubwa)
Ila biashara kama biashara nilianza 2015 ila ile kubwaa yenye faida kubwa ni 2019.

Nakiri, biashara ina upepo, kuna siku unauza balaaa, kuba siku majanga.

Ila si hata ajira, kuna miezi inapita ulambi posho.

Mzee baba mimi hapa na save itimie mil 30 nikimbie ajira ya CCM niwe full time enterpreneur.

We niwekee siti kitaa huko nakuja..!!!

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Aisee biashara ni ngumu mkuu nina mwaka wa 6 hata kibanda sina zaidi ya gofu
 
Sijui lolote kuhusu UTT, nikitaka kuwekeza naanzia wapi? Naenda benk au vipi..
 
Nenda google rafiki angu, kuna nyuzi nyingi hata humu jamii forum zinazoelezea kuhusu UTT. Kiufupi ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja, unaweka hela yako, UTT wanawekeza hiyo hela alafu faida mnagawana, wewe unapata asilimia 10 ya hela uliyoweka kila mwezi. Ni uhakika hakuna utapeli sababu uko chini ya serikali.
Mkuu uko serious kweli?10 % kila mwezi?

Nadhani kila mtu angeweka huko.
 
Back
Top Bottom